DC Mussa Kilakala - Tanzania ni Baba wa Demokrasia, Viongozi Wanapatikana kwa Ridhaa ya Wananchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,695
1,241

DC MUSSA KILAKALA - TANZANIA NI BABA WA DEMOKRASIA, VIONGOZI WANAPATIKANA KWA RIDHAA YA WANANCHI

"Hali ya Wilaya ya Morogoro ni shwari, wananchi wengi wanaendelea kujitokeza kwaajili ya kujiandikisha ili wapate fursa ya kupiga kura ifikapo tarehe 27 Novemba, 2024. Tunatambua tarehe 11 Oktoba, 2024 Rais Samia Suluhu Hassan aliowaongoza Watanzania katika zoezi la kujiandikisha" - Mhe. Mussa Kilakala, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro

"Rais Samia Suluhu Hassan ametoa siku ya tarehe 27 Novemba, 2024 iwe ni mapumziko. Siku hii wananchi wote wa Wilaya ya Morogoro tutakuwa na fursa ya kupiga kura" - DC Mussa Kilakala

"Naomba niendelee kuwahamasisha wale ambao bado hawajajiandikisha katika Wilaya ya Morogoro wajitokeze kwa wingi ili wapate fursa ya msingi ya kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024" - DC Mussa Kilakala

"Wote tunafahamu Tanzania ni Baba wa Demokrasia ndani na nje ya Tanzania na viongozi wake wanapatikana kwa ridhaa ya wananchi. Ni muda sasa wa kwenda kuchagua viongozi ambao tunawahitaji kwa maslahi mapama ya Amani, Maendeleo na kutuweka pamoja kama Watanzania kama watu wa Morogoro" - Mhe. Mussa Kilakala, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-10-17 at 13.32.38.mp4
    11 MB
Back
Top Bottom