DC Hapi amsimamisha kazi mwanasheria manispaa ya Kinondoni

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amemsimamisha kazi mwanasheria wa manispaa ya Kinondoni, Anord Kinyaiya.

Kinyaiya amesimamishwa kazi leo Jumanne Julai 24, 2018 kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwakumbatia watu wanaolalamikiwa na wananchi.

Hapi amechukua uamuzi huo baada ya wananchi kutoa kero zao katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kinondoni Shamba, wakiwemo wafanyakazi 13 wa kampuni ya kuzoa taka ya Total West Solution walioeleza jinsi wanavyozungushwa kulipwa kiasi cha Sh15milioni wanazodai.

Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Ridhiwan Hussen amesema waliwasilisha malalamiko yao kwa mkuu huyo wa wilaya na kutakiwa kwenda kwa mwanasheria huyo ili wapitie madeni wanayoidai kampuni hiyo.

Amedai walipofika kwa Kinyaiya aliwazungusha na kuwatamkia wazi kuwa Hapi hana mamlaka ya kushughulikia suala lao.

“Binafsi ninadai mshahara wa miezi 11, watu wote 13 tunadai Sh15milioni, hata tunapokwenda ofisini kwa mwanasheria, meneja wa kampuni nae hatokei na wamekuwa na utaratibu wa kuwasiliana wao wenyewe, kwa kweli inatupa shaka sana,” amesema Hussein.

Amesema anashangazwa na Kinyaiya kuwapendelea wenye fedha badala ya wananchi wanyonge wanaodai haki yao.

“Ninakusimamisha kazi na sitaki kukuona katika ofisi yangu. Ninataka wakuchunguze hayo mambo unayolalamikiwa na ikibainika utachukuliwa hatua za kisheria,” amesema Hapi.

“Polisi mkamateni huyu meneja popote atakapokuwepo na awekwe ndani kwa saa 48 na baadaye achukuliwe hatua za kisheria ili awalipe vijana hawa mishahara yao.”

Kwa upande wake Kinyaiya alikanusha madai kuwa aliwaeleza wafanyakazi hao kuwa suala lao haliwezi kupatiwa ufumbuzi na Hapi, kubainisha kuwa alikuwa akishughulikia madai yao.

Chanzo: Mwananchi
 
bwana happy huna na hutakuwa na hayo mamlaka ya kumsimamisha kazi mwanasheria. wewe sio mamlaka yake ya ajira.
 
wewe huna tofauti na fatuma karume,kapitie sheria na kanuni kwanza
mamlaka ya ajira halmashaur ni mkurugenzi acha uzuzu wako. atamsimamisha ili aonekane kwenye taarifa ya habar amekunja ndita tu kwakuwa kiongozi wenu ndivyo anavyowajaza upepo nanyi mkajaa . kila kitu mnatishana mnatisha mnafukuza badala ya kuibomoa mifumo ambayo ndiyo tatizo hasa
 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amemsimamisha kazi mwanasheria wa manispaa ya Kinondoni, Anord Kinyaiya.

Kinyaiya amesimamishwa kazi leo Jumanne Julai 24, 2018 kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwakumbatia watu wanaolalamikiwa na wananchi.

Hapi amechukua uamuzi huo baada ya wananchi kutoa kero zao katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kinondoni Shamba, wakiwemo wafanyakazi 13 wa kampuni ya kuzoa taka ya Total West Solution walioeleza jinsi wanavyozungushwa kulipwa kiasi cha Sh15milioni wanazodai.

Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Ridhiwan Hussen amesema waliwasilisha malalamiko yao kwa mkuu huyo wa wilaya na kutakiwa kwenda kwa mwanasheria huyo ili wapitie madeni wanayoidai kampuni hiyo.

Amedai walipofika kwa Kinyaiya aliwazungusha na kuwatamkia wazi kuwa Hapi hana mamlaka ya kushughulikia suala lao.

“Binafsi ninadai mshahara wa miezi 11, watu wote 13 tunadai Sh15milioni, hata tunapokwenda ofisini kwa mwanasheria, meneja wa kampuni nae hatokei na wamekuwa na utaratibu wa kuwasiliana wao wenyewe, kwa kweli inatupa shaka sana,” amesema Hussein.

Amesema anashangazwa na Kinyaiya kuwapendelea wenye fedha badala ya wananchi wanyonge wanaodai haki yao.

“Ninakusimamisha kazi na sitaki kukuona katika ofisi yangu. Ninataka wakuchunguze hayo mambo unayolalamikiwa na ikibainika utachukuliwa hatua za kisheria,” amesema Hapi.

“Polisi mkamateni huyu meneja popote atakapokuwepo na awekwe ndani kwa saa 48 na baadaye achukuliwe hatua za kisheria ili awalipe vijana hawa mishahara yao.”

Kwa upande wake Kinyaiya alikanusha madai kuwa aliwaeleza wafanyakazi hao kuwa suala lao haliwezi kupatiwa ufumbuzi na Hapi, kubainisha kuwa alikuwa akishughulikia madai yao.

Chanzo: Mwananchi
Huu ni ubashite mwingine, unamsimisha mtu kazi kwa kusikiliza majungu ya uswahilini
 
mamlaka ya ajira halmashaur ni mkurugenzi acha uzuzu wako. atamsimamisha ili aonekane kwenye taarifa ya habar amekunja ndita tu kwakuwa kiongozi wenu ndivyo anavyowajaza upepo nanyi mkajaa . kila kitu mnatishana mnatisha mnafukuza badala ya kuibomoa mifumo ambayo ndiyo tatizo hasa
mkurugenzi na Dc nani mkubwa?
kasome vizuri Local government authorty act ujionee mwenyewe badala ya kumwaga povu
 
sio swala la ukubwa ni suala la mamlaka husika. kwani watumishi wa halmashaur wanawajibika kwa nani mkuu? mengine wala hayahitaji kusoma ni kuelewa tu. mkurugenzi ndio msimamizi wa watumishi pale niambie Dc anapata wapi mamlaka ya kusimamisha kazi mtu?
 
Mwanasheria nae anasimamishwa kirahisi tu.....au ni kiki ...maana leo Happy alikuwa Clouds kujipromot
 
mkurugenzi na Dc nani mkubwa?
kasome vizuri Local government authorty act ujionee mwenyewe badala ya kumwaga povu
kwa hiyo dc anaweza kuzuia pesa ya halmashauri isitumike? kwa maana ya accounting officer?
 
mkurugenzi na Dc nani mkubwa?
kasome vizuri Local government authorty act ujionee mwenyewe badala ya kumwaga povu
acha ubishi mkuu wa wilaya hana mamlaka yyte ya kumsimamisha mtumishi yoyote kazi hata wale wa ofisini kwake mamlaka anayo katibu tawala sio DC.
na kwa upande wa halamashauri hata Mkurugenzi hana mamlaka ya kumfukuza mtumishi kazi-mwenye mamlaka hayo ni bodi ya ajira ambaye mwenyekiti wake ni meya au mwenyekiti wa halmashauri husika.
 
Mwanasheria nae anasimamishwa kirahisi tu.....au ni kiki ...maana leo Happy alikuwa Clouds kujipromot
yani mkuu hawa wanajua mkuu wao anataka nn .misifa ya kijinga ndio maana . embu angalia taarifa ya habar kila mtu anamtisha mwenzie? taarifa ya habar zote zimejaa siasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom