DC amkwida diwani katika chakula

DC amkwida diwani katika chakula

Tunata kiongozi anayejiheshimu na kujithamini katka safu ya uongozi wa nchi hii. Kiongozi unapovunjiwa heshima inabidi uonyeshe kujithamini kwako kuchukua hatua kwa yule aliyekuvunjia heshima na wananchi unaowaongoza waone kweli umejithamini kwa kuchukua hatua.

Kuna namna nyingi za kuonyesha kujithamini mara unapovunjiwa heshima. Nasikitika kusema kuwa Diwani Sipemba hakujithamini kwa kitendo chake cha kutochukua hatua baada ya kudalilishwa, kwa kifupi , diwani kakubali kudhalilishwa pamoja na wale waliomchagua.
 
hivi chakula huko Kahama ni adimu sana ??

Nashauri hii tabia ya kupanga foleni ife hasa kwa upande wa kupata chakula na Mpesya tafadhari sana usituaibishe watu wa Mbeya hasira za kubwagwa na Sugu usizihamishie Kahama
...Haaaa haaaa haaaaaa ukizingatia ulikuwa ubwabwa mh!!! roho zinakimbia bhana!
 
Diwani alivunja utaratibu. Kuna itifaki alikuwa akiifanya mkuu wa wilaya hivyo diwani angesubiri wakati wake ufike. Inakuwa kama waligombea chakula!

Ni kweli ila itifaki ikivunjwa busara inatakiwa itumike hasa mtu mzima anapokuwa katika mstari inabidi umpotezee alafu unampa elimu, hata hivyo diwani yule nae amekomaa kisiasa hajasusa msosi akaugonga bila zengwe pale DC alipomtoa mikononi mwa police
 
Benson Mpesya akapimwe akili,akumbuke kuwa kuna siku atakwenda kufanya kazi kata ya diwani aliyemdhalilisha,na yeye kama dc hana watu diwani ana watu,akumbuke yaliyotaka kumpata Makamu wa Raisi tunduma hadi akaokolewa na Ernest Silinde David.
 
...Haaaa haaaa haaaaaa ukizingatia ulikuwa ubwabwa mh!!! roho zinakimbia bhana!

Huko ndipo unalimwa kama msimu ni mzuri kilo moja huwa inashuka mpaka Tsh.500 (mia tano), hapa nadhani kuna dhana kama ile ya utotoni chakula cha nje ya nyumbani ni kitamu maana mtoto kimepikwa kile kile nyumbani kula ni issue lakini akienda kwa ajirani anakula mpaka basi
 
kwikwiwiwwwwwwwwwwwwwwwwwww hii haikuwa nzuri hata kidogo.anyway kama hakufwata itifaki asingetumia nguvu zote hizo na kumdhalilisha namna hiyo angemsema baadae chakula ni kitu kidogo sana. au kilikuwa hakitoshi?

halafu DC anakagua mstari wa chakula kujua nani kala nani yupo nani hayupo??????? hii ni aibu hana wasaidizi hana kazi zingine.?

na wewe diwani hata kama njaa yako imezidi imezalilishwa bado wala?
je angekuwa wa ccm angemfanya hivi? hapa mwisho nauliza tu.
 
Shija Felician, Kahama
MKUU wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, juzi alimkwida na kumuondoa katika mstari wa viongozi kwenda kupata chakula, Diwani wa Kata ya Nyihogo (Chadema), Amos Sipemba.

Chakula hicho kilikuwa maalum kwa msafara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Katika tukio hilo lililotokea wakati wa chakula cha mchana katika viwanja vya nyumba ya mapumziko alipokuwa amefikia waziri mkuu, Mpesya alianza kuwakaribisha wageni wa kimkoa kutangulia kupata chakula, huku akiwataka baadhi ya viongozi wa wawakilishi wa wananchi ,kuungana na msafara huo.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye alionekana kuwa makini zaidi na ugeni huo, akiwa mara yake ya kwanza kupokea ugeni wa kitaifa tangu aipoteuliwa miezi minne iliyopita, alisimamia ugawaji wa chakula kwa wageni na wenyeji waliokuwa katika msafara huo.

Baada ya kumaliza kutangaza wageni wa kimkoa, aliwachagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Machibya Jidulamabambasi na makamu wake, Lucas Makulumo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya wa Kahama, Alfred Mahanganya na makamu wake Mibako Mabubu.

Hali kadhalika Diwani wa Kahama Mjini ili waungane na msafara huo katika upata chakula.


Diwani Sipemba akiwa na mwenzake wa Kata ya Mwendakulima (TLP), Ntabo Majabi nao walijipachika kwenye mstari wakiwa nyuma ya Diwani wa Kata ya Kahama Mjini, Abasi Omari, ambaye Mpesya alimtaka ajumuike na ugeni kutoka mkoani.

Lakini alipoona Sipemba yuko mstarini, mkuu huyo wa wilaya alikwenda na kumtaka asiingie kwenye mstari lakini diwani huyo alikaidi amri.

Kitendo hicho kilimfanya Mpesya ampige jeki kwa nyuma kwa kutumia mkanda wa suruali aliyokuwa amevaa (diwani) na kumnyanyua mithili ya mhalifu.

Hatua hiyo ilimwezesha kiongozi huyo kufanikiwa kumuondoa diwani huyo kwenye mstari wa wageni na kumrejesha nyuma ambako alidakwa na askari polisi waliokuwa wakilinda usalama katika eneo hilo.

Hata hivyo baadhiya madiwani walilalamikia kitendo hicho walichokielezea kuwa ni cha udhalilishwa kwa mwenzao hasa baada ya kubaini kuwa diwani mwenzie wa TLP aliyeingia naye kwenye mstari, aliachwa mstarini.

Baada ya malalamiko hayo, mkuu wa wilaya alikwenda tena kwenye mstari wa wageni wa kimkoa na kumtaka diwani aliyekuwa amebaki kwenye mstari, atoke na alifanya hivyo.

Alisikika akisema mara nyingi madiwani wamekuwa wakivuruga itifaki katika misafara ya wageni wa kitaifa na kwamba sasa lazima waheshimu na kufuata taratibu.

Hata hivyo wakati ugawaji chakula ukiendelea mkuu huyo, alimfuata diwani huyo na kumnasua kutoka kwenye mikono ya polisi waliokuwa wamemshikilia.

Alimpeleka ndani ya ukumbi na kumuinganisha na wageni katika kupata chakula, jambo ambalo watu walilitafsiri kuwa ni kujisafisha baada ya kumdhalilisha diwani.

haya maandishi yako hayana mvuto kusoma, japo habari yenyewe ni nzuri huku janvini
 
haya maandishi yako hayana mvuto kusoma, japo habari yenyewe ni nzuri huku janvini

1.hujalazimishwa kusoma

2.unaweza kuweka mvuto kwa kufanyia editing kadri upendavyo wewe

3. hoja yako ni ya kipuuzi.
 
Jamani kateuliwa kuwa mkuu wa wilaya?aaaaarrrgh hii nchi vip?
 
Back
Top Bottom