Deci; . Haukua mradi wa serekali?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Deci; . Haukua mradi wa serekali?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Emma Lukosi, Sep 16, 2010.

 1. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu wanajamvi leo najitokeza tena kuzungumzia swala zima la wizi uliofanywa na serikali ya chama chao cha mapinduzi kupitia kiji mini organization walicho kipa jina la DECI.
  Wakati maswala mazima ya shughuli za DECI zikiendelea watu wakipanda pesa na kupewa risiti zao huku vyombo vya habari vikikaa kimya kusubiri watu wajae mtegoni, serikali ilikua wapi!?, kwani iliendesha shughuli zake kwa takribani karibu miaka mitatu. Swali la msingi “hivi ile taasisi ingekua inauza silaha ni watu wangapi wangekua wanamiliki machine guns?, je kungekua kunauzwa sumu ni watanzania wangapi wangepoteza maisha yao?. Hii inazihirisha moja kwa moja kuwa serekali kwa namna moja au nyingine ilikua inahusika kwa vigezo vifuatavyo: Kwanza katika jengo lao la DECI kulikua na askari wa usalama wa raia wa Tanzania ambao walikua wanalinda, je kibali walipata wapi na walikua wakilinda nini?. Ina maana serikali ilikua ikifahamu wazi nini ambacho kilikua kinaendelea. Je baada ya serikali kuzikamata zile fedha hadi leo mbona malipo hayafanyiki kwa wahanga wa tukio?. Ifahamike kua serikali ya ccm ililazimika kusitisha zoezi zima la utapeli wao wa DECI baada ya kuona Watumishi wengi wa Uma wakitoa ela za serikali na kwenda kuzipanda kama walivyokua wakifanya wahasibu kutoka serikalini.
  Nmaliza kwa kusema “Hatuoni kwa sababau sio vipofu ila tumefunga macho”. Alietufunga na Atufungue.
   
Loading...