DC amfukuza kazi Mganga wa zamu kwa uzembe kazini baada ya kukataa kumtibu Mtoto wa miezi 6

Hakuna daktari hapo huyo ni clinical officer,wa kufukuzwa haraka sana

kabombe upeo wako ni mdogo sana. Linapokuja suala la kazi katika hospitali hizo tofauti za kada kwa madaktari huwezi kuliona, infact mgonjwa anajua wote ni madaktari.
Haijarishi ni Co, AMO, MD, MMED lakini wote wana haki na wajibu sawa katika kumhudumia mgonjwa.
 
Last edited by a moderator:
DC hana uwezo wa kumfukuza Kazi Daktari sio mamlaka yake ya nidhamu Na mtumishi wa umma hafukizwi kazi kwa style hiyo kuna taratibu labda Kama angekuwa houseboy wake
 
Kama ni kweli amemfukuza kazi huyo tabibu basi amepitiwa na hasira tu kwani huyo DC ni mtu asiyependa kuona wananchi wananyanyaswa,nakumbuka wakati wa operesheni tokomeza alivyokuwa upande wa wananchi waliokuwa wanaonewa kawa kuwaambia waripoti uonevu naye atadili na askari au mtu yeyote anaewanyanyasa raia!
 
Wangempa nafasi hy Tabibu kujitetea maana ninavyojua kama mtu mwenye fani hy akiwa amechoka basi kutibu kwake kuna mashaka na kunaweza leta athari kwa mgonjwa, pia sijui.ni sheria ipi inampa mamlaka mkuu wa wilaya kumfukuza kazi mtumishi wa serikali. Maana hy tabibu ni mwajiriwa wa mkurugenzi

ndg ww unatetea uozo, udaktari ni wito bora kama hawez asepe kuliko kuacha watu wanapoteza maisha kwa uzembe
 
Maadili!! Maadili!! Hii kada ya C/O kwenye tiba ni shida. Hawana maadili,ni ngumu sana kushtakiwa kwani hicho cheo haitambuliki W.H.O. Hawa jamaa hawana kiapo cha kazi yao,wanapitwa na wauguzi ambao huapa,na kuahidi kuishi kiapo chao. Wengi wao wamesaidia Sana kutibu vijijini(miaka ya 90 kurudi nyuma),ila hawa wa BRN ni shida tupu. Huyo aliyekataa kumtibu mgonjwa huenda alikuwa tungi.
wewe acha kuandika usichokijua..una uhakija gani huyo mganga wa zamu alikuwa ni co na sio ca?..acha chuki binafsi.kuna wakati wagonjwa huwa wanakera..kwa mfano unaweza kuta mama alimleta mgonjwa asubuh sana wakati ugonjwa sio wa dharura..muda huo maabara vipimo vinavyofanyika huwa ni vya dharura tu.. sina lengo la kumtetea huyo mganga ila usiwe na tabia ya kujaji mtu bila kuelewa mazingira sahih ya tukio.
 
nyie watz,dc hana mamlaka ya kumfukuza mtumishi,someni kanuni na taratibu za utumishi wa umma
 
Wanapoomba kazi mikono nyuma wakipata tu kosa kiburi na kufanya wanavyotaka wao hayo matatizo yapo sehemu nyingi sana katika hospitari za serikali mbona hospitari za watu binafsi hayo hayapo?
 
Mkuu hiyo Idadi ya 700 ina walakini pia kumbuka population ya watz inaongezeka na haipungui

www.wavuti.com/2014/05/hotuba-ya-rais-kikwete-katika.html?m=1

Soma hiyo hotuba hapo, au pitia/ulizia takwimu kwa msajili wa madaktari pale wizarani, Mkuu.
 
mkuu unazungumzia mtaa gani huo wenye ma MD?? au umeamua tu kufurahisha Jukwaa???



Yaani daktari MD wamejaa mitaani, you can't be serious

umeniwahi mkuu...... hakuna MD anayekaa tu mtaani kakosa kazi...
 
mkuu unazungumzia mtaa gani huo wenye ma MD?? au umeamua tu kufurahisha Jukwaa???
Yaani daktari MD wamejaa mitaani, you can't be serious


Mkuu ninaongelea huyo huyo MD unayemfahamu,(yaani aliyesoma na kumaliza miaka mitano).
Mfano juzi juzi hapa MNH ilihitaji watu watano, na ikaamua kuongeza idadi hadi wanane. Number ya walioomba nafasi ni 156!
Okay unaweza kusema hii ni MNH na "wengi" wanataka kubaki hapa mjini lakini je jiulize;

Ni wangapi wako mtaani leo hii bila ajira(mfano hawa vijana waliomaliza internship kuanzia mwezi wa tisa!Wako wapi?
Kwa kiwango chake cha elimu(MD) anapaswa kufanya kazi kuanzia hospitali ya wilaya kwenda juu). Ni hospitali ngapi hata hao MDs hawapo? Yes, kuna private sector na pengine wako huko, lakini ji hospitali ngapi za Private(zenye uwezo wa kumlipa MD) tena mikoani?

Miaka ya nyuma Output ilikuwa ndogo, by 2012 mwishoni Tanzania ilikuwa na jumla ya madaktari 1800TU, yaani wenye shahada ya kwanza na kuendelea(MDs, Specialists). Hii ilikuwa kabla ya watu kuondoka kwenda Rwanda, Botswana n.k baada ya migomo ya madaktari.

Kuanzia mwaka 2013 idadi ya madaktari(MD) wanaomaliza ilikuwa 700 kwa mwaka. Idadi hii haija include wale wahitimu wa kwanza wa Ifakara(Morogoro) wa mwaka huu, vile vile mwaka huu UDSM na St. Joseph University/College wameanzisha vyuo vya afya.

Private hospital nyingi hawawezi kuwaajiri MDs (wengi ni C. O na AMO, MDs ni wachache chunguza hili pia) hawawezi kuwalipa(atleast to maintain.) na hiyo ndiyo sababu wengi wako mtaani wakisubiri ajira ya serikali!



MD aliyekuwa mtaani ni mzembe!!!! au anataka abaki DAR!!

nawajua watu walimaliza intern 2014 wengine walipata ajira sehemu zaidi ya tatu mikoani wanachagua wapi kwenye mshahara wa kutosha ...

ukiachana na kukaa wodini MD kuna shughuli nyingi tu za kufanya options kibao..

narudia tena MD walio mtaani ni wazembe..
 
naongea from experience.. sijui taratibu za halmashauri.. but mama yangu mzazi alilazwa apollo india 2012.. nilienda kumwona.. kuna siku usiku kama saa 8 aliumwa sana kichwa... daktari aliyekuwepo akampigia simu mtu aliyemfanyia surgery specialist.. akaamka usiku na kuendesha gari yake 1 and a half hour mpaka hospital maana miji ya watu ni mikubwa watu wanaishi mbali mbali.. na ct scan na mri ikawashwa usiku huo kujua nini shida.. na yule.specialist alishinda nae mapaka kesho yake.. na alikuja na pajama..

na aliondoka baada ya kuhakikisha mgonjwa amepata huduma sahihi...

ingekuwa bongo nina uhakika tungeambiwa tusubiri asubuhi
 
Back
Top Bottom