DC autamani Uongozi wa UVCCM Mkoani Arusha……… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC autamani Uongozi wa UVCCM Mkoani Arusha………

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Sep 14, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya kushangaza mmoja kati ya vijana aliyepata zawadi ya U-DC kwa kuiwakilisha moja kati ya Wilaya zilizopo Mkoani Tanga ameonekana kuutamani nafasi ya uongozi wa juu ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoani Arusha.

  Ila baada ya kugundua kuwa hana vigezo na wala hatoshei ameona bora ampigie kampeni yule ambaye ataweza kumtumia kwa maslahi na kwa manufaa yake binafsi na si kwa maslahi ya Vijana wa Arusha. Hata hivyo vijana Mkoani Arusha wamegundua hilo na wameamua kumtumia ujumbe DC huyo kwa kupitia watu wake wa karibu akiwemo mgombea mwenyewe.

  Habari kutoka Ngorongoro, Karatu na Arusha Mjini zinasema kuwa japo Kampeni bado ila DC huyo ameamua kutelekeza kazi yake aliyopewa na Mhe Raisi na amekuwa akipita huko kumwombea kura huyo ambaye yeye anatamani ashinde ili aweze kutumikiwa yeye kinyume na Kanuni za Jumuiya na wakati wote amekuwa akihudhuria vikao vya uchaguzi japo si mjumbe.

  Hata hivyo DC huyo ameonywa na Vijana katika Mkoa husika abaki katika Kituo chake cha kazi na kumtumikia yule aliyempa wajibu huo badala ya kuendelea kumwaibisha, vile vile DC huyo amepongezwa kwa namna ambavyo anamtengenezea mgombea nafasi nzuri ya KUSHINDWA kama ambavyo yeye aliwahi kushindwa katika uchaguzi wa namna hiyo.

  Wakati huo huo vijana Mkoani hapa wamempongeza sana M’kiti mteule wa Jumuiya hiyo katika ngazi ya Wilaya (Arusha Mjini) aliyechaguliwa hivi karibuni kwa namna alivyomuumbua DC huyo pale ambapo DC huyo alipojikosha kwa kutoa ofa kwa washindi wa Jumuiya hiyo akiwepo M’kiti huyo kwenda Lushoto eti kwa fungate.

  M’kiti huyo mteule baada ya kutumia hekima na busara zake aligundua kuwa ofa ya DC huyo ni za hila, fitina, unafiki, na uzindaki kwamba alitaka washindi hao waende Lushoto ili akaendeleze Kampeni za kuwatafutia Vijana wa Arusha kiongozi, hivyo katika hotuba yake iliyoonesha ukomavu wa Kisiasa na hekima ya hali ya juu M’kiti huyo alimtaka DC huyo aachane kabisa na fikra hizo za kialinacha na kipinokyo zilizojaa ubatili na ufinyu wa mawazo na kama kweli ana nia hiyo basi fedha hizo za fungate aziingize kwenye SACCOS ya Vijana.

  Sasa basi the so called DC is urged kufanya haya;

  1. Kwamba, akamwombe msamaha mgombea anayempigia Kampeni kwa kumtengenezea mazingira mazuri sana ya KUSHINDWA,

  2. Kwamba, aache na akome kabisa kulitumia jina la Mhe Raisi vibaya katika kuomba kura kwa mbwembwe kwamba ametumwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa,

  3. Kwamba, ajiulize ni kwa nini alipata kura 6 alipokuwa akigombea nafasi kama hiyo mwaka 2008 na ajipe jibu vile vile ni kwa nini huyo anayempigia Kampeni atapata kura 3 mwaka huu,

  4. Kwamba, Jumuiya ilishamkataa toka mwaka enzi kwa kuzingatia masharti na vigezo hivyo asifikiri U-DC wake unaweza kuifanya Jumuiya impe huyo amtakaye kura za huruma,

  5. Kwamba, atafakari sababu za kushindwa kwa Mgombea aliyemtaka Arusha Mjini,

  6. Kwamba, atambue kuwa viongozi wanaotafutwa ni wa Arusha na si wa Tanga wala Lushoto,

  7. Kwamba, atafakari vile vile ni kwa nini mgombea wa Arusha aliamua kutumia hela walizompa yeye na wenzie tena hela nyingine alipewa nyumbani kwa aliyewahi kuwa kiongozi wa Jumuiya ila mgombea aliamua kuongezea mtaji na si vile ambavyo yeye(wao) walitaka zitumike,

  8. Kwamba, aamini kuwa nafasi aliyonayo ni zawadi tu (emphasis added) na kimsingi hana sifa ya kuwa nayo ndiyo maana bado mpaka leo hajajua wajibu wake, hivyo hata sifa ya kuwa Meneja Kampeni kama hana,

  9. Kwamba, asifikiri vile ambavyo yeye alishikwa mkono na kupewa U-DC ndivyo ambavyo atashika mtu mkono kuchagulia Vijana wa Arusha kiongozi,

  10. Kwamba, aheshimu Katiba, Kanuni na Taratibu za Chama chetu ambazo kwazo viongozi hupatikana,

  11. Kwamba, amtembelee aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM ili amfunde juu ya Ahadi za MwanaTANU ambazo vile vile zipo katika Nyongeza “A” ya Katiba ya CCM hasa kile kifungu cha (5); kwamba cheo ni dhamana……………..

  12. Kwamba, awe mpole na awe mwingi wa mikakati katika Siasa na si kukurupuka, Mathalan umekuja Ngorongoro kuomba kura ila bado tunashangaa kama kweli ulikuwa na nia thabiti ya kumwombea kura huyo unayemtaka manake uliozungumza nao si tu kwamba hawahusiki kokote bali vile vile uwezo wa kukuombea kura hawana,

  13. Kwamba, akafungulie watoto account (kama anao) kwa hizo hela za U-DC na aache kuzipoteza bila malengo,

  14. Kwamba, atumikie Watanzania kadri ambavyo Mhe Raisi wetu alidhani kuwa ataweza,

  15. Kwamba, Sisi Vijana wa Arusha tumechoshwa na makundi ndani ya chama na tumeshajiandaa kutoka huko hivyo hatuko tayari U-DC wake utumike kuyaendeleza,

  16. Kwamba, ajifunze kupitia umakini na umahiri wa M’kiti mpya wa Arusha mjini,

  17. Kwamba, atambue kuwa hakuna kitu kibaya kama kujihalalisha kuwa wewe ni mtu wa dezo 24/7 manake kimsingi elimu yake ni ya dezo, kazi aliyobahatika kuwa nayo ni ya dezo, maisha aishiyo ni ya dezo.………..

  18. Kwamba, atafute namna ya kuendelea kutetea zawadi aliyopewa kwa kujituma na kuwajibika ipasavyo manake kuipata tena ni sawa na kukutanisha Ardhi na Mbingu.

  Naomba vile vile nimkumbushe nelo hili kwa kuwa naona yupo mbali sana na Quran Takatifu “Success is really attained by him who purifies it, and failure is really suffered by him who pollutes it” Sura Ash-Shams 91, Aya 9, 10.

  Mwisho japo si kwa umuhimu inabidi Mhe. Waziri Mkuu achukue uamuzi mgumu kwa manufaa ya Taifa letu ili basi hawa MA-DC (hasa hawa Vijana) wapelekwe kwenye kile chuo kilichopo Dodoma wakapigwe brush manake nadhani hawako sawa Kimaadili kabisa manake alianza yule wa Degree ya chu.. sasa kafuata huyu na tuzidi kutegemea wengine.
   
 2. m

  mwl JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 619
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Hee, hapo mwisho umeniacha hoi "akapigwe brush" salaaaaaaale!!!
   
 3. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,717
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  DC na KADA wa CCM. Huyo jamaa ni kundi linalompinga EL. Alishafukuzwa uanachama wa JVCCM, lakini ni Swahiba wa Mwana wa Mfalme
   
 4. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,834
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Ungepeleka kwenye gazeti hii makala yako
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,328
  Likes Received: 191
  Trophy Points: 160
  Just be straight! Huyo ni Mrisho Gambo, kijana aliyemwambia mwanasheria wa wilaya huko Korogwe kwamba digrii yake ni ya c.h.u.p.i! Poor boy!
   
 6. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,834
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Kuna watu ni mafundi wazuri sana kwa kuandika umbea
   
 7. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hahahah duh matatizo ya kupewa vyeo kishikaji
   
 8. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mrisho Gambo sio mtu smart. Sio mtu strategic wala hana sifa za uongozi. Ukimuangalia yeye ukamlinganisha na watu kama akina January (kwakuwa wote wamepata uongozi kama zawadi) utagundua yeye ni mtu dhaifu sana. Wala sioni kama ana akili, busara wala maarifa. Simuoni yeye kama Mtu mwenye long term prospects kwenye siasa za Tanzania.

  Anaoenekana ni mtu wa Mori, mumkari na papara. Mtu kapewa ukuu wa Wilaya juzi kama zawadi, badala ya kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kukita mizizi yake na kujizatiti yeye kila siku yuko kwenye magazeti kwakumtukana huyu, kumpiga yule, kufanya blanda hii na blanda ile. Sio mtu mtii, mnyenyekevu, mpole na mwenye busara. Ni jeuri, mwenye visirani, majivuno na visasi.

  Gambo - strategic people tends to lay low and strategies b4 making moves. They tend to build alliances and avoid unnecessary commotions and confrontations. Humuoni mwenzio January-anaongea once a month na anaongea mambo ya maana. Hajawahi kumtukana wala kumdhihaki mtu. Anajenga alliances and bridges for the long haul.
   
 9. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
   
 10. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ccm nikama pombe za kinyeji zinaweza chacha wakati wowote kunauwezekano ameona dalili za ccm zinaelekea kubaya aingie kwenye siasa
   
 11. m

  moseskwaslema Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hebu jaribuni kunipa profile yake ya taaluma kwani shule nayo ina nafasi yake.
   
 12. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu wa Lushoto inasemekana kasoma shule za kuunga unga na anajisifu kuwa eti kamaliza Shahada yake Mt. Meru Unvrty na hiki chuo Arusha kinafahamika kuwa watu huenda pale kuchukua degree zao na si kuzitafuta.

  DC huyu huyu almanusra juzi (Ijumaa) atandikwe vibao na mkongwe mmoja ndani ya Kamati ya Siasa baada ya kutaka kutumia hiyo zawadi ya UDC aliyopewa kuwaletea madharau baadhi ya Wakongwe mle ndani.
   
 13. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Filipo;

  Huyo Mrisho ni wa Korongwe kuna haka kengine ka Lushoto hovyo kabisa. Haya ni majanga ya Nchi
   
 14. B

  BigMan JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,096
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  shule ni shule tu iwe ya kuunga ama ya moja kwa moja mfano Salim ahmed Salimu alifeli kidato cha nne lakini aliweza kuunga unga mpaka kafika juu katika elimu kuliko idadi kubwa ya watu wenye elimu ya moja kwa moja
   
Loading...