DC Hapi amtembelea rais wa awamu ya pili nyumbani kwake

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
DC HAPI AMTEMBELEA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI NYUMBANI KWAKE.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo mchana ametembelea Rais mstaafu wa awamu ya pili Mh. mzee Ali Hassan Mwinyi nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es salaam.

Akiwa nyumbani kwa mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni walizungumzia mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya Kinondoni na historia ya nchi kwa ujumla. Rais mstaafu alimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa uamuzi wake wa kumtembelea na kumtakia kheri katika majukumu yake.

Aidha mh. Mkuu wa Wilaya alimshukuru Rais mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi na kumtakia afya njema na maisha marefu.

d3cf5eb47a5261e8ac3c44c7f4c75c99.jpg
 
je katika job descrption yake kuna sehemu imeandikwa atembelee kaya za wilayani kwake? makatibu tarafa wafanye kazi gani, makatibu kata, wenyeviti wa mitaa na vitongoji!!! ndio maana JPM hapendi wazururaji!!! , DC chapa kazi acha kuzurura mheshimiwa
 
Kazi ya kwanza ya DC ni kupokea Mwenge katika wilaya yake.Kazi ya pili ni ulinzi na usalama wa wilaya yake (Mwenyekiti).Kazi tatu ni kutembelea magodown ya sukari kuhakikisha wafanyabiashara hawafichi bidhaa adimu.
 
Leo hajatinga gwanda?? maana hawa jamaa hawaishiwi maigizo
 
kama kijana ni muhimu kutembelea wazee, huwezi fahamu unapata baraka kiasi gani. Mi naona ni mfano mzuri kwa viongozi wa wilaya kuwatembelea wazee waliopo karibu na mipaka yao.
 
N
kama kijana ni muhimu kutembelea wazee, huwezi fahamu unapata baraka kiasi gani. Mi naona ni mfano mzuri kwa viongozi wa wilaya kuwatembelea wazee waliopo karibu na mipaka yao.
Ni kweli halafu licha ya baraka unajua ukiwa kiongozi unahitaji ushauri wa hapa na pale ili kuzidi kuboresha zaidi utendaji wa kazi. uongo mbaya experience matters!
 
Huyu jamaa anavaa magwanda ya mgambo halafu anapanda kwenye VX V8, Maigizo mengine hata hayaendani.
 
Back
Top Bottom