Ab-Titchaz
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 14,630
- 4,267
Duh!Hii ilikuwa hatari kwa kweli
Kama hio bunduki isingali misfire, jamaa angalikua al-marhum!
Umeona eeh?maana pale unajipenyeza gongoni yake kama unataka kumpa roba kumbe una kula jugural! au una piga direct za ubavuni karibu ya kwapa mbona hachelewi!silaha ninayoiamini mimi ni kisu tu
Kiongozi wa chama cha Upinzani nchi Bulgaria anusurika kifo. Hii ni hatari, sijui jamaa alikuwa anatishia au alipania kweli? Kama nia yake ilikuwa ni kuua, alikuwa na sababu gani ya kwenda hadi kule mbele. Si angepiga risasi kutokea alipokaa? Au alikuwa anatafuta tu umaarufu?
Tuombe Mungu Tanzania tusifikie huku. Cheki hiyo video.
Nimependa huko kiongozi alivyomkunja jamaa haraka haraka. Japo katika hali ya kawaida ilitakiwa risasi iwe imeshatoka kama kweli bunduki ingekuwa na risasi.Hii ni noumer aisee
Aaah, ndiyo maana kumbe, maana sijaona mantiki kabisa ya kushindwa kushoot hadi katika distance hiyo aliyokuwa amefika. kumbe ilikuwa geresha? Sidhani kama ingekuwa rahisi kwake kuua kwa visu mbele ya umati wote huo.Ilikuwa ni gas pistol, haikuwa ya moto ingawaje jamaa alikutwa na visu viwili mifukoni.
aaah, hili nalo sikulijua. nilidhani angeweza hata kusogea viti vya mbele tu na kuweza kupiga risasi kulko kupanda hadi jukwaani.Hii bastola ni ndogo haiwezi kuua zaidi ya mita 30, alitaka kupata best shot
Lakini ilikuwaje hadi huyo jamaa akapanda stejini? Walinzi walikuwa wapi?