DC anusa ufisadi kwenye mikataba

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
MIKATABA mibovu ya ukodishwaji wa mashamba makubwa ya kahawa wilayani Hai kati ya bodi za vyama vya msingi vya ushirika na wawekezaji imeonekana kuwanufaisha zaidi wawekezaji na kuviacha vyama hivyo vikiwa taabani.

Mikataba hiyo iligunduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dkt, Norman Sigalla katika ziara ya wiki moja ya kukagua mashamba hayo na kushuhudia kasoro kubwa katika mikataba hiyo.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya wawekezaji kuingia mikataba na makampuni mengine ya kulima mazao mbadala kinyemela, na wengine kufikia hatua ya kuanzisha biashara ya utalii wa farasi na nyumba za kulala
wageni.

Mashamba ambayo kwa mujibu wa Dkt. Sigala ni pamoja na Makuru linalomilikiwa na Chama cha Msingi cha Nshara na Makoa linalomilikiwa na Chama cha Msingi cha Uduru

Kutokana na hali hiyo, Dkt. Sigala ameziagiza bodi za vyama hivyo kukutana na wawekezaji wao na kufanya marekebisho ya mikataba ambayo itanufaisha vyama hivyo na kutoa taarifa za kupitia upya mikataba hiyo kwake katika kipindi cha mwezi mmoja.

"Pande zote zikae ikiwa na maana pande za vyama na wawekezaji ili waweze kufanya marekebisho na kuwa na mikataba yenye tija kwa pande zote, na nipate taarifa hiyo ndani ya mwezi mmoja," alisema Dkt. Sigala

Aliongeza kuwa katika marekebisho hayo ya mikataba, wanasheria wa wilaya na maafisa ushirika lazima washirikishwe moja kwa moja ili kulinda maslahi ya vyama hivyo na serikali ambayo ndiyo yenye dhamana na mashamba hayo.




Majira Gazeti
 
Back
Top Bottom