KERO DED Lushoto tusaidie tutoke CWT

KERO DED Lushoto tusaidie tutoke CWT

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
  • Tags Tags
    cwt
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwalimu kutoka tarafa ya Mlola, Lushoto DC.

Mkurugenzi Mtendaji Lushoto DC tunaomba utusaidie walimu tulioandika barua za kujitoa CWT na kuhamia CHAKUHAWATA, ofisi ya utumishi inasuasua kushughulikia barua zetu kwa zaidi ya miezi tisa sasa licha ya kufuatilia mara nyingi tangu mwezi Januari mwaka huu.

Wengi tuliandika barua hizo tangu Novemba mwaka jana lakini mpaka mwezi Julai mwaka huu barua hizo hazijafanyiwa kazi.

Tulikuja ofisi kwako mara tatu lakini tuliambiwa haupo ofisini. Kutokana na jiografia ya wilaya ya Lushoto tunatumia gharama kubwa za usafiri karibu kila mwezi kufuatilia utekelezaji wa suala hili ambalo ni haki yetu kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.

Hivyo tunaomba ulisimamie ili haki yetu iweze kupatikana.
 
Back
Top Bottom