DC aongoza maandamano kumuunga mkono Kikwete

Angekuwa nao angechakachua kura za Dr. Slaa? Lakini ata kama anao, ni wanamna gani, ni kama wewe na wengineo wanafaidika na ufisadi?
Sumaye amewaambia kuwa ni DOLA ikukubali ndipo utakuwa Rais wa Nchi hii. Dr Slaa hakubaliki kwenye DOLA yetu. Wakuu wa sasa wa vyombo vya DOLA ni WACHAFU mno.
 
Angekuwa nao angechakachua kura za Dr. Slaa? Lakini ata kama anao, ni wanamna gani, ni kama wewe na wengineo wanafaidika na ufisadi?

Hivi alichakachua kura ngapi? Yaani matokeo halali kwa mujubu wa utafiti huru yalimpa kura ngapi Dr. Slaa na kisha zikachakachuliwa kwa kiasi gani kumpa ushindi wa asilimia 61 Mheshimiwa Dr. Rais Kikwete. Pamoja na kuahidi, CHADEMA hawajawahi kuja na data tofauti za hizi za tume ya uchaguzi kuthibitisha kilio chao cha kuchakachuliwa kwenye ura za urais.
 
Duh sasa kama katika maandamano tunabeba mishale, hapa kweli tunataka amani. Halafu hao sungusungu wamefahamu majukumu yao? kama jeshi.:hug:
 
Haukatazwi kufikiri hivyo. Sote tulikuwepo mwaka 2005, 2010 hadi leo. Nje ya JF, JK bado anakubalika sana tu. Kuna wanaonufaika sana na yeye kuwa Rais wa Tz.
Kwenye RED: Nimekuandikia wasio kuwa na taarifa ndio wanamkubali i.e wavijijini, yes kuna wanaonufaika sana i.e MAFISADI. Go to Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) and click on list of shame, JK is number eleven. So kama una taarifa kama mimi kwanini humkubali?
 




SERIKALI wilayani Kwimba imesema kwamba, itawakamata na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wanasiasa watakaotumia majukwa kuitukana, kufanya uchochezi na kuhatarisha amani.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kupinga maandamano ya uchochezi, hivi karibuni mjini Ngudu, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Christopher Kangoye alisema wanasiasa ‘uchwara’ wasiifanye Kwimba uwanja wa kupangia vurugu na uchochezi.
Kangoye ambaye ni Mtemi wa jeshi la jadi la wilaya hiyo (Sungusungu) alisema hayo baada ya kupokea heshima na salamu za askari zaidi ya 2,000 wa jeshi hilo , waliodai kwamba wamechoshwa maandamaono na mikutano ya uchochezi ya wanasiasa.
“Tutawakamata wanasiasa wanaodai wanakuja kufanya mikutano kwa nia nzuri kisha wanatumia fursa hiyo kufanya uchochezi, kumtukana Rais na Serikali, Kwimba siyo uwanja wa kupangia uchochezi,” alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Alieleza kwamba nchi yetu imejengwa kwa misingi imara ya demokrasia, amani, mshikamano na umoja wa kitaifa ambao unapaswa kulindwa kwa nguvu yote na kila mmoja, hivyo kuruhusu kundi la watu waivuruge ni kuuza amani ya watanzania.
Alisema maelfu ya sungusungu hao, wananchi, viongozi wa vyama vya siasa, Vitongoji, Vijiji, Kata na wilaya waliohudhuria kwenye mkutano huo wa kupinga siasa za uchochezi zinazoweza kuvunja amani ya nchi, ni ishara kwamba wana Kwimba wanataka amani siyo mambo ya Tunisa au Libya .
Sungusungu hao wakiongozwa na Mteni wa Tarafa ya Ibindo Shimbi Mogani, wakiimba nyimbo za kusisitiza amani kwa lugha ya kisukuma,walisema uchaguzi umekwisha wana Kwimba wanachapa kazi na kusomesha watoto kuondoa umaskini na ujinga, waachiwe amani waliyozoea.
Waliimba “Obebe Slaa nelechama lyako mle bayojase.” Yaani wewe Dk.Slaa na chama chako ni wachonganishi na kuwaasa wananchi wasiwape nafasi ya kuchochea vurugu na pia kumtaka Mtemi wao (Kangoye) achukue hatua kama serikali wilayani mwake wanapotokea wachochezi.
Awali mkutanao huo ulitanguliwa na maombi ya sala kuiombea nchi iwe na amani na kuepuka vurugu kama za Misri, Tunisia na Libta, kabla ya jeshi hilo kutoa heshina na nasaha hizo.
Waliotoa maombi hayo ni Sheikh Mkuu wa wilaya ya Kwimba Sad Seif(BAKWATA) na Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa wilayani humo, Mchungaji Samuel Makima (AICT Kwimba) ambao walisema kuwa uchaguzi ulisha isha viongozi wakapatikana hivyo wajibu wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.
wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.

Mgambo wakiimba wimbo maalum kwa kilugha wenye ujumbe wa kukomesha maandamo yanoyafanywa na Chama cha CHADEMA.



Watu wa aina hii ni kukamata chapa fimbo za kutosha na makonzi ya maana labda watapata ufahamu
 
Well done wana kwimba na DC wenu mmeonyesha njia na wengine watafuata kwa kuepuka kuwa mbuzi wa kafara kwa manufaa ya wachache wa CHADEMA walioshindwa kupata uongozi wa njia za demokrasia kupitia uchaguzi ulio huru na wa haki
 
Hapo pana ghiliba tu. Hapo kuna pesa kidogo imetembea ili kujenga jina la DC, f-stop.
 
Hivi alichakachua kura ngapi? Yaani matokeo halali kwa mujubu wa utafiti huru yalimpa kura ngapi Dr. Slaa na kisha zikachakachuliwa kwa kiasi gani kumpa ushindi wa asilimia 61 Mheshimiwa Dr. Rais Kikwete. Pamoja na kuahidi, CHADEMA hawajawahi kuja na data tofauti za hizi za tume ya uchaguzi kuthibitisha kilio chao cha kuchakachuliwa kwenye ura za urais.
Kura ziligeuzwa za DR Slaa alichukua Kikwete za Kikwete akapewa Dr Slaa,kamaa DR Slaa si jabali kitu gani mfumo mzima wa serikali na CCM wanamgwaya yeye
Nguvu kubwa kweli inawekwa kumdhibiti utafikiri tuko utawala wa makaburu na Nelson Mandela
 
Elimu kitu kimoja muhimu sana kuliko hata pesa.wasukuma ndugu zangu mkubali tu kwamba nyie bado sana.
 
Haukatazwi kufikiri hivyo. Sote tulikuwepo mwaka 2005, 2010 hadi leo. Nje ya JF, JK bado anakubalika sana tu. Kuna wanaonufaika sana na yeye kuwa Rais wa Tz.


unachokisema ni kweli kabisa, mfano hapo kwenye RED ni watu kama Rostam Aziz & co, na makuwadi wao kama wewe.
 

jo61.jpg
[/COLOR][/I][/B][/URL]
Mgambo wakiimba wimbo maalum kwa kilugha wenye ujumbe wa kukomesha maandamo yanoyafanywa na Chama cha CHADEMA.[/CENTER]

Haaa haaa haaaaa..........! Njaa mbaya sana. Yaani badala ya kuzungumzia matatizo ya ufisadi na umaskini namna ya kuviondoa vitu hivyo, wanakimbilia kuandamana dhidi ya CHADEMA? Yaani siku hizi kila mwana-CCM akiongea lazima aitaje CHADEMA, simply kwa sababu wanahofia madaraka yao kuwa hatarini! Na bado mwaka huu lazima mtaipata fresh, CHADEMA endeleeni kuwasahaulisha wasilete maendeleo ili 2015 wasiweze kuonesha maendeleo yoyote, kisha muwaondoe IKULU kirahisi!
 
Well done wana kwimba na DC wenu mmeonyesha njia na wengine watafuata kwa kuepuka kuwa mbuzi wa kafara kwa manufaa ya wachache wa CHADEMA walioshindwa kupata uongozi wa njia za demokrasia kupitia uchaguzi ulio huru na wa haki

Hivi ni kazi ya DC kufanya mambo ya siasa? Kama DC aliona kwamba CHADEMA ilikosea kufanya maandamano kwa nini hawakuwakamata? Huyu DC pamoja na Mkubwa wake wa kazi (JK) sijui kama wanaelewa kwamba wanatakiwa wafanye kazi namna gani, maana hata JK amefikia mahali eti naye ANALALAMIKA! Narudia tena, RAIS WETU ANALALAMIKA, badala ya kuchukua hatua! Jamani kama urais kazi yake ni kulalamika kwamba chama fulani kinakuonea basi kila mtu anaweza kushika nafasi ya urais!
 
Jinsi CHADEMA 'ilivyochochea vurugu' kwa mujibu wa CCM ni kauli hizi:
  1. Kwamba maisha ni magumu na serikali inabidi kufanya iwezavyo kuyaboresha
  2. Kwamba serikali isilipe DOWANS
  3. Kwamba Waziri wa ulinzi awajibike kwa uzembe wa mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto
Sasa huyu bwana DC atueleze ni vipi kauli hizi zinahatarisha amani.
 
Ndiyo faida ya kuwa na wananchi maskini na wenye elimu duni. Ni rahisi sana kuwakusanya na kuwashirikisha katika jambo lolote lile ilimradi uandae ng'ombe mmoja na Tshirts. Huo ndiyo mtaji wa sisiem. Wilaya zote ambazo literacy ya wananchi ni kubwa, siyo rahisi kuwakusanya na kuwapotezea muda wao wakiwa mabarabarani kuunga mkono jambo linaloleta hata ukakasi kulisikia. Poleni wana Kwimba kwa kutumiwa na mafisadi.

Baada ya maandamano hayo uchwara, sitashangaa kusikia mkuu wa wilaya amepandishwa cheo na kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kama comedy, inachekesha kweli hii nadhani lingeanzishwa jukwaa la Mizaha!
 
Back
Top Bottom