Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasary na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro walijikuta wakigeuz msiba wa Mkurugenzi wa Aicc Elishilia Kaaya aliyefiwa na baba yake mzazi kuwa uwanja wa mapambano na mifasho ya kisiasa.
Wakati Nasary akiwaomba radhi wananchi wake wa jimbo hilo kwa kutoonekana jimboni kwake kwa muda mrefu akisaka wafadhili wa maendeleo ,Muro alisema serikali haisubiri wafadhili katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Nasary pamoja na Mambo mengine alitaka wananchi hao wamsamehe kwa kutoonekana jimboni kwake kwa muda mrefu kwa kuwa alikuwa akisaka wafadhili wa maendeleo nchini Marekani.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alitumia wasaa huo kumjibu Mbunge huyo kwa kumweleza kuwa wakati hayupo jimboni kwake shughuli za maendeleo zimetekelezwa kwa kiwango kikubwa kwani serikali imetoa kiasi cha sh,bilion 1 kwa ajili ya maendeleo ya Afya pamoja na kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya Huduma zingine wilayani humo.
Muro alimwambia Nasari kuwa hawawezi kusubili wafadhili bali serikali inatekeleza kwa vitendo.
Msiba huo ulihudhuliwa na mkuu wa Majeshi Wa kwanza mstaafu Jenerali Mirisho Sarakikya , Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,Mbunge wa Arumeru Joshua Nassari na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro leo wakati wa Mazishi ya Mzee Daniel Saitore Kaaya(93) huko kijiji cha Nguruma Arumeru leo jioni ambao walijikuta wakibaki vinywa wazi wakati mipasho ya vigogo hao ikitamalaki.
Sent using Jamii Forums mobile app