Death and immortality; Is there life after death?

Death and immortality; Is there life after death?

Kwa hiyo kitendo cha kufa je nini kinakufa,lakini unaposema ubongo ni pumbao usisahau kuwa our consciousness creates the universe bila hii consciousnesses hauwezi kutambua uwepo wako hapa duniani.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kufariki ni neno la kiarabu lililotokana na neno faraka maana yake kutengana so kutengana baina ya mwili na roho
Nikisema brain ni pumbazo nna maana nna maana kitengeza illusion emulation na hiyo illusion ni specific kwa kila mtu.
 
Habari za masiku ma GT.

Is there life after death?
Hili ni swali ambalo pengine tumekuwa tukijiuliza lakini kwa bahati mbaya haujapata conclusion,hivyo naliweka javni hapa kwa GT ili kulichambua na ikiwezekana kupata ukweli.

Kabla nitaweka mkasa mfupi wa kweli kabisa unaonihusu.
Wiki iliyopita nilipata taarifa ya msiba wa Baba yangu mkubwa hivyo ilinilazimu huko nilipokuwa(mkoani) nirudi ili nishiriki katika ibada hii ya mazishi.Nilipofika nyumbani ambako msiba ulikuwepo nilikabidhiwa jukumu ambalo kwangu lilikuwa gumu sana na hii ni kwa sababu ni mara yangu ya kwanza.Nilitakiwa niulinde mwili wa marehemu kwa wakati wa usiku hadi asubuhi bila mimi mlinzi kulala hata lepe la usingizi.Unajuwa kutokana na stori nyingi sana zinazohusu maiti zina ogofya nilipata na woga usio na mfano ile siku sitaweza isahau katika maisha yangu.
Mwili wa marehem Baba yangu mkubwa ulikuwa pembeni na mimi nilikaa ubavuni mwake kwa usiku huu,lakini kilichonitisha zaidi umeme haukuwepo kulikuwa na giza la kutisha.
Lakini nilijikaza hadi asubuhi,kulipokucha tuliendelea na shughuli za mazishi,nashukuru tulizika salama kabisa bila tatizo lolote lile.
Baada ya mazishi yale nilijiuliza maswali mengi sana ambayo leo niyaweka kwenu tujadili kwa mapana yake.
Wakati tunazika yule kiongozi wa dini alitoa darsa fupi pale msibani kuwa huyu marehemu ipo siku atafufuliwa na mwili mpya ili kulipwa matendo yake aliyofanya akiwa duniani.Nilipatwa na mshtuko sana inakuwaje mwili ambao utaliwa na funza na kubaki mifupa ukavalishwa tena nyama mpya,je huyo mtu akifufuliwa atakuwa ni yuleyule wa duniani mwenye malengo,akili,mind zilezile?

Ndipo nilipoamua kuandika mada hii.

Death and immortality.
Is there life after death?
Death is the permanent cessation of all biological function that sustain a living organism while
Immortality involves freedom from death.

Ubongo ndio unaratibu shughuli zote za mwili hivyo kwa ufahamu wangu pindi mtu anapofariki ubongo unakuwa umeshindwa kufanya kazi na mwili mtu nakuwa amepoteza maisha.Kufa kwa ubongo ndipo unapelekea sehemu zote za mwili/viungo kufa.
Hivyo kufa ni kitendo cha ubongo kushindwa kufanya kazi.
Conscious awareness tuliyonayo inatokana na ubongo,Hii consciousnesses ndio huu uhai tulionao ambao huletwa na ubongo.Pindi ubongo unapokufa/kushindwa kufanya kazi kitendo hiki tunaita kifo.

Kama mtu akifa hawezi tena kuwa hai tena re~creation kwa sababu ubongo unakuwa umekufa na kuoza tayari.

Lakini kuna nadharia kuwa tunapokufa tutafufuliwa katika mwili mpya(resurrection) God re-creation.
Katika nadharia hii based kwenye mwili,nafasi,roho.Kuwa kifo ni kile kitendo cha mwili na roho kutengana,hivyo mwili unabaki hapahapa duniani tunazika,kochoma it depends na mila na tamaduni za jamii husika lakini roho inaenda kwa Mungu.So binadam ni divine energy(roho) hivyo roho inaishi milele haifi immorty.

Roho inapotengana na mwili inaenda kuishi kwa Mungu ikisubiri mwili wake siku ya ufufuo(resurrection) ili ilipwe kwa matendo yake ya kule duniani.
Katika nadharia hii Mungu ndiye muumba na yeye ndiye atakaye urudisha uhai tena kwa viumbe wake kwa kuumba tena.

Lakini nadharia hii imejaa maswali mengi ambayo hayana majibu.
Maswali hayo ni kama vile
a)Soul na Ubongo upi unaratibu consciousnesses katika mwili wa binadam?
b)kama jibu ni ubongo,Je mwili unapotengana na roho na roho kwenda kwa Mungu mwili(ubongo wake)kubaki duniani hivyo kuoza na kupotea.Umbaji huu wa pili utaweza kumfufua binadamu yule yule wa awali?
Ebu angalia~Ili mtu A awe ni sawa mtu B lazima watu hawa wafanane vilevile katika malengo,ufahamu,mindset,mitazamo yao.
Mambo hayo hapo juu huongozwa na brain(ubongo).
c)Je wakati mwili upo ukiharibika hapa duniani roho itakuwa inafanya nini huko ilipo?
d)Roho inaweza kuishi bila mwili?
,kama inaweza kwanini Mungu ajihangaishe kuumba tena viumbe upya wakati roho inajitosheleza.
e)Roho na mwili kipi kilianza kabla?

Conclusion.From above arguments kifo ni kifo hakuna maisha mengine baada ya kufa hakuna.
Karibuni.......




iPhone 7plus
Katika mwili wa binadamu akili ipo wapi ?

Unajifunza nini unapo muona chizi,punguani,mwandawazimu ?

Unaweza kataa ya kuwa hitimisho lako limehengeka katika ujinga ?

Nipo ......
 
Roho (pumzi ya uhai ) inapotoka inakuwa mzimu katika ulimwengu wa roho . Kabla ya hizi dini za wazungu , mababu walikuwa wanaomba mizimu na wanafanikiwa . Mf . Ukame ukizidi wanaomba mizimu na mvua inanyesha ila ukitumia hizi dini zao hata upige magoti mpaka yachubuke hupati majibu kama ya mizimu . Basi maisha baada ya kifo yapo ila kwa mfumo mwingine .

Sent using Jamii Forums mobile app

Upi huo mfumo ukiachana na hizi nadharia mbili.Je binadam aliyekufa na kuoza atafufuliwa na kurudishiwa roho yake


Sent using Jamii Forums mobile app
 
The truth sits upon the lips of dying man.siku ukifa ndio utajua ukweli wote.vinginevyo hapa duniani tutadanganyana tu.kila mtu atakuja na nadharia yake kuhusu kifo but yote ni uongo mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Dead tells no tale.Ni kweli dying man ndiye anaeujuwa ukweli wa huko aliko kupo katika hali gani.Lakini hii haifanyi tuweze ku jihoji na kupata japo mwanga kuhusu safari yenye utata


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unauliza kitu ambacho wewe mwenyewe hauna maarifa nacho.
Kwa upande wangu mimi sijuwi akili ni nini hivyo kujibu swali lako itakuwa ngumu sana.


Sent using Jamii Forums mobile app

Nakusaidia ili uthibitishe kauli yako.

Akili ni uwezo kuyadiriki maarifa,fikra,mawazo.

Sasa jibu maswali yangu,niliyokuuliza hukk nyuma.

Nipo .....
 
Katika mwili wa binadamu akili ipo wapi ?kwa mujibu wa maelezo yako basi akili ipo katika ubongo.

Unajifunza nini unapo muona chizi,punguani,mwandawazimu ?Hakuna ninachojifunza pindi niwaonapo hawa watu ila nadhani hata wao pia wanatuona sisi hatupo sawa.

Unaweza kataa ya kuwa hitimisho lako limehengeka katika ujinga ?Kama hitimisho langu ni ujinga ebu weka lako liwe mandala.
Lakini haujajibu hata swali langu moja kuhusu roho na mwili hapo huu.

Nipo ......




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pia ukumbuke sio watu wote wakifa wanaoza inategemea na matendo yako hapa duniani kuna watu Mwenyezi Mungu ameharamisha udongo usiozeshe mili yao mpk siku ya hukumu mfano yupo firauni wa Misri japo hakuzikwa ila ajaoza na wala hanuki pia mwaka jana Indonesia kulikua na upanuzi wa barabara so ikabidi makaburi kufukuliwa basi miongoni mwa makaburi yaliofukuliwa lilikua kaburi ya Imaam wa msikiti ambaye alifariki miaka kumi iliyopita lakini alikua kama ndo kazikwa leo leo bimana alikuwa bado mwili wa moto, namalizia mambo haya yanategemea sn na imaan yako jinsi inavyokutuma, na mapokeo yake. kuna kisa cha watu wa pangoni ambao walikuwa saba waliweza kulala miaka 309 bila kufa wala kuzeeka walipoamka walijikuta kama wamelala dakika tu kisa kilitokea kostantinopoo Uturuki ya leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili ni nini tuanze hapo kabla sijajibu swali lako


Sent using Jamii Forums mobile app
Akili kwa maana ya "mind" kwa Kiingereza. Mtu akifariki, ubongo na mwili huoza. Uwepo wa "akili" au "mind" unategemea uwepo wa ubongo. Kama ubongo ukiharibika, ukidhoofika, au ukafa basi akili nayo inaathiriwa kulingana na hali ya ubongo. Kulingana na elimu ya Fizikia, hakuna maisha baada ya kifo.
 
Hivi unafikiri semen in just maji, mule kuna cells(sperm) ambazo huenda kurutubisha yai la kike hivyo kupatikana mtoto.

Na hii sio unique kwa binadamu tu hata kwa wanyama.

Na si lazima iwe kwenye tumbo la mwanamke kwa sababu wanasayansi wameweza kufanya huo muunganiko wa sperm na egg in laboratory.

In all account science keeps winning over this mythical stories that's why there are no ambulance in mosques or churches.
Sasa nimetula wacha nianze kuchangia.

Kwa kustaajabu kwako kwamba mtu kaoza ardhini vipi atarudi tena kuwa mzima?
Hukuanza kusema weye bali wameanza zamani kusema watu huko nyuma..

Nanukuu Qurani

أإذا متنا وكنا ترابا وعظاما أإنا لمبعوثون

[ ASS'AFFAT - 16 ]
Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?

أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ
(ASS'AFFAT - 17)
Hata baba zetu wa zamani?
قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَاخِرُونَ

(ASS'AFFAT - 18)
Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ

(ASS'AFFAT - 19)
Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
وَقَالُوا يَا وَيْلَنَا هَـٰذَا يَوْمُ الدِّينِ

(ASS'AFFAT - 20)
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.
هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ

(ASS'AFFAT - 21)
Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha.

Yani wewe ukifa hata uoze vipi lazima ufufuliwe tu mkuu,huu ukweli mchungu sana yani,unawakera watu ambao wanapenda uvivu.

Sasa baada ya utangulizi huo na mimi nianze kuuliza kwa kuanzia tuu.

" hivi kati ya maji kugeuka na kuwa mtu na kati ya mifupa na nyama iliyooza kugeuka kuwa mtu kipi ni rahisi zaidi kufanyika akatokea mtu?"
 
Namshukuru mungu ,kuwa muislama ,sababu yote tunafundishwa nakuambiwa baada ya kifo kuna ufufuo na hesabu ,sasa hapa nimimi mwenyewe tu ,kufanya ibada au la , uzuri wake hata hao wanaopinga wanakufa kama ,sisi alafu wanapumbazana ,hakuna malipo, kumbe wanafanya kazi ya shetani ,siku ya hukumu ndio kuni za motoni , mungu tupe waislam mwisho mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waga najiulizaga sana, hivi aliyekufa mwaka 2 or let say mwaka 100 atafufuliwa siku sawa na aliyekufa mwaka 2000.? Au ni kamba tu tunalishana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii sasa chai tena ya tangawizi, alafu ebu fatilia vizuri hiyo stori ya firaun ndio uje tena
Mkuu pia ukumbuke sio watu wote wakifa wanaoza inategemea na matendo yako hapa duniani kuna watu Mwenyezi Mungu ameharamisha udongo usiozeshe mili yao mpk siku ya hukumu mfano yupo firauni wa Misri japo hakuzikwa ila ajaoza na wala hanuki pia mwaka jana Indonesia kulikua na upanuzi wa barabara so ikabidi makaburi kufukuliwa basi miongoni mwa makaburi yaliofukuliwa lilikua kaburi ya Imaam wa msikiti ambaye alifariki miaka kumi iliyopita lakini alikua kama ndo kazikwa leo leo bimana alikuwa bado mwili wa moto, namalizia mambo haya yanategemea sn na imaan yako jinsi inavyokutuma, na mapokeo yake. kuna kisa cha watu wa pangoni ambao walikuwa saba waliweza kulala miaka 309 bila kufa wala kuzeeka walipoamka walijikuta kama wamelala dakika tu kisa kilitokea kostantinopoo Uturuki ya leo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namshukuru mungu ,kuwa muislama ,sababu yote tunafundishwa nakuambiwa baada ya kifo kuna ufufuo na hesabu ,sasa hapa nimimi mwenyewe tu ,kufanya ibada au la , uzuri wake hata hao wanaopinga wanakufa kama ,sisi alafu wanapumbazana ,hakuna malipo, kumbe wanafanya kazi ya shetani ,siku ya hukumu ndio kuni za motoni , mungu tupe waislam mwisho mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna moto mkuu,ishi kwa amani kabisa mpaka pale kifo kitakapo kufikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom