DC na DED mpya Siha kuweni makini na watu hawa

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Hivi karibuni Serikali iliwaapisha mkuu mpya wa wilaya ya Siha,Thomas Apson(aliyetokea wilayani Mwanga) pamoja na mkurugenzi mpya,Upendo Mangali(aliyetokea mkoani Kigoma) kwenda kwenye vituo vyao vya kazi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Sisi kama wadau wa maendeleo wilayani Siha tunaamini kwamba mabadiliko yaliyofanywa na serikali yataleta tija na maendeleo katika wilaya yetu ya Siha.

Lakini pamoja na mabadiliko haya tumeona ni vyema kuwatahadharisha viongozi hawa wapya kuwa makini na baadhi ya watu katika wilaya hii ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wapika majungu,wachonganishi,wafitini,waongo,wachumia tumbo na kikwazo cha maendeleo.

Namba moja ni Mbunge wa Siha,DR. GODWIN MOLLEL

Huyu ni kikwazo namba moja katika maendeleo ya halmashauri ya Siha kwasababu amekuwa akishiriki mbinu mbalimbali za kukwamisha utendaji katika halmashauri ya Siha.

Pamoja na kwamba ni mwakilishi wa wananchi lakini amekuwa akiingilia masuala ya utendaji wa halmashauri kwa sababu zake za kisiasa(political interest)

Kwa mfano huyu ndiye aliyechangia kuivuruga halmashauri ya Siha kipindi cha mwendazake alishiriki mbinu za kumtimua aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Godson Ngumuo kwa sababu tu alijua kwamba atapambana naye katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Siha mwaka 2020.

Dr Mollel pia alishiriki katika mbinu za kuwatimua baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo akiwemo aliyekuwa mkurugenzi, Valerian Juwal na Frank Maleto(mweka hazina)kwasababu tu walikuwa kikwazo katika kutimiza malengo yake mbalimbali katika halmashauri hiyo.

Katika mbinu ya kuwatimua aliwatumia aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo,Onesmo Buswelu na Mkurugenzi wake,Ndaki Mhuli kwasababu tu walikuwa wameunda umoja mtakatifu wa kuitafuna halmashauri hiyo kwa maslahi yao.

Pia Dr Mollel ameshiriki kukwamisha mambo mbalimbali katika.halmashauri ya Siha kwa mfano ujenzi wa hospitali ya wilaya ambapo aliungana na Buswelu pamoja na Ndaki kupitisha azimio la kuagiza milango na vigae vya hospitali hiyo bila kufuata taratibu za manunuzi kwa maslahi yao na hawajawahi kuhojiwa popote pale kwann walifanya hivi kinyume na taratibu na manunuzi.

Mbunge huyu anatajwa kama mtu mchonganishi,mfitini na vinyongo kwa kuwa yoyote ambaye anashindwa kutimiza malengo yake atatumia mbinu yoyote ili aweze kumwondoa kwa gharama yoyote na watumishi wengi wanamtaja kama ni mtu mwenye mbinu na mikakati michafu pindi maslahi yake ya ubunge yanapoguswa.


No,2 DUNCAN URASSA

Huyu ni mwenyekiti wa halmashauri ya Siha tatizo la huyu kiongozi ni kutokuwa na msimamo katika kusimamia masuala mbalimbali yenye maslahi kwa halmashauri hiyo.

Urassa anatajwa kama ni mtu asiye na makuu lakini likija suala la msimamo Mara zote huyumba kwa mfano aliwahi kushinikizwa na mkurugenzi aliyepita (Ndaki) pamoja na mkuu wa wilaya aliyepita(Onesmo) kwamba ni lazima asaini nyaraka ya kumwondoa mwenyekiti wa halmashauri hiyo (Ngumuo) na kama akishindwa basi hatopitishwa kwenye kura za maoni za CCM katika uchaguzi uliopita.

Kutokana na kutokuwa na msimamo Urassa pamoja na madiwani wengine walisaini nyaraka hiyo na kisha kufanikiwa kumwondoa mwenyekiti huyo ambaye alipigwa vita kutokana na kusimamia maslahi ya watumishi wa halmashauri huyo ambao walikuwa wakinyanyaswa na kufukuzwa hovyo bila taratibu.,kanuni na sheria za utumishi wa umma.

TAKUKURU & POLISI

Pamoja na kwamba vyombo vya Takukuru na Jeshi la Polisi wilayani Siha kufanya kazi kubwa sana katika kusimamia maslahi ya serikali kama matumizi sahihi ya fedha za umma, usalama wa RAIA na Mali zao lakini kwa upande mwingine vyombo hivi vinatajwa kama kutumika kukandamiza haki za watumishi.

Vyombo hivi vimekuwa vikilalamikiwa sana kutumika na baadhi ya watu katika kukandamiza haki kwa wanyonge kwa maslahi ya baadhi ya watu na hii imepelekea kwa kiasi kikubwa kuvifanya kutoaminika mbele za wananchi.

Kwa mfano Takukuru wilayani Siha chini ya aliyekuwa mkurugenzi wake ,Deo Mtui iliwahi kumwita na kumhoji aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo( Ngumuo) kwa kile wanachodai alikuwa akijipa kazi mbalimbali za halmashauri hiyo na kisha kukwepa kodi.

Jambo la ajabu baada ya kumhoji na kisha kumwachia baada ya kukosa ushahidi wa kutosha mpaka Leo yapata takribani miaka mitatu sasa Takukuru wilayani Siha hawajarejesha simu ya kiongozi huyo pamoja na kuifuatilia bila mafanikio mpaka sasa.

Jambo jingine Takukuru wilayani Siha wamekuwa wakiwahoji baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo ambao walifukuzwa kazi akiwemo Aliyekuwa mweka hazina(Frank Maleto) na aliyekuwa mkurugenzi (Valerian Juwal) kwa takriban miaka mitatu sasa bila upelelezi kukamilika.

Watumishi hawa wamekuwa wakiripoti miaka nenda rudi katika ofisi za Takukuru wilayani Siha jambo la kushangaza ambalo kila mmoja anajiuliza je ni uchunguzi gani ambao umekuwa ukichukua zaidi ya miaka minne bila kukamilika?je kuna nn kinaendelea?

Lakini pia jeshi la polisi wilayani Siha halikwepi lawama katika kukandamiza haki za raia wilayani Siha kwa kuwa Mara kwa Mara linatajwa kutumika na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu kupokea maelekezo ambayo kimsingi yanaharibu taswira nzuri ya jeshi letu.

Kwa mfano mwaka juzi jeshi hili liliawakamata baadhi ya watumishi kwa maelekezo ya Mkuu wa wilaya aliyehamishwa(Onesmo Buswelu) na kisha kuwafikisha katika kituo cha polisi cha Sanya Juu na kuwashikilia kwa siku 40 bila dhamana.

Kitendo cha kuwashikilia watumishi hawa kwa siku 40 na kisha kuwaachia bila kuwafikisha mahakamani kilitoa picha hasi kwa jeshi la polisi na kupelekea baadhi ya RAIA kutokuwa na imani na jeshi hili.

WITO WANGU

Wito wangu kwa viongozi wapya ni kuwa makini na waliotajwa hapo juu wakati mkitekeleza majukumu yenu jiepusheni sana na majungu,fitina na maneno ya uchonganishi mjitahidi kufanya kazi kwa weledi,taratibu,kanuni,sheria na hofu ya Mungu na ninaamini mkiyafuata haya mtafanikiwa.

Ninaamini kabisa Rais Samia Suluhu Hassan aliwateua kwa kuwaamini kwamba mtamsaidia kazi na hamtamwangusha hivyo wananchi wana matumanini makubwa sana kwamba mtawavusha salama katika nyanja za kimaendeleo Mungu awatangulie.(itaendelea)

Kazi iendeleeeee...........

Ndimi Mzalendo
 
Mkurugenzi mpya wa halmashauri ya Siha,Upendo Mangali
IMG_20210827_093025_775.JPG
 
Sawa Mr. Ngumuo tumekusikia. Sisi kama Serikali tunafanya shughuli zetu kwa kufuata misingi ya haki na ustawi wa wananchi wetu.

Hivyo tutazifanyia kazi hizi shutuma zako. Maana Serikali ya chama cha mapinduzi ni serikali sikivu sana.
 
Back
Top Bottom