GE2025 DCP David Misime: Wanawake mkahamasishe amani majumbani kuelekea uchaguzi Oktoba 29

GE2025 DCP David Misime: Wanawake mkahamasishe amani majumbani kuelekea uchaguzi Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi ,(DCP) David Misime ameeleza kuwa jukumu la kulinda amani ni la kila Mtanzania, kwani vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani vinafanywa na watu waliopo katika jamii

‎Misime amebainisha hayo katika Kongamano la Wanawake wa Dar es salaam, linalofanyika leo Oktoba 26, 2025, katika ukumbi wa mikutano wa DYCCC, Chang'ombe mkoani Dar es Salaam

‎"Suala la ulinzi na usalama katika jamii si suala la polisi pekee bali ni suala la jamii nzima", amesema DCP Misime.

‎Amewasihi wanawake Kutumia sauti zao kuwakemea wanafamilia katika mambo yanayoweza kuvunja amani ili kuhakikisha amani inaendelea kutawala na kuhamasisha watu katika jamii kujitokeza kupiga kura

‎Kongamano hilo linaangazia faida na madhara ya uchaguzi likiwa na kaulimbiu, 'usipomchagua unayemtaka, utachaguliwa usiyemtaka"



Chanzo: Jambo TV
 
Screenshot_20250922-171016.jpg
 
Back
Top Bottom