DC nusura amsweke rumande padre

DC nusura amsweke rumande padre

Huyu DC -----.Udini umemjaa
.Na sio huyo tu,
Wateule wengi wa MSHUA ni wa vibarakashea ambao udini ndo kaulimbiu Yao.

Udini nyie wakiristo ndo umewajaa mnataka ma DC wote wawe wagalatia??? mbona yule DC aliyewachapa waalimu alikuwa mgalatia na hamjasema ni JK ni mdini acheni ujinga nyie...........
 
ukiona watawala wamebatiza wapinzani wao kuwa magaidi, wakawafanya wananchi wanaowatwala kuwa ndodndocha, na sasa wanapambana na viongozi wa kiroho ujue kuwa mwisho wao umekaribia

Mwisho wa IDD amin wa Uganda ilikuwa pale alipoanza kuwaua viongozi wa DINI!! CCM haiko mbali!!
 
FIKRA NGUMU;

Mahali popoote duniani ambapo kanisa limestawi jamii husika lazima iwe maskini wa kutupwaaa. Rejea kisa cha Askofu Oscar Romero wa Amerika ya kusini ambako kanisa limeshika hatamu na akaanzisha " Liberation Theology " lakini alipingwa hadi na Papa kutoka Vatican....Kanisa halikutaka jamii ile ikombolewee, Alikufa katika mazingira ya kutatanishaa sanaaa.. !

Kanisa pia halitaki jamii ya Ki Tanzania ikombolewe na Umaskini !

KAnisa lipi au uongo!! KAnisa la TAnzania linastawi kwa sababu ya waamini wao na sio Misaada!!
 
tatizo la kupewa madaraka kwa kujuana. mtu aliyesoma administration hawawezi kufanya mambo kama hayo. Tunaomba CV ya huyu mama!
 
Huyu DC -----.Udini umemjaa
.Na sio huyo tu,
Wateule wengi wa MSHUA ni wa vibarakashea ambao udini ndo kaulimbiu Yao.

Mbona mimi hajanichagua, tena tumetoka kijiji kimoja na nimehitimu UDSM?
 
tatizo la kupewa madaraka kwa kujuana. mtu aliyesoma administration hawawezi kufanya mambo kama hayo. Tunaomba CV ya huyu mama!
hili nalo janga.Haya ndio waliyojifunza kwenye ile semina iliyogharimu mamilioni ya pesa za watz kabla ya kuapishwa na kukabidhiwa ofisi?!
 
Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki parokia ya Chumbageni, Padre James Kabosa ameponea chupuchupu kuswekwa ndani na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa wilaya mwenyewe, Padre Kabosa na msemaji wa Askofu, Padre Peter Kagaba walipozungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti.

Imedaiwa kuwa padre huyo aliepuka kuswekwa ndani kwa kuondoka ofisini hapo baada ya kutofautiana na mkuu huyo wa wilaya na hivyo kumuita mkuu wa polisi wa wilaya afike na kumsweka ndani ndipo wazee wa kanisa waliokuwa wameambatana naye kumsihi Padre aondoke.

Imedaiwa kuwa baada ya tukio hilo Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Baba Askofu Anthon Banzi, alifika ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya akitaka kujua chanzo cha Padre Kabosa kufukuzwa na kutishiwa kuswekwa ndani.

Habari zimebainisha kuwa baada ya mkuu wa wilaya kuona Askofu ofisini akiwa na waumini alimuelewesha kiini cha kumtimua Padre na kumuomba msamaha.

Waumini waliokuwa wamemsindikiza Askofu wao walishikwa na butwaa baada ya kumuona mkuu wa wilaya huyo akipiga magoti mbele ya Askofu Banzi na kuomba abarikiwe na askofu kwa madai mumewe pia ni mkatoliki abarikiwe ili Mungu amsaidie katika kazi zake za kuiongoza jamii.

Akiongea na NIPASHE kuhusu tukio hilo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Mikael, Kiule Msofe, alisema tukio la kufukuzwa kwa Padre lilitokea Machi 27, mwaka huu majira ya saa 8 mchana na tukio la Askofu kufika kwa mkuu huyo wa wilaya lilitokea Aprili 3 na kuwa matukio yote mawili alikuwapo na kuyashuhudia.

Kuhusu chanzo cha tukio hilo, Kiule alisema ni kutokana na mgogoro wa ardhi wa eneo la wazi lililogawanywa na diwani wa kata ya Nguvumali, Selemani Mhina (sele boss) CCM, lililopo mbele ya kanisa la Kigango cha Majani Mapana kinyume cha sheria za ardhi.

Alisema kanisa katoliki lilishaomba eneo hilo zaidi ya mara mbili kwa Jiji la Tanga na kujibiwa kuwa ni eneo la wazi na lakini lilitolewa kwa wafanyabiashara kwa madai kuwa ni agizo la mkuu wa wilaya ili kujenga mashine za kusaga nafaka.

Kwa upande wa padre Kabosa alikiri kupatwa na kadhia hiyo lakini alidai kuwa tayari suala hilo linashughulikiwa na viongozi wakuu wa kanisa hilo kwa hatua zaidi za kurejesha amani na mshikamano ulioonekana kukosekana.
Naye Mkuu wa wilaya, Dendego alipotakiwa kuelezea shutuma hizo alikiri ujio wa padre Kabosa ofisini kwake na kutofautiana kimazungumzo lakini alidai kuwa alimuamuru kuondoka ofisini hapo kwa kuwa hakumtambua kama ni kiongozi wa dini.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alikanusha tuhuma za kueneza udini na kwamba hilo halikufanyika kwa ajili ya udini bali ni moja ya matokeo ya kiutendaji.

Alimtupia lawama na kumtaja diwani Mhina kuwa ndiye anayechochea mgogoro huo kwa kueneza udini kuwa yeye anawapendelea waislamu jambo ambalo ni hatari.

Chanzo: Nipashe Jumapili

huyu ni mmoja wa maDC waislam at work agaist wakristu,gazeti la Alnuru lituchambulie mgogoro huo tafadhali
 
Udini nyie wakiristo ndo umewajaa mnataka ma DC wote wawe wagalatia??? mbona yule DC aliyewachapa waalimu alikuwa mgalatia na hamjasema ni JK ni mdini acheni ujinga nyie...........
aliwachapa waalimu wote wakiislamu,wakikristo na wale waliokuwa wapagani..........shame on you.
 
Like father like sons and duaghters.........ahahaaaaaaaaaaaaa tutegemee mengi toka kwa vimada, mabar-maid na viburudisho vya Rwanda Magere (Great Womaniser)
 
Mfumo dume tu umewajaa.......na hao wanaume ma DC ni kina nani? Hata huyo mama inawezekana ni wanaume tu wanamkorofisha na kutaka kumletea madharau.......chapa kazi madam DC cha muhimu fuata sheria na taratibu.
 
Huyu mwanamke analeta ubabe wa uccm kwa viongozi wa kiroho,bahati yake anaitwa halima,angekuwa joyce.wee mbona tungechoma hadi ofisi.akamuulize yule mtoto aliyekojolea naniihiii.
 
FIKRA NGUMU;

Mahali popoote duniani ambapo kanisa limestawi jamii husika lazima iwe maskini wa kutupwaaa. Rejea kisa cha Askofu Oscar Romero wa Amerika ya kusini ambako kanisa limeshika hatamu na akaanzisha " Liberation Theology " lakini alipingwa hadi na Papa kutoka Vatican....Kanisa halikutaka jamii ile ikombolewee, Alikufa katika mazingira ya kutatanishaa sanaaa.. !

Kanisa pia halitaki jamii ya Ki Tanzania ikombolewe na Umaskini !

Kujikomboa na umasikini ni pamoja na kuipa jamii sio tu ya wakristo wenyewe bali wote fursa ya elimu,afya na ukombozi wa kiroho.Chukulia mfano wa hapa Tanzania sehemu ambazo wamissionari wa mwanzo walipita sio tu kwamba zina wasomi wengi bali pia zimeendelea kuliko kuliko sehemu ambazo hazina/hazikuwa wa wamissionari.
The Fixer,hiyo FIKRA NGUMU yako ni inaonyesha ni jinsi gani kichwani usivyokuwa na kitu au ni sehemu ya wale wenzetu ambao dunia nzima wanalalamika mambo yanayofanana ......eti mfumo kristu.........,pole sana
 
hili nalo janga.Haya ndio waliyojifunza kwenye ile semina iliyogharimu mamilioni ya pesa za watz kabla ya kuapishwa na kukabidhiwa ofisi?!
bora wangefundisha Wenyeviti wa Vijiji kuliko MaDC
 
Huyu mwanamke analeta ubabe wa uccm kwa viongozi wa kiroho,bahati yake anaitwa halima,angekuwa joyce.wee mbona tungechoma hadi ofisi.akamuulize yule mtoto aliyekojolea naniihiii.

Sasa naanza kuamini kuwa CDM kinaamini katika udini hii imekuwa issue tu kwa kuwa padri amekutana na mikono ya sheria kwani mapadri wao wapo juu ya sheria ?? Nampongeza sana huyu DC kama anateleza wajibu wake hata kama ni ccm...............
 
Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki parokia ya Chumbageni, Padre James Kabosa ameponea chupuchupu kuswekwa ndani na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa wilaya mwenyewe, Padre Kabosa na msemaji wa Askofu, Padre Peter Kagaba walipozungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti.

Imedaiwa kuwa padre huyo aliepuka kuswekwa ndani kwa kuondoka ofisini hapo baada ya kutofautiana na mkuu huyo wa wilaya na hivyo kumuita mkuu wa polisi wa wilaya afike na kumsweka ndani ndipo wazee wa kanisa waliokuwa wameambatana naye kumsihi Padre aondoke.

Imedaiwa kuwa baada ya tukio hilo Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Baba Askofu Anthon Banzi, alifika ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya akitaka kujua chanzo cha Padre Kabosa kufukuzwa na kutishiwa kuswekwa ndani.

Habari zimebainisha kuwa baada ya mkuu wa wilaya kuona Askofu ofisini akiwa na waumini alimuelewesha kiini cha kumtimua Padre na kumuomba msamaha.

Waumini waliokuwa wamemsindikiza Askofu wao walishikwa na butwaa baada ya kumuona mkuu wa wilaya huyo akipiga magoti mbele ya Askofu Banzi na kuomba abarikiwe na askofu kwa madai mumewe pia ni mkatoliki abarikiwe ili Mungu amsaidie katika kazi zake za kuiongoza jamii.

Akiongea na NIPASHE kuhusu tukio hilo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Mikael, Kiule Msofe, alisema tukio la kufukuzwa kwa Padre lilitokea Machi 27, mwaka huu majira ya saa 8 mchana na tukio la Askofu kufika kwa mkuu huyo wa wilaya lilitokea Aprili 3 na kuwa matukio yote mawili alikuwapo na kuyashuhudia.

Kuhusu chanzo cha tukio hilo, Kiule alisema ni kutokana na mgogoro wa ardhi wa eneo la wazi lililogawanywa na diwani wa kata ya Nguvumali, Selemani Mhina (sele boss) CCM, lililopo mbele ya kanisa la Kigango cha Majani Mapana kinyume cha sheria za ardhi.

Alisema kanisa katoliki lilishaomba eneo hilo zaidi ya mara mbili kwa Jiji la Tanga na kujibiwa kuwa ni eneo la wazi na lakini lilitolewa kwa wafanyabiashara kwa madai kuwa ni agizo la mkuu wa wilaya ili kujenga mashine za kusaga nafaka.

Kwa upande wa padre Kabosa alikiri kupatwa na kadhia hiyo lakini alidai kuwa tayari suala hilo linashughulikiwa na viongozi wakuu wa kanisa hilo kwa hatua zaidi za kurejesha amani na mshikamano ulioonekana kukosekana.
Naye Mkuu wa wilaya, Dendego alipotakiwa kuelezea shutuma hizo alikiri ujio wa padre Kabosa ofisini kwake na kutofautiana kimazungumzo lakini alidai kuwa alimuamuru kuondoka ofisini hapo kwa kuwa hakumtambua kama ni kiongozi wa dini.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alikanusha tuhuma za kueneza udini na kwamba hilo halikufanyika kwa ajili ya udini bali ni moja ya matokeo ya kiutendaji.

Alimtupia lawama na kumtaja diwani Mhina kuwa ndiye anayechochea mgogoro huo kwa kueneza udini kuwa yeye anawapendelea waislamu jambo ambalo ni hatari.

Chanzo: Nipashe Jumapili

Makucha ya Ibilisi yanaanza kuchomoka taratibu.
 
Sina uhakika kama Rais anajua jinsi Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanavyoamrisha watumishi wa Serikali kuwekwa kizuizini ( wao wanaita kuweka ndani). Kwa Mkoa wa Tanga kitendo hiki ni cha kawaida kabisa. Mtu asiposimama RC au DC akipita anaamriwa kuwekwa kizuizini.
Mambo yanayofanyika mkoani Tanga ni HERI WAKATI WA MKOLONI
 
Back
Top Bottom