Pure_sapiens
JF-Expert Member
- Dec 25, 2016
- 2,245
- 2,128
Habari za masiku ma GT.
Is there life after death?
Hili ni swali ambalo pengine tumekuwa tukijiuliza lakini kwa bahati mbaya haujapata conclusion,hivyo naliweka javni hapa kwa GT ili kulichambua na ikiwezekana kupata ukweli.
Kabla nitaweka mkasa mfupi wa kweli kabisa unaonihusu.
Wiki iliyopita nilipata taarifa ya msiba wa Baba yangu mkubwa hivyo ilinilazimu huko nilipokuwa(mkoani) nirudi ili nishiriki katika ibada hii ya mazishi.Nilipofika nyumbani ambako msiba ulikuwepo nilikabidhiwa jukumu ambalo kwangu lilikuwa gumu sana na hii ni kwa sababu ni mara yangu ya kwanza.Nilitakiwa niulinde mwili wa marehemu kwa wakati wa usiku hadi asubuhi bila mimi mlinzi kulala hata lepe la usingizi.Unajuwa kutokana na stori nyingi sana zinazohusu maiti zina ogofya nilipata na woga usio na mfano ile siku sitaweza isahau katika maisha yangu.
Mwili wa marehem Baba yangu mkubwa ulikuwa pembeni na mimi nilikaa ubavuni mwake kwa usiku huu,lakini kilichonitisha zaidi umeme haukuwepo kulikuwa na giza la kutisha.
Lakini nilijikaza hadi asubuhi,kulipokucha tuliendelea na shughuli za mazishi,nashukuru tulizika salama kabisa bila tatizo lolote lile.
Baada ya mazishi yale nilijiuliza maswali mengi sana ambayo leo niyaweka kwenu tujadili kwa mapana yake.
Wakati tunazika yule kiongozi wa dini alitoa darsa fupi pale msibani kuwa huyu marehemu ipo siku atafufuliwa na mwili mpya ili kulipwa matendo yake aliyofanya akiwa duniani.Nilipatwa na mshtuko sana inakuwaje mwili ambao utaliwa na funza na kubaki mifupa ukavalishwa tena nyama mpya,je huyo mtu akifufuliwa atakuwa ni yuleyule wa duniani mwenye malengo,akili,mind zilezile?
Ndipo nilipoamua kuandika mada hii.
Death and immortality.
Is there life after death?
Death is the permanent cessation of all biological function that sustain a living organism while
Immortality involves freedom from death.
Ubongo ndio unaratibu shughuli zote za mwili hivyo kwa ufahamu wangu pindi mtu anapofariki ubongo unakuwa umeshindwa kufanya kazi na mwili mtu nakuwa amepoteza maisha.Kufa kwa ubongo ndipo unapelekea sehemu zote za mwili/viungo kufa.
Hivyo kufa ni kitendo cha ubongo kushindwa kufanya kazi.
Conscious awareness tuliyonayo inatokana na ubongo,Hii consciousnesses ndio huu uhai tulionao ambao huletwa na ubongo.Pindi ubongo unapokufa/kushindwa kufanya kazi kitendo hiki tunaita kifo.
Kama mtu akifa hawezi tena kuwa hai tena re~creation kwa sababu ubongo unakuwa umekufa na kuoza tayari.
Lakini kuna nadharia kuwa tunapokufa tutafufuliwa katika mwili mpya(resurrection) God re-creation.
Katika nadharia hii based kwenye mwili,nafasi,roho.Kuwa kifo ni kile kitendo cha mwili na roho kutengana,hivyo mwili unabaki hapahapa duniani tunazika,kochoma it depends na mila na tamaduni za jamii husika lakini roho inaenda kwa Mungu.So binadam ni divine energy(roho) hivyo roho inaishi milele haifi immorty.
Roho inapotengana na mwili inaenda kuishi kwa Mungu ikisubiri mwili wake siku ya ufufuo(resurrection) ili ilipwe kwa matendo yake ya kule duniani.
Katika nadharia hii Mungu ndiye muumba na yeye ndiye atakaye urudisha uhai tena kwa viumbe wake kwa kuumba tena.
Lakini nadharia hii imejaa maswali mengi ambayo hayana majibu.
Maswali hayo ni kama vile
a)Soul na Ubongo upi unaratibu consciousnesses katika mwili wa binadam?
b)kama jibu ni ubongo,Je mwili unapotengana na roho na roho kwenda kwa Mungu mwili(ubongo wake)kubaki duniani hivyo kuoza na kupotea.Umbaji huu wa pili utaweza kumfufua binadamu yule yule wa awali?
Ebu angalia~Ili mtu A awe ni sawa mtu B lazima watu hawa wafanane vilevile katika malengo,ufahamu,mindset,mitazamo yao.
Mambo hayo hapo juu huongozwa na brain(ubongo).
c)Je wakati mwili upo ukiharibika hapa duniani roho itakuwa inafanya nini huko ilipo?
d)Roho inaweza kuishi bila mwili?
,kama inaweza kwanini Mungu ajihangaishe kuumba tena viumbe upya wakati roho inajitosheleza.
e)Roho na mwili kipi kilianza kabla?
Conclusion.From above arguments kifo ni kifo hakuna maisha mengine baada ya kufa hakuna.
Karibuni.......
iPhone 7plus