DC wangu Monduli umepotoshwa

Kipa Ile

Member
Sep 30, 2021
7
3
DC WANGU MONDULI AMEPOTOSHWA

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!!!

Kwanza napenda kusema sikusudii wala sipendi kujibishana na mkuu wangu wa wilaya Kwenye vyombo vya habari.

Lakini nimelazimika kusema kidogo ili kuondoa upotoshwaji mwingi aliosema DC Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.

Kitu ambacho nimeshangaa na kujiuliza mimi ni nani mpaka DC akanituhumu tena Kwenye vyombo vya habari na bila kunipa nafasi ili na mimi nihojiwe.

Cha ajabu vyombo vyote vya habari wanatishwa wasitoe taarifa ya upande wetu.

Na mimi nimeamua kutumia kalamu yangu kujibu baadhi ya hoja alizozitoa kwa kisingizio eti waliomtangulia walikosa muda wa kushugulikia.

Naomba kusema tuhuma hizi sio mpya zimetengenezwa tangu 2017 ili kuzima mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wenye fedha waliopora ardhi ya kijiji na wananchi.

Kwa bahati mbaya sana ofisi ya DC kwa muda wote umekuwa upande wa waporaji na sisi wananchi kukosa msaada kila walipofika katika ofisi hizo.

Nimekuwa mhanga kwa jambo hili nimetengezewa kesi nyingi nimepelekwa mahakamani nilinyimwa dhamana nilikaa magereza mara kadhaa na kutengenezewa kesi ili tu ninyamaze Lakini kwa kuwa nilipewa dhamana na wananchi wenzangu nimekataa dhuluma hizi na nipo tayari kuteswa kufungwa tena kupewa kesi tena au kufukuzwa Lakini sintauza haki za wana Eng'arooji leo wala kesho.

Jambo lingine katika hili ambalo DC hajui ni kwamba tuhuma hizi nimeshachunguzwa mara tatu na takukuru na sijakutwa na hatia.

Hata ofisi ya ukaguzi wa ndani walishanihoji mara nyingi na hawakuona Cha maana kinacholalamikiwa namshauri DC achukue taarifa hizo katika ofisi hizo wala asipoteze muda mwingi.

Mikono yangu ni misafi naamini taarifa zipo mh DC angezisoma.

Labda niseme kwa ufupi hoja hizi za kutengeneza ili kunivunja moyo japo zinaniimarisha.

1.kwamba tawi langu la ccm limenilalamikia
Kwanza dc sio msemaji wa ccm malalamiko yaliopelekwa ccm yatashugulikiwa na uongozi wa ccm na sijawahi kuulizwa na chama nashangaa dc anataka pia kuwa katibu wa ccm
Hata hivyo atambue tawi la engarooji limenipendekeza kugombea uwenyekiti wa kijiji 2019 na niliteuliwa na nikashinda kwa zaidi ya asilimia tisini Kwenye kura za maoni.

Siamini chama ingemwamini mbadhirifu
Kwa hili nawaachia chama waseme zaidi

2.Hoja ya kunisimamisha madaraka kwa mujibu wa sheria wenye mamlaka wa kuniondoa ni wale walionipa ridhaa au chama changu kilichonichidhamini
Nashauri dc mambo mawili anipeleke, mbele ya umma wa engarooji akawahoji kwa mujibu wa sheria wakapige kura ya kuniondoa.

Namwomba asinionee kwa kuwa ana mamlaka na nguvu ya dola atumie njia ya haki kuniondoa
Aniandikie tuhuma zangu nizijibu na mwisho aje mbele ya mkutano bila mitutu ya bunduki
Au ikimpendeza anipeleke katika chombo cha haki ambayo ni mahakama nikajitetee asitumie mamlaka yake vibaya ili kutuondoa Kwenye hoja ya msingi.

3.kunyang'anya watu ardhi na kugawa kwa watu
Niambiwe ardhi kiasi gani na ni ya nani na nimempa nani na kama kuna ushahidi utolewe.

Mgogoro ninaujua ni ule wa ekari 1285 za kijiji ambayo waporaji wamechukua na kesi ipo mahakamani namwomba dc kama wao wameshindwa kutatua waiachie mahakama uhuru wa kuamua kesi ndio chombo cha juu Chenye kutoa haki.

Namwomba asiingilie hili jambo lipo mahakamani na anajua.

Tumeenda huko kwa kuona huku ktk ofisi yake tumekosa msaada huko nyuma japo tulionyesha imani kwake alipokuja Lakini imekuwa tofauti.

4.Hoja ya 150 milioni
Nyumba hizi zilijengwa na wageni wa Robin Hunt Safaris kwa kununua vifaa kumlipa fundi na ikisimamiwa na mhandisi wa wilaya
Hakuna sh hata moja nimepokea wala kijiji kimepokea kwa mfadhili bali walijenga nyumba na nyumba zipo engarooji zinatumika.

Kwa hili wakaguzi walikuja na takukuru pia. Labda kama kosa langu kukubali nyumba hiyo zijengwe basi niambiwe.

Wafadhili wapo waulizwe kama nilishika hata shilingi.

5.Hoja ya mapato na matumizi na hoja ya kuchangisha michango bila kibali
Nitazijibu kwa pamoja.

Sijawahi kuchangisha fedha yeyote niliomba ushahidi hakuna nilichunguzwa na takukuru huko nyuma sikuwa na hatia hoja hii ni ili kufifisha mapambano dhidi ya ardhi yetu na hii haiwezi kutuzuia.

Fedha zilichongwa ni sh 10000 ya kila mwananchi wa mondul na zinasimamiwa na wilaya sisi tulikabidhi huko.

7.Kuchukua mifugo na kuuza hii nayo naipuuza kama ambavyo nilipuuza tangu mwanzo

Kuhusu kufoji mihutasari mimi sio mwandishi wa mihutasari na hata hivyo vipo vyombo vya kuchunguza. Viachwe vifanye kazi.

Najiuliza kama Mh DC angekuwa na nia njema kwanini asingewapa vyombo vinavyohusika nafasi ya kuchunguza kabla ya kuchukua hatua hii haraka ya ghafla inatoka wapi.

Ndio tunapata hisia kuna msukumo wa rushwa katika ofisi yake na hili nilimwandikia kumtahadharisha wapo watu wanauza,Mifugo ili kuleta fedha katika ofisi yako.

Mwisho niseme nimwombe tena dc aache mahakama itoe haki na kama tuhuma dhidi yangu zenye mshiko Uchunguzi huru ufanywe ili niwe na Imani maana Kwa Sasa Ofisi yako inachuki na Mimi.

Wenu

Ngalama Mapema.
Mwenyekiti Kijiji Cha Eng'arooji
 
Nyie wamasai mnapenda sana migogoro. Kwani ardhi Monduli imeisha? Hamieni eneo jingine kabisa mkaanze upya.

Ngorongoro mmegoma kutoka, mmeahidiwa kupewa maeneo mengine mazuri na huduma juu ila mmegoma kuhama.

Mnapenda sana mabifu ya ardhi, Badilikeni!
 
Magufuli alikosea sana kuwapa vyeo makada wa ccm !!! Vyeo vya UDC ,URC vimekuwa vya hovyo sana miaka ya karibuni
 
Back
Top Bottom