Daz Baba amgundua mchawi wake

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,386
Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop,
Daz Baba amedai amegundua kitu
ambacho kinamkwamisha ashindwe
kufanya vizuri kama zamani
Daz-Baba11.jpg

Daz ambaye amewahi kufanya vizuri na
nyimbo nyingi ikiwemo ‘Namba 8’,
ameimbia Bongo5 kuwa uwekezaji
katika kazi zake za muziki ndio kitu
ambacho kinamfelisha.
“Mimi kitu ambacho kinanikwamisha
kwa sasa ni video kali. Kwa sababu
nyimbo zangu ni kali sana na sijawahi
kufanya kazi mbaya katika maisha
yangu,” alisema Daz. “Kama ningepata
management kali ya kusimamia muziki
wangu na kuwekeza ningerudi vizuri
kwenye game,”
Aliongeza, “Siwezi kukata tamaa na
bado napambana najua bado nafasi ya
kufanya vizuri ninayo kwa sababu kila
kitu ninacho katika muziki wangu,”
Daz amedai kwa sasa anatafuta
management ambayo itasimamia muziki
wake.
Rapa huyo ni mmoja kati ya wasanii wa
Kundi la Daz Nunda ambao walifanya
vizuri katika kipindi cha nyuma.
Source: Bingo5
 
Mhh, muziki anaoimba hauna mashiko, hatuupendi, aimbe kama zamani, pia kwa msanii appearance nzuri ni muhimu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom