DC ataka vyoo vya Kike Mashuleni

DC ataka vyoo vya Kike Mashuleni

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Muhongo amesema ipo haja kwa kila shule kujenga vyoo maalumu kwa ajili ya matumizi ya mtoto wa kike.

Akiongea katika hafla ya changizo la kupata taulo za kike zipatazo pakiti144,000 kwa ajili ya wasichana 12,000 katika mkoa wa Arusha, lililofanyika katika Hotel ya Mount Meru jijini Arusha ,Ametoa wito kwa kila shule kuhakikisha zinajenga vyoo maalumu kwa ajili ya faragha kwa mtoto wa kike pindi wanapokuwa anajisaidia kuweza kufanya na mambo mengine hasa wanapokuwa kwenye siku zake za hedhi.

"Choo cha kawaida si rafiki sana kwa mtoto wa kike kwa sababu hakimpi nafasi ya kijisitiri zaidi pale wanapokuwa na uhitaji wa kujiweka salama hivyo ni vizuri tukaanzisha kampeni ya kila shule kuwa na vyumba maalumu vya choo 'Amesema Mkuu wa wilaya .

Hata hivyo hafla hiyo ilikosa mwitikio Mkubwa wa wachangiaji na kushindwa kufikia Malengo ya kupata pakiti 144,000 za taulo za kike,ambapo kiasi cha shilingi milioni 5 tu ziliahidiwa jambo ambalo linakatisha tamaa kufikia Malengo ya kumkomboa mtoto wa kike .

Akiongea wakati wa hafla ya kampeni ya kuwasaidia wasichana wa kike kupata taulo za kike kwa ajili ya kijisitiri ,Mratibu wa taasisi ya Vision for Youth kupitia Mradi wake wa Tuwajali,Jonathan Mollel amesema lengo la taasisi hiyo ni kuwafikia wasichana wote wenye changamoto hiyo waliopo mashukeni.

Amesema wamefanya utafiki katika Mkoa wa Arusha na kubaini wasichana wapatao 12,000 katika Mkoa wa Arusha wanauhitaji wa taulo za kike sawa na pakiti 144,000 kwa mwaka zenye thamani ya sh,million 360.

[https://lh3]

[https://lh3]
 
Utakuta gharama zilizotumika kuanzia ukumbi,msosi na bahasha ya mheshimiwa inazidi walichoahidiwa...
 
Back
Top Bottom