DC aagiza kiongozi wa 4U Movement kuswekwa ndani.

DC aagiza kiongozi wa 4U Movement kuswekwa ndani.

chaikavu

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2015
Posts
760
Reaction score
473
[h=2]DC aagiza kiongozi wa 4U Movement kuswekwa ndani.[/h]


NA ANCETH NYAHORE



5th September 2015


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa










Rose-5Aug2015.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Rosemary Kirigini.


Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Rosemary Kirigini, amedaiwa kuagiza kukamatwa na kuwekwa mahabusu kiongozi wa kikundi cha 4U Movement katika Wilaya ya Maswa, Madeleke Masanja, kwa madai ya kuanzisha mtandao hatari kwa usalama wa nchi. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupewa dhamana katika kituo cha polisi Wilaya ya Maswa, Madeleke alisema kitendo hicho kilichofanywa na Mkuu wa wilaya ni kinyume na demokrasia nchini.

Alisema Agosti 27, mwaka huu, akiwa katika eneo lake la kazi majira ya saa 7:30 mchana Shule ya Msingi Binza, alifika Afisa Usalama wa Wilaya ya Maswa anayemfahamu kwa jina moja la Peter na kumweleza kuwa anamhitaji akamtengenezee mlango ofisini kwake na kuondoka naye kwenye gari.

Alisema walipofika ndani ya ofisi aliwekwa chini ya ulinzi kwa madai kuwa anajihusisha na mtandao huo ambao ni hatari nchini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kwani kinahusishwa na masuala ya ugaidi.

Tulipofika ndani ya ofisi yake aliniweka chini ya ulinzi na kisha kumpigia simu Mkuu wa polisi wa wilaya ya Maswa SSP Kanyorota ambaye alifika muda si mrefu na kuanza kunihoji nami niliwaeleza wazi kuwa malengo ya 4u movement si kama wanavyodai bali ni vuguvugu la mabadiliko ndani ya nchi kupitia balozi wa mabadiliko Edward Lowassa tangu akiwa ndani ya CCM na sasa nje ya CCM na si dhambi ni haki yetu ya kikatiba,’ alisema.

Alisema mara baada ya mahojiano yaliyochukua saa nne alipelekwa mahabusu katika kituo cha polisi bila ndugu na jamaa zake kufahamu.




CHANZO: NIPASHE
DUUUU! NDIO TUMEFIKA HUKO?



 
Kwenye Safari ya Kutafuta Ukombozi wa Kweli Vikwazo,Maonevu,dhuruma na dhihaka Ni sehemu ya Mafanikio. Ukiona Dalili Hizi Basi Ujue

Kunakaribia Kucha Na Asubuhi Njema Ipo Karibu. Hii Vita ya Mabadiriko Imeshakolea na Hakuna Namna yoyote Watawala Wataizuia.

Tujue ya Kwamba Katika Aguko la CCM,Wanufaika Ni Wengi Ambao Hadi Sasa Hawataki Kuamini Kabisa Kama Chimbo lao (Kitumbua

Chao) Kinaenda Kuingia Mchanga Soon.
 
Hata Libya walifanya hivyo lakini mwisho wake u ajulikana
wananchi wakishataka mabadiriko lazima tu yatokee
 
Aisee ccm na policcm wamefikia hapo kweli democrasia imekanyagwa
 
Back
Top Bottom