Dear brothers if ur single and lonely take this one

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,299
2,000
Amwoneaye huruma mwenzake hufikiria mbele, wakati atakapopata taabu atasaidiwa.Moja ya pambo bora kabisa katika sura ya mwanamke ni aibu au haya,kila penye haya ya dhati pana chembe chembe ya umakini,busara na hekima pia pana uwajibikaji na uaminifu kwa mwanmke mwenye pambo hili la haya/aibu .Mwanamke ni gauni jeupe lisilo na doa ambalo hushonwa kwa ubora mkubwa na mwanaume bora anayethamini utu na mapenzi ya mke wake.

Mwanamke asiyeweza kupika wala kufua nguo,wala mwanamke asiyeweza kukata kucha za miguu yake hawezi tunza mume wake wala hawezi tunza mtoto wake hata siku moja,Wanawake wote bora wanalingana sifa na tabia ,na tabia zao ni wachapakazi ,waaminifu kwenye ndoa zao na huvumilia shida na raha za mume wake bila kukata tamaa,Wanawke wenye tabia ya kuiba waume za watu ndio wenye sifa za uvivu,mapenzi ya pesa na majivuni yasio na tija na vivazi vya kuwarubuni waume za watu kwa mavazi yasiyo na staha wala heshima .

80/20 ni sheria ya mapenzi yenye maana mkeo wa ndoa anakupa 80%ya mapenzi na kila kitu ila unakosa 20% toka kwake ambazo wewe unazitafuta nje ,kwa hawa wanawake wavivu wa fikra,ambao sio waaminifu kwenye mapenzina wavivu,unapoteza 80% ya mapenzi bora na yenye Baraka za mwenyezi Mungu na wazazi na kwenda kuzifuata 20% kwa wanawake wanaopoka waume za watu,Mkeo akigundua kuwa umemsaliti unapoteza Baraka,heshima na uaminifu kwa ajili ya mwanamke mjinga na kumuacha mwanamke bora.Jifunze kurekebisha 20% za mkeo ili awe mkamilifu na sio kwenda kuzitafuta nje.

Wanawake bora hawaibi waume za watu bali hutunza wanaume bora ila wanawake wazuri wasio bora huiba wanaume wazuri wasio bora ,Kuwa makini kutofautisha kati ya mwanamke bora na mwanamke mzuri .Wanawake bora ni adimu kupatikana kama dhahabu sababu hawapatikani kwa urahisi na daima huficha maungo yao kwa mavazi yenye staha. Wanawake wazuri wasio bora hupatika kwa urahisi sana na utawagundua kwa mavazi ya kuonyesha maungo yao na nguo za kubana makalio.Moyo wenye mapenzi ya dhati na Ubongo wenye hekima na busara wa mwanamke ndio hutunza ndoa na sio sura wala shape ambazo hutunza mtoto wala ndoa.

Dear brothers If you are single and lonely take this one.The beauty of a woman is not in the clothes she wears, the figure that she carries or the way she combs her hair. The beauty of a woman must be seen from her eyes because that is the doorway to her heart, the place where love resides
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,772
2,000
Nimeingia jukwaa la ushauri nasaha, nimejikuta nimeusoma bila kupenda, humu JF unaweza hata kusalishwa dini nyingine bila kupenda
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom