Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, ametoa msaada wa vyakula vya futari na Eid kwa wafungwa wa Gereza la Wanawake Kingolwira na Gereza la Mahabusu Morogoro.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Gereza la Wanawake Kingolwira, SP Atupelye Luwanja, alimshukuru DC Kilakala kwa moyo wa upendo na kuwajali wafungwa katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.
Naye Mkuu wa Gereza la Mahabusu Morogoro, SSP Alfred Lemgoha, amepongeza hatua hiyo, akisema ni kitendo cha kiungwana kinachoonesha mshikamano na upendo kwa wafungwa.