DC Senyamule: Hakuna wa kuharibu hifadhi ya misitu Same

DC Senyamule: Hakuna wa kuharibu hifadhi ya misitu Same

acer

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
1,595
Reaction score
142
Ililazimu Kamati ya Ulinzi Na Usalama (KUU) Wilaya ya Same kutembelea msitu wa hifadhi Chome (Shengena) baada ya kupata taarifa ya uvamizi wa wachimbaji madini ya dhahabu ndani ya msitu huo.

Uharibifu uliokutwa ni mkubwa Na ni umbali wa zaidi ya km. 2 kutoa eneo la mpaka.
Watu 6 walikwisha kamatwa Na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Ambao 4 wanatoka kijiji cha Mhero kata ya Chome Na 2 wanatoka kijiji cha kanza kata ya Lugulu.

Mkt. Wa KUU (DC) alitoa maelekezo yafuatayo kwa wananchi:-
~ Viundwe vikundi vya ulinzi shirikishi kwa vijiji 27 vinavyozunguka msitu huo.
~ Iwekwe kambi kwa muda ili kuhakikisha uchimbaji hauendelei Na kuwashika watakaoingia.
~ Mashimo yafukiwe Na miti ipandwe kurudishia hali ya eneo husika.
~ KUU kila ngazi kuanzia vijiji hadi Wilaya zitimize wajibu wao.
~ KUU vijiji vyote 27 iwe ni ajenda ya kudumu kuzungumzia hali ya Msitu huo ( uchimbaji dhahabu, moto, kukata miti, kuingiza mifugo)
~ Masaa 48 kwa kila atakayekamatwa kabla ya kuenda mahakamani.
~ TFS - miradi ya uchumi kwa vikundi vyote vya ulinzi shirikishi pamoja Na wananchi wengine
~ TFS - Motisha kwa watoa taarifa.
~ Polisi - mashtaka sahihi.
Wito kwa woote kushiriki vita hii inayotaka kuharibu urithi wetu Na wa watoto Na wajukuu zetu. Kwani bila msitu Huu Maji Same ni shida.

Ziara hiyo ilifanyika Tar. 07/09/2017 ikiwashirikisha wataalamu kutoka TFS na Halmashauri.
349801784946508a3a05eafdfa5b242e.jpg
d8c431af06e144ff9c4adcd8ced70aef.jpg
2d6f797366ede087e9bd943f8d7bd154.jpg
 
..kuna tatizo kubwa zaidi la uchimbaji wa bauxite.

..akiweza kusimamisha uchimbaji huo atakuwa ameiokoa wilaya yake.
 
..DC ashikamane na wabunge wake.

..mmoja ni wa ccm, na mwingine ni mwanamama mwenzake toka cdm.

..akishirikiana nao wakawa kitu kimoja ktk malengo na mipango yao, wilaya ya same itasonga mbele.

..same ndiyo wilaya iliyonyuma kimaendeleo kishinda wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro.

..DC na wabunge wawe kitu kimoja.

cc Zanika
 
..DC ashikamane na wabunge wake.

..mmoja ni wa ccm, na mwingine ni mwanamama mwenzake toka cdm.

..akishirikiana nao wakawa kitu kimoja ktk malengo na mipango yao, wilaya ya same itasonga mbele.

..same ndiyo wilaya iliyonyuma kimaendeleo kishinda wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro.

..DC na wabunge wawe kitu kimoja.

cc Zanika
Umenena vyema JokaKuu
DC wa Same Mh:Rosemary Senyamle ni Killed ngozi wa kitaifa na anashirikiana na kuhudumia wananchi na viongozi wote wa Wilaya yake bila kujali itikadi za kisiasa,Kidini na Kabila.
Kwa sasa tunafahamu wabunge wamo Bungeni na wengi walikuwa kwenye vikao vya Kamati za Bunge.

Ni vema pia tukawaomba ama kuwashauri wabunge wetu wapende kukaa majimboni mwao kipindi wanakuwa hawana kazi za vikao vya Kibunge. Kwa Same ninaamini Mama Rosemary hana tatizo na wabunge wake na anashirikiana nao vizuri.
 
..timu ya waandishi wa habari iangazie na uharibifu unaotokea msitu wa Shengena.
 
Back
Top Bottom