DC Hai amtupa rumande saa 48 diwani wa CCM

DC Hai amtupa rumande saa 48 diwani wa CCM

NGolo Kante

Member
Joined
Feb 28, 2017
Posts
80
Reaction score
131
Hai. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amemsweka ndani saa 48 , Diwani wa Okaoni (CCM), Moris Makoi na kutengua umiliki wake wa shamba la kahawa la Nkwansira lenye ukubwa wa ekari zaidi ya 500.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika Kijiji cha Nkwansira, DC huyo amesema mwekezaji huyo ambaye ni Diwani ameshindwa kuendeleza shamba hilo na kusababishia serikali hasara kwa kutokulipa kodi.

Aidha amesema mwekezaji huyo amekua akiwanyanyasa wafanyakazi katika shamba hilo na kuwanyima mishahara.

"Kuanzia leo nimetengua maamuzi ya kikao cha wajumbe 31 waliopitisha na kummilikisha shamba hili mwekezaji huyu hivyo, simtambui pamoja na shughuli zake zote ndani ya wilaya hii,"amesema Mkuu huyo.

Mkuu huyo amechukua hatua hiyo, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kijiji hicho wakimlalamikia mwekezaji huyo kutokana na matumizi mabaya ya shamba hilo ambalo ameshindwa kuliendeleza na badala yake kulibadilisha matumizi.

Pia, amesema amekua akikwepa kodi na hajawahi kuona kumbukumbu zozote za kulipa kodi kwa mwekezaji huyo na kwamba hamtambui.
"Sina kumbukumbu zozote za mwekezaji huyu na simtambui katika wilaya hi,"amesema Sabaya.

"Haiwezekani shamba hili ambalo amepewa na serikali kulima kahawa alitumie kulishia mifugo na kuotesha maharage,"amesema.

Wakizungumzia kuondolewa kwa mwekezaji huyo, wananchi wa kijijini hicho wamefurahishwa na uamuzi ya mkuu huyo na kuomba shamba hilo lirudi mikononi mwa wananchi.

Mmoja wa wanakijiji hao, Remani Ulomi amemsema shamba hilo lingeweza kutoa ajira nyingi kwa vijana kwani tangu mwekezaji huyo apewe eneo hilo ameshindwa kutoa ajira kwa vijana hao.

"Shamba hili limekua pori, ameshindwa kuliendeleza na ajira hapa hatuna zaidi shamba hili limejaa kila ina ya wanyama, tunaomba shamba hili lirudi mikononi mwetu hatumtaki mwekezaji huyu"amesema. Hata hivyo, amemuagiza Kaimu Ofisa ushirika wa Wilaya hiyo, Joel Marandu kutoa ekari 10 kwa wananchi hao na utekelezaji wake uanze mara moja ili wananchi hao wanufaike na ardhi yao.

Chanzo: Mwananchi
 
Haya mamlaka ya madc kuwasukuma watu ndani yalikua ya wakolon
Kwa karne
Hii bado hayo mamlaka wanayo kana kwamba ni wafalme. Its too much
 
Siku zote huwa naamini Tanzania haiendelei kwa ajili ya roho mbaya walionao wananchi zidi ya wananchi wenzao. Msingi wa haya mambo ni ujamaa. Tanzania ukiwa tajiri utachukiwa mpaka na mwenyekiti wa kitongoji kapuku asiyejiweza
 
tumeipenda wenyewe mmmmm
acha waisome namba eeeeee
wajinga wale................
ccm mbele kwa mbele

huyu diwani alikuwa mstari wa mbele kuimba na kupiga pushup kwenye kampeni...
Pich please, na sisi wanachama wa CUF tumuone
 
Shule, shule, shule, shule shule shule
Sasa hili ndio jibu ya swali nililouliza ? Kwamba sijaenda shule kisa nimeuliza Dc ana mamlaka ya kumnyang'anya mtu ardhi anayo miliki kihalali ?
 
Kinachonishangaza zaidi kwa hawa sijui niwaitaje
Kwa kumweka mtu ndani wanaona ni sifa au?
Maana unapoonyesha ubabe wa namna hii wengine tunaona sio busara kabisa na ni kujidhalilisha mwenyewe huku ukijiona ufahari.

Yaani na usingizi unapita ukijisemea "nimemuweka ndani"

Kwani wakitoa maamuzi bila kumuweka ndani mtu ujumbe hautufikii
 
Ila hili jamaa ni fisadi kweli arusha yenyewe amejimilikisha vibanda vya manispaa vingi kinyamaa anakwepa kodi au anakushikia chini aliyekupangishia ukalipe manispaa kodi ambayo ni vingine laki au elfu hamsini kwa mwezi na bado umlipe kodi yake yeye laki tano mpka saba kwa mwezi, alikuwa anamiliki choo apa stand ndogo unalipia mia mbili na hatoi risiti yeyote wakamshtukiaga saivi kakinyanganywa, ana nyumba maeneo ya jr kiwanja cha iyo nyumba yake alimtapeligi mama mjane mmoja akishirikiana na mwenyekiti tapeli wa mtaa wa banda mbili maarufu kwa jina la chopo bahati mbaya au nzuri uyu mwenyekiti ni wa chadema anawaliza watu wengi sana naona karma imegeukia kipande yake sasa tapeli huyu
 
Kumbe alishazoea acha sheria ifuate mkondo wake wallah
 
mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm wilaya ya Hai Bw ole Lengai amemuweka ndani Mjumbe mwenzake wa mkutano mkuu wa ccm wilaya ya Hai ndugu Morris.

ccm oyee!

note: byakanwa alipomvuruga mbowe alikula shavu, sasa huyu nae anasaka plate number tu.
 
Pich please, na sisi wanachama wa CUF tumuone

Umenikumbusha sakata la CUF Temeke Mwembe yanga siku profesori alipochomekewa tanganyika jeki, naona this time amesoma alama za nyakati akaamua ku mute
 
tumeipenda wenyewe mmmmm
acha waisome namba eeeeee
wajinga wale................
ccm mbele kwa mbele

huyu diwani alikuwa mstari wa mbele kuimba na kupiga pushup kwenye kampeni...

Wakati mwingine rejea tukio la cag kuulizwa kadamnasini kuhusu 1.5 tril
 
Back
Top Bottom