DC wa Arusha atuhumiwa TAKUKURU

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,820
1,195
MKUU wa Wilaya ya Arusha Mjini John Mongella, ameingia matatani baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) “kumchongea” kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwa anatumia madaraka yake vibaya na kujihusisha rushwa katika masoko ya Halmashauri ya Jiji.

Chama hicho cha upinzani kimemwandikia barua Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, kikimtuhumu DC Mongella ya kuwa anajihusisha na rushwa katika masoko ya Jiji.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba CDM/Ar19/98/14 ya Aprili 28 mwaka huu imetiwa saini na Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha Mjini wa chama hicho Ephata Nanyaro.

“Tunaleta kwako tuhuma za rushwa dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, (John Mongella) kwenye masoko yafutayo,” inasema sehemu ya kwanza ya barua hiyo.

Katika barua hiyo Nanyaro anadai kuwa katika soko la kuuza nguo za mitumba la Krokon ushuru unaokusanywa haujawahi kupelekwa Halmashauri na badala yake viongozi wa soko hupeleka fedha hizo kwa Mkuu wa Wilaya.

Anaeleza ya kuwa hatua ya fedha hizo za ushuru kutopelekwa Halmashauri ni kinyume cha Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 2000 na kwamba “mgao” anaopelekwe Mkuu wa Wilaya ni uvunjaji wa sheria.

Raia Mwema katika siku za nyuma lilipata kufichua taarifa za kuwapo kwa ufisadi wa mamilioni ya fedha za makusanyo ya ushuru wa soko hilo la Krokon kwa kuandika habari katika moja ya matoleo yake ya mwezi Machi mwaka huu.

Taarifa za ufisadi huo zilidai kuwa kiasi cha shilingi milioni 4.2 hukusanywa kila mwezi kutoka katika vizimba zaidi ya 700 ambapo kwa kila kizimba wafanyabiashara hulipa shilingi 6000 kwa mwezi.

Hata hivyo fedha hizo hazikuwahi kufikishwa katika hazina ya Halmashauri ya Jiji kama sehemu ya mapato na badala yake inadaiwa kuwa viongozi wa soko wamekuwa “wanagawana” fedha hizo na baadhi ya viongozi wa serikali katika ngazi ya Wilaya na Mkoa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, soko jingine ambalo mapato yake yanahusishwa na Mkuu huyo wa Wilaya ni soko la Kilombero ambalo inadaiwa zaidi ya milioni 60 zilipotea mwaka 2013.

“Kati ya mwezi Januari na Aprili mwaka 2013, Mkuu wa Wilaya alijichukulia maamuzi ya kuwapeleka wakusanya ushuru katika soko hilo kinyume cha sheria na hivyo kusababisha upotevu wa shilingi milioni 60 fedha za walipa kodi,” inaendelea kueleza barua hiyo.

Zipo nyaraka kadhaa ambazo zinaonyesha Mkuu huyo wa Wilaya akiagiza vijana waliokusanya ushuru katika soko hilo walipwe shilingi milioni 4 kwa kazi hiyo wakati aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji Zipora Liana akikataa kwa madai kuwa vijana hawakuwa na mkataba wowote na Halmashauri wa kufanya kazi hiyo.

Nanyaro anadai pia katika barua yake kuwa soko jingine ni soko jipya la NMC, ambako Halmashauri inakusanya shilingi 100,000 kwa siku wakati makusanyo halisi ni shilingi 650,000 kwa siku.

“Kwa kuwa taasisi yako inazuia na kupambana na rushwa, na kwa kuwa rushwa ni adui wa haki na ni jukumu la kila mpenda haki kuzuia na kupambana na rushwa ni matarijio yetu kuwa ofisi yako itafanyia kazi tuhuma hizi kwa mujibu wa sheria,” inasema barua hiyo.

Akizungumzia hatua ya CHADEMA kuandika barua hiyo Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha Juventus Baitu aliimbia Raia Mwema kuwa hana taarifa ya kuandikwa barua hiyo na ilikuwa haijamfikia.

“Sijaiona hiyo barua, na nadhani bado haijafika mezani kwangu. Ningekuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo kama ningepata nakala ya barua yenyewe,”alisema Kamanda Baitu.

Alisema hata hivyo, taasisi yake iko tayari kuzifanyia kazi tuhuma zote zinazowasilishwa bila kujali wadhifa na nafasi ya mhusika katika jamii kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria za nchi.

Kwa upande wake Mongella aliliambia Raia Mwema kwa njia ya simu kuwa amepata taarifa za suala hilo mwezi moja uliopita lakini bado alikuwa hajaitwa na maafisa wa Takukuru.

“Ndiyo nimesikia taarifa kama mwezi moja uliopita kuhusu madai hayo ila bado sijaitwa na mtu yoyote….wakiniita nitawapa ushirikiano wa kutosha,”alisema Mongella.

Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza:”Kimsingi mambo hayo yote ni fitina za kisiasa dhidi yangu. Utajiuliza hivi DC anahusikaje na masuala ya mapato ya Halmashauri?”

Hata hivyo, Nanyaro alipoulizwa na gazeti hili taarifa kuwa barua yake haijafika Takukuru alijibu kuwa barua ilifikishwa muda mrefu uliopita na kitabu cha kumbukumbu za barua katika ofisi za CHADEMA Wilaya kinaonyesha kuwa barua hiyo imepokowa na Takukuru.

“Barua ilifikishwa na kumbukumbu kuwa imepokewa zipo katika dispatch, kilichopo ni kwamba Takukuru wameanza ubabaishaji wao kwa kuwa anayelalamikiwa ni kiongozi wa serikali ambaye hawana ujasiri wa kumhoji,” alidai Nanyaro.

Aliongeza ya kuwa nakala ya barua yenye madai dhidi ya Mkuu wa Wilaya wamezipeleka pia kwa Waziri wa Tamisemi Hawa Ghasia na Wakala wa Ugavi na Manunuzi (PPRA).

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Idd Juma hakuwa tayari kuzungumzia suala la fedha za ushuru wa masoko kutoingia katika hazina ya Halmashauri kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao cha Kamati ya Fedha.

“Ndiyo tunataka kuanza kikao cha Kamati ya Fedha muda huu naomba unipigie kesho Jumanne nitakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia suala hilo,” alisema.

Meya wa Jiji la Arusha, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi hakupatikana kupitia simu yake lakini mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo ambaye ni Diwani wa CCM alieleza kusikitishwa kwake na jinsi mambo yanavyoendeshwa ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha.

“Haya madai yote ni ya kweli, kuna masoko ambayo mapato yanayokusanywa hayapelekwi Halmashauri, na mambo haya tumeyapigia kelele mapaka tumechoka kwa kuwa kuna wakubwa wana mikono yao katika ukusanyaji wa mapato,” alisema Diwani huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

Takwimu zinaonyesha kuwa kutokana na kushamiri kwa ufisadi katika ukusanyaji wa mapato, Jiji la Arusha pamoja na kuwa na vyanzo vingi vya mapato, hadi mwaka 2012 lilikuwa linakusanya shilingi milioni kati ya 350-400 kwa mwezi.

Mapato hayo yalipanda hadi kufikia milioni 750-800 mwaka jana baada ya Mkurugenzi mpya Zipora Liana kushika hatamu ambaye hata hivyo hakudumu kutokana na kuhamishiwa Tamisemi kwa kile kinachoelezwa kuwa ni “fitina za wakubwa” huku sasa kukiwa na tetesi kuwa mapato tayari yameanza kushuka tena kutokana na uzembe na ufisadi katika makusanyo.

Source:
Raia Mwema
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Hapa naona mfululizo wa matatizo na matatizo ya nyongeza.

Kwanza kabisa, nadhani hili swala halikai sawa kama litawekwa kwenye mizani ya Rushwa. Huu ni wizi na ubadhirifu wa fedha za umma. Kama kina Nanyaro wana ushahidi wa kutosha nadhani wamekosea kuchukua hatua. Kilichotakiwa kufanywa ni kumshitaki mkuu wa wilaya mahakamani kwa makosa ya:

1. Matumizi mabaya ya madaraka

2. Ubadhirifu wa mali ya umma

3. Wizi wa kuaminiwa

4. Wizi wa kawaida. (kama mwizi yeyote tu)

Kwa upande mwingine, sioni ni vipi kuna mtu ana imani na TAKUKURU. Naona kama utendaji wao una utata. Hebu niambieni pamoja na rushwa kukithiri, mpaka hadharani, mbona hatusikii wala kuona wanaokamatwa, kushitakiwa na kupatikana na hatia? mbona hata wanaokamatwa wanaachiwa kila mara? na mbona rushwa ndiyo kwanza inapandisha bendera kila asubuhi? Nadhani ni vema Watanzania mkakumbuka kuwa ni TAKUKURU hiyo hiyo ikishirikiana na ofisi ya CAG ndiyo ilihusika kuipaka mafuta tenda ya Richmond kuwa ilikuwa halali na iliyofuata taratibu! Na sidhani kama kuna namna ya kuiamini TAKUKURU kuwa inaweza kupambana na rushwa.

Binafsi nadhani ili kuondoa kasoro nyingi zinazojitokeza ndani ya serikali kama hizi, ni vizuri kwanza turudi nyuma na tukumbukie makosa yetu. kwani ni mambo kama haya yanayofanya tuone umuhimu wa Azimio la Arusha, na kwamba waliolifuta kihuni walikuwa wanatafuta nafasi ya kufanya haya. Pia nadhani kwa sasa tuanze kufikiria namna ya kushughulika mambo kama haya kwani ni wazi kuwa hata TAKUKURU yenyewe inapaswa kuchunguzwa kwa tuhuma za rushwa!
 
PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,924
2,000
laana ya kuwafuku za kama mbwa,wapangaji wa nyumba za almashauri ya jiji la arusha itamtafuna,john mongela, maana yeye ndiealiekua kamanda na kinara wa kuwaondoa wapangaji kama mbwa,tena kuna tetesi kwenye ishu ya kuwaondoa wapangaji,alipiga mtonyo,wa nguvu,kimsingi ni kama madiwani hawana kazi,maana hu
yu mkuu wa wilaya ndiye almashauri yenyewe,mimi nawashauri hawa madiwani wafungue kesi mahakamani ya kupinga mkuu wa wilaya kuingilia shuguli za almashauri.kuliko kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere,
 
Arnold Ringo

Verified Member
Jan 23, 2014
2,319
1,170
Hi ni Hatari sana na nimuhimu kufwatiliwa kwa haraka zote maana Ushuru wa sehemu ndio moyo wa sehemu husika ni hatari sana sana
 
Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
ukoo wa panya bhana. kila kukicha ni kubuni njia ya kuliibia taifa hili. we have a long to go.
 
mmaranguoriginal.

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,058
1,195
Hata ccm hatumtaki huyu mongela anachochea ukabila kwa kuleta machafuko ni pimbi anawachukia watu toka kilimanjaro.tulishamweleza hii vita yake na wachaga anapambana na tulioko ccm
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,284
2,000
MKUU wa Wilaya ya Arusha Mjini John Mongella, ameingia matatani baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) “kumchongea” kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwa anatumia madaraka yake vibaya na kujihusisha rushwa katika masoko ya Halmashauri ya Jiji.

Chama hicho cha upinzani kimemwandikia barua Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, kikimtuhumu DC Mongella ya kuwa anajihusisha na rushwa katika masoko ya Jiji.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba CDM/Ar19/98/14 ya Aprili 28 mwaka huu imetiwa saini na Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha Mjini wa chama hicho Ephata Nanyaro.

“Tunaleta kwako tuhuma za rushwa dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, (John Mongella) kwenye masoko yafutayo,” inasema sehemu ya kwanza ya barua hiyo.

Katika barua hiyo Nanyaro anadai kuwa katika soko la kuuza nguo za mitumba la Krokon ushuru unaokusanywa haujawahi kupelekwa Halmashauri na badala yake viongozi wa soko hupeleka fedha hizo kwa Mkuu wa Wilaya.

Anaeleza ya kuwa hatua ya fedha hizo za ushuru kutopelekwa Halmashauri ni kinyume cha Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 2000 na kwamba “mgao” anaopelekwe Mkuu wa Wilaya ni uvunjaji wa sheria.

Raia Mwema katika siku za nyuma lilipata kufichua taarifa za kuwapo kwa ufisadi wa mamilioni ya fedha za makusanyo ya ushuru wa soko hilo la Krokon kwa kuandika habari katika moja ya matoleo yake ya mwezi Machi mwaka huu.

Taarifa za ufisadi huo zilidai kuwa kiasi cha shilingi milioni 4.2 hukusanywa kila mwezi kutoka katika vizimba zaidi ya 700 ambapo kwa kila kizimba wafanyabiashara hulipa shilingi 6000 kwa mwezi.

Hata hivyo fedha hizo hazikuwahi kufikishwa katika hazina ya Halmashauri ya Jiji kama sehemu ya mapato na badala yake inadaiwa kuwa viongozi wa soko wamekuwa “wanagawana” fedha hizo na baadhi ya viongozi wa serikali katika ngazi ya Wilaya na Mkoa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, soko jingine ambalo mapato yake yanahusishwa na Mkuu huyo wa Wilaya ni soko la Kilombero ambalo inadaiwa zaidi ya milioni 60 zilipotea mwaka 2013.

“Kati ya mwezi Januari na Aprili mwaka 2013, Mkuu wa Wilaya alijichukulia maamuzi ya kuwapeleka wakusanya ushuru katika soko hilo kinyume cha sheria na hivyo kusababisha upotevu wa shilingi milioni 60 fedha za walipa kodi,” inaendelea kueleza barua hiyo.

Zipo nyaraka kadhaa ambazo zinaonyesha Mkuu huyo wa Wilaya akiagiza vijana waliokusanya ushuru katika soko hilo walipwe shilingi milioni 4 kwa kazi hiyo wakati aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji Zipora Liana akikataa kwa madai kuwa vijana hawakuwa na mkataba wowote na Halmashauri wa kufanya kazi hiyo.

Nanyaro anadai pia katika barua yake kuwa soko jingine ni soko jipya la NMC, ambako Halmashauri inakusanya shilingi 100,000 kwa siku wakati makusanyo halisi ni shilingi 650,000 kwa siku.

“Kwa kuwa taasisi yako inazuia na kupambana na rushwa, na kwa kuwa rushwa ni adui wa haki na ni jukumu la kila mpenda haki kuzuia na kupambana na rushwa ni matarijio yetu kuwa ofisi yako itafanyia kazi tuhuma hizi kwa mujibu wa sheria,” inasema barua hiyo.

Akizungumzia hatua ya CHADEMA kuandika barua hiyo Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha Juventus Baitu aliimbia Raia Mwema kuwa hana taarifa ya kuandikwa barua hiyo na ilikuwa haijamfikia.

“Sijaiona hiyo barua, na nadhani bado haijafika mezani kwangu. Ningekuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo kama ningepata nakala ya barua yenyewe,”alisema Kamanda Baitu.

Alisema hata hivyo, taasisi yake iko tayari kuzifanyia kazi tuhuma zote zinazowasilishwa bila kujali wadhifa na nafasi ya mhusika katika jamii kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria za nchi.

Kwa upande wake Mongella aliliambia Raia Mwema kwa njia ya simu kuwa amepata taarifa za suala hilo mwezi moja uliopita lakini bado alikuwa hajaitwa na maafisa wa Takukuru.

“Ndiyo nimesikia taarifa kama mwezi moja uliopita kuhusu madai hayo ila bado sijaitwa na mtu yoyote….wakiniita nitawapa ushirikiano wa kutosha,”alisema Mongella.

Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza:”Kimsingi mambo hayo yote ni fitina za kisiasa dhidi yangu. Utajiuliza hivi DC anahusikaje na masuala ya mapato ya Halmashauri?”

Hata hivyo, Nanyaro alipoulizwa na gazeti hili taarifa kuwa barua yake haijafika Takukuru alijibu kuwa barua ilifikishwa muda mrefu uliopita na kitabu cha kumbukumbu za barua katika ofisi za CHADEMA Wilaya kinaonyesha kuwa barua hiyo imepokowa na Takukuru.

“Barua ilifikishwa na kumbukumbu kuwa imepokewa zipo katika dispatch, kilichopo ni kwamba Takukuru wameanza ubabaishaji wao kwa kuwa anayelalamikiwa ni kiongozi wa serikali ambaye hawana ujasiri wa kumhoji,” alidai Nanyaro.

Aliongeza ya kuwa nakala ya barua yenye madai dhidi ya Mkuu wa Wilaya wamezipeleka pia kwa Waziri wa Tamisemi Hawa Ghasia na Wakala wa Ugavi na Manunuzi (PPRA).

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Idd Juma hakuwa tayari kuzungumzia suala la fedha za ushuru wa masoko kutoingia katika hazina ya Halmashauri kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao cha Kamati ya Fedha.

“Ndiyo tunataka kuanza kikao cha Kamati ya Fedha muda huu naomba unipigie kesho Jumanne nitakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia suala hilo,” alisema.

Meya wa Jiji la Arusha, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi hakupatikana kupitia simu yake lakini mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo ambaye ni Diwani wa CCM alieleza kusikitishwa kwake na jinsi mambo yanavyoendeshwa ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha.

“Haya madai yote ni ya kweli, kuna masoko ambayo mapato yanayokusanywa hayapelekwi Halmashauri, na mambo haya tumeyapigia kelele mapaka tumechoka kwa kuwa kuna wakubwa wana mikono yao katika ukusanyaji wa mapato,” alisema Diwani huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

Takwimu zinaonyesha kuwa kutokana na kushamiri kwa ufisadi katika ukusanyaji wa mapato, Jiji la Arusha pamoja na kuwa na vyanzo vingi vya mapato, hadi mwaka 2012 lilikuwa linakusanya shilingi milioni kati ya 350-400 kwa mwezi.

Mapato hayo yalipanda hadi kufikia milioni 750-800 mwaka jana baada ya Mkurugenzi mpya Zipora Liana kushika hatamu ambaye hata hivyo hakudumu kutokana na kuhamishiwa Tamisemi kwa kile kinachoelezwa kuwa ni “fitina za wakubwa” huku sasa kukiwa na tetesi kuwa mapato tayari yameanza kushuka tena kutokana na uzembe na ufisadi katika makusanyo.

Source:
Raia Mwema

Mgao wa uongozi kifamilia. Huyu mkuu wa wilaya ni familia ya mama Getrude Mongela. Utaona hizi ni mbio za kupokezana vijiti . Nasikitika kuona uongozi ndani ya Ccm majina ni yale yale. Watanzania amkeni!!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom