DCI Manumba: Tumejiandaa

DCI Manumba: Tumejiandaa

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
10,955
Reaction score
4,662
Wakati wa Jeshi la Polisi la Tanzania likisema linafuatilia taarifa za vitisho za kundi la Al-Shabaab la Somalia za kushambulia, Mtanzania mmoja, Vedasto Nsanzugwanko ambaye alijeruhiwa kwenye shambulio la Kenya ameelezea yaliyomkuta.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alisema jana kuwa wameanza kufuatilia kwa undani taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kwamba kundi la Al-Shabaab linajipanga kuishambulia Tanzania na Uganda.

DCI Manumba alikiri kusikia taarifa hizo na kusema kuwa Jeshi la Polisi limeanza kufanya uchunguzi wa kina: “Siwezi kukueleza ni uchunguzi wa aina gani tutakaofanya, hiyo ni siri yetu.”

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Meja Eric Komba alisema kuwa kuna uwezekano taarifa hizo zikapikwa na wajanja wachache kwa ajili ya kuwajengea hofu wananchi.

“Taarifa za kwenye mitandao wakati mwingine ni uzushi mtupu… kuna kipindi ziliwekwa taarifa za uongo zinazohusu jeshi hili,” alisema.

Alipotakiwa kutoa msimamo wa jeshi hilo iwapo taarifa hizo zitakuwa na ukweli alisema, “Jeshi tuko tayari kwa jambo lolote.”

source: DCI Manumba: Tumejiandaa - Kitaifa - mwananchi.co.tz

My take: Ni kwa neema za Mungu tuu ndio mpaka leo hatushambuliwi lakini si kwa uimara wa jeshi la polisi.

Picha chini ni askari maalumu wa kupambana na ugaidi. picha ya kwanza akimpa escort mtuhumiwa wa ugaidi.
Picha ya pili askari wetu shupavu akidhibiti uhalifu.
attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • askari 2.jpg
    askari 2.jpg
    54.1 KB · Views: 756
  • askar.jpg
    askar.jpg
    10 KB · Views: 787
DCI Manumba asichezee Moto haya mambo si ya kujigamba tumejipanga. Hata siku moja huwezi kujipanga kuzuia ugaidi madawa ya kulevya tu yamewashinda ambayo yanageuzwa kuwa kemikali kila leo......naomba asicheze kabisa na hawa jamaa kwa kusema wamejipanga.
 
huyu Meja Eric Komba asijidai kujitoa ufahamu kuwa taarifa za kwenye mitandao ni za kupikwa , eti kuwa hata jeshi lilishazushiwa. kama anaongelea yale ya mtwara amechemsha huyu.
 
hata malawi walisema hivyo hivyo serious watanzania ni taifa hovyo sana duniani kote sina uhakika na wengine lakini tuna maneno mingi wakati watendaji ni wengine kabiasa ,wanapiga domo wao wanakaa oficini tena wamejificha kaka na dada zetu JWTZ wanaenda uwawa .
 
Amejipanga nini? Hadi leo hii unaingia na gari yako quality center hakuna hata kukaguliwa. Kuna wale walinzi wenye virungu tu. Huu ni uchemfu, si wakati wa kuropoka kushabikia ugaidi kama Mwigulu, si wakati wa kujisifu, hawajatuamlia. Hivi hawa viongozi wetu wataacha lini kutoa majibu na kauli nyepesi kwa issue nzito kama hizi?
 
Hiyo kauli ya DCI sijaipenda, tena asituchefue watanzania!! Kwani matukio ya jamii hiyo ya ugaidi yameishaanza kuonjwa na Tanzanis. Fikiria habari ya milipuko ya mabomu Arusha na Umwagiwaji tindikali baadhi ya watu, Mbona mpaka leo hakuna jawabu lolote la kutia moyo watanzania, kulitumainia jeshi lao la Polisi?
Kauli za Majigambo ya namna hii hayafai kabisa! Mengi yalishatokea na kauli za kujigamba kuahidi kuwa vitendo vibaya havingeweza kutokea lakini vimetokea...Ni AIBU!!!
 
Wakati wa Jeshi la Polisi la Tanzania likisema linafuatilia taarifa za vitisho za kundi la Al-Shabaab la Somalia za kushambulia, Mtanzania mmoja, Vedasto Nsanzugwanko ambaye alijeruhiwa kwenye shambulio la Kenya ameelezea yaliyomkuta.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alisema jana kuwa wameanza kufuatilia kwa undani taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kwamba kundi la Al-Shabaab linajipanga kuishambulia Tanzania na Uganda.

DCI Manumba alikiri kusikia taarifa hizo na kusema kuwa Jeshi la Polisi limeanza kufanya uchunguzi wa kina: “Siwezi kukueleza ni uchunguzi wa aina gani tutakaofanya, hiyo ni siri yetu.”

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Meja Eric Komba alisema kuwa kuna uwezekano taarifa hizo zikapikwa na wajanja wachache kwa ajili ya kuwajengea hofu wananchi.

“Taarifa za kwenye mitandao wakati mwingine ni uzushi mtupu… kuna kipindi ziliwekwa taarifa za uongo zinazohusu jeshi hili,” alisema.

Alipotakiwa kutoa msimamo wa jeshi hilo iwapo taarifa hizo zitakuwa na ukweli alisema, “Jeshi tuko tayari kwa jambo lolote.”

source: DCI Manumba: Tumejiandaa - Kitaifa - mwananchi.co.tz

My take: Ni kwa neema za Mungu tuu ndio mpaka leo hatushambuliwi lakini si kwa uimara wa jeshi la polisi.

Kiongozi!

Serikali hovyo, inazaa watendaji hovyo kabisa. Hivi huyo anaye sema tumejiandaa anajua anacho kisema au ni ili mradi waTanzania wasikie kwamba kiongozi wa Taasisi flani ya serikali amesema?

hivi pale Ubungo terminal kuna usalama gani kama watu wanaamua kufanya yaliyo tokea Nairobi? Ni maeneo gani hapa Tanzania ambayo yanakusanya watu wengi, panafanyika ukaguzi kiasi kwamba ana sema tumejiandaa? Kama vibaka waliwahi kuingiza na kutapeli watu pale Magogoni bila kizuizi, unategemea nini kwenye maeneo ya kawaida?!!

Asilete mzaha na hili jambo kabisa. Labda kama wamejiandaa kwa upande wa Magogoni, lakini huku kwetu tunapo pishana kila siku, sijaona lolote la kuwazuia hao maharamia.
 
DCI Manumba asichezee Moto haya mambo si ya kujigamba tumejipanga. Hata siku moja huwezi kujipanga kuzuia ugaidi madawa ya kulevya tu yamewashinda ambayo yanageuzwa kuwa kemikali kila leo......naomba asicheze kabisa na hawa jamaa kwa kusema wamejipanga.

Manumba afadhali akae kimya kuliko kujigamba ilihali wameshindwa kuwakamata hawa UAMSHO wanaowamwagia watu tindikali; itakuwa hao kaka zao AL SHABAB wanaotumia silaha kali!!
 
kama mabomu mawili ya Arusha walishidwa kujua yamepigwa na nani,zanzibar tindikali ni kila siku na wahusika wanashidwa kuwakamata,ni alshababu ndio watataweza?
Mungu atuepushie mbali tu!
 
Sijajua vizuri kujiandaa huku labda afafanue. Hivi kama kuna ndege ya kigeni inatua hapa kwetu na inabeba Twiga,Tembo,Viboko,Nyani,Panya nk tena wakiwa wazima na kuondoka nao! Ndio tumejiandaaje hapo. Kulinganisha na Kenya inavyopata majanga makubwa kila mara,Watanzania naona kama tunalindwa na Mungu aliye hai siku zote!
 
DCI usije ukawaudhi al-shabaab umeona yaliyotokea kenya mpaka sasa watoto mashababi 14 wanawatoa jasho.
 
Mngejipanga mambo ya kishenzi kama ya kinaulimboka, Kibanda na mengi tu yasingekuwa hayajulikani mpaka leo, hawa jamaa wamelewa mdaraka... na silazima kulisemea kila jambo wakati mwingine ukimya ukujengea hisia za hekima!
 
Manumba anafikiri kauli ya Pinda itafanya kazi kwa magaidi.
 
[QUOTEMy take: Ni kwa neema za Mungu tuu ndio mpaka leo hatushambuliwi lakini si kwa uimara wa jeshi la polisi.[/QUOTE]

Kama ni mtihani nakupa 100%
 
Mijitu mingine ya ajabu sana hapa Tanzania. Sijui hawajui hasara kiuchumi ambayo kenya wamepata na watayoendelea kupata kutokana na tukio hili. Hii mijitu badala kuchunga mimeno yao wao wanaikenua kenua kujifanya wao ndio mashujaa kuliko wenzao, Mossad wako pale lakini ndoma imekesha siku ya nne sasa !!, Wao wangeweza nini????. Wachunge upumbavu wao tena wakome, wasituletee matatizo kwa kuuwita ugaidi uje. Waige Serikali ya Rwanda, UG na Burundi, hawa mabwana wanafanya mambo yao kimya kimya hawaropoki kama haya malevi ya kwetu. Pumbaf.....u.
 
Hawa ndio viongozi wetu ngoja aje Kova aanzishe movie ...................................
 
Tuombe mungu tu , polisi wa nchi yetu wapo kwa ajili ya maandamano ya wapinzani tu .
 
Hawa watu hawapo serious kabisa...kazi ni kupambana na CDM tu...lakini mwatukio mengine chali
 
Manumba, hapo ulipo hebu geuka nyuma umuone Alshabab anataka kukuzibua.
Sasa mmejipanga kwa lipi? Wapi? Nani? Saa ngapi?
Msituletee balaa nyie Manyumbu na kauli zenu za kijinga-jinga.
Bomu mbili pale Chuga mpaka leo hamjui aliyelipua, Zanzibar na tindikali Padre kuuawa mpaka leo hamjui chochote leo hii mmejiandaa, mmejiandaa kuliberaliwa au mmejiandaa kulipua mabomu tena??
Al shabab wapo wamejaa Tanzania nzima kila kona wakiongozwa na kiongozi wao mkuu hapa nchini IGP Mwema.
 
Back
Top Bottom