DC Hai amtupa rumande saa 48 diwani wa CCM

DC Hai amtupa rumande saa 48 diwani wa CCM

Kwani hilo shamba amelipata vipi hadi apokonywe?
 
Ila hili jamaa ni fisadi kweli arusha yenyewe amejimilikisha vibanda vya manispaa vingi kinyamaa anakwepa kodi au anakushikia chini aliyekupangishia ukalipe manispaa kodi ambayo ni vingine laki au elfu hamsini kwa mwezi na bado umlipe kodi yake yeye laki tano mpka saba kwa mwezi, alikuwa anamiliki choo apa stand ndogo unalipia mia mbili na hatoi risiti yeyote wakamshtukiaga saivi kakinyanganywa, ana nyumba maeneo ya jr kiwanja cha iyo nyumba yake alimtapeligi mama mjane mmoja akishirikiana na mwenyekiti tapeli wa mtaa wa banda mbili maarufu kwa jina la chopo bahati mbaya au nzuri uyu mwenyekiti ni wa chadema anawaliza watu wengi sana naona karma imegeukia kipande yake sasa tapeli huyu
Huyu tapeli bado analindwa, siku hizi ni mwenyekiti wa halmashauri ya Moshi vijijini na diwani kata ya ukaoni...anafanya UONEVU na kwa kutumia cheo chake hakuna wa kufanya CHOCHOTE. Wananchi WANAONEWA nae
 
Hai. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amemsweka ndani saa 48 , Diwani wa Okaoni (CCM), Moris Makoi na kutengua umiliki wake wa shamba la kahawa la Nkwansira lenye ukubwa wa ekari zaidi ya 500.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika Kijiji cha Nkwansira, DC huyo amesema mwekezaji huyo ambaye ni Diwani ameshindwa kuendeleza shamba hilo na kusababishia serikali hasara kwa kutokulipa kodi.

Aidha amesema mwekezaji huyo amekua akiwanyanyasa wafanyakazi katika shamba hilo na kuwanyima mishahara.

"Kuanzia leo nimetengua maamuzi ya kikao cha wajumbe 31 waliopitisha na kummilikisha shamba hili mwekezaji huyu hivyo, simtambui pamoja na shughuli zake zote ndani ya wilaya hii,"amesema Mkuu huyo.

Mkuu huyo amechukua hatua hiyo, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kijiji hicho wakimlalamikia mwekezaji huyo kutokana na matumizi mabaya ya shamba hilo ambalo ameshindwa kuliendeleza na badala yake kulibadilisha matumizi.

Pia, amesema amekua akikwepa kodi na hajawahi kuona kumbukumbu zozote za kulipa kodi kwa mwekezaji huyo na kwamba hamtambui.
"Sina kumbukumbu zozote za mwekezaji huyu na simtambui katika wilaya hi,"amesema Sabaya.

"Haiwezekani shamba hili ambalo amepewa na serikali kulima kahawa alitumie kulishia mifugo na kuotesha maharage,"amesema.

Wakizungumzia kuondolewa kwa mwekezaji huyo, wananchi wa kijijini hicho wamefurahishwa na uamuzi ya mkuu huyo na kuomba shamba hilo lirudi mikononi mwa wananchi.

Mmoja wa wanakijiji hao, Remani Ulomi amemsema shamba hilo lingeweza kutoa ajira nyingi kwa vijana kwani tangu mwekezaji huyo apewe eneo hilo ameshindwa kutoa ajira kwa vijana hao.

"Shamba hili limekua pori, ameshindwa kuliendeleza na ajira hapa hatuna zaidi shamba hili limejaa kila ina ya wanyama, tunaomba shamba hili lirudi mikononi mwetu hatumtaki mwekezaji huyu"amesema. Hata hivyo, amemuagiza Kaimu Ofisa ushirika wa Wilaya hiyo, Joel Marandu kutoa ekari 10 kwa wananchi hao na utekelezaji wake uanze mara moja ili wananchi hao wanufaike na ardhi yao.

Chanzo: Mwananchi
Moris Makoy amezoea kujimilikisha Mali za serikali. Jijini Arusha ALIWAHI kupata tenda ya kukusanya Kodi za pango kwa niaba ya jiji katika vibanda vya stendi ndogo. Alitumia nafasi hiyo kuwanyang'anya wenye malimbikizo ya kodi na kuvigeuza vibanda hivyo ni vyake. Akaanza kupangishia wananchi na kulipisha Kodi kuanzia shilingi laki nne mpaka milioni Moja kwa mwezi na Kodi hiyo ilipwe kwa mwaka. Wakati huo alikuwa hapeleki fedha jiji na kusababisha migogoro na jiji kwani walikuja kufungua vibanda vya wafanyabiashara halisi wanaofanya biashara hapo. Moris ndio chanzo Cha kupanda kwa Kodi mara dufu staendi ndogo na ni chanzo kikubwa Cha mgogoro uliopo stendi ndogo. Stendi hiyo imehodhiwa na watu wachache wanajiita wajenzi kitu ambacho sio Cha kweli..wengi walinunua vibanda hivyo kwa waliomaliza mkataba na jiji wa ujenzi wa miaka kumi...Moris Makoy ni mnyanyasaji sana na analindwa popote pale anapofanya unyang'anyi ama uhalifu. Kwa kutumia hicho cheo Cha mwenyekiti wa halmashauri
 
Back
Top Bottom