Kwanza ungesema nn kaz yake na nn faida yake..... Hapo ndo tuje na jibu la.... Naomba kuipata....
Cyanogenmod ni Custom OS kwa ajili ya baadhi ya Android devices, Cyanogenmod inakupa experience ya stock Android kama ile inayopatikana kwenye simu na tablet za Nexus..
Pia Cyanogenmod inakuwezesha wewe mtumiaji kupata root access by default, wakati pia inakupa uwezo wa kuchagua performance rate ya simu yako kutokana na mahitaji yako ya nguvu ya processor.
Kwa sababu Cyanogenmod inatengenezwa na kampuni huru ya Cyanogen Inc, OS hii inakuja bila Google Applications hivyo kukupa uhuru wa kuchagua kama unahitaji huduma za Google au la...
Cyanogenmod kwa sasa imekuwa kwa kasi sana, watengenezaji wa simu kama Oppo, Micromax, na OnePlus wametoa simu zao zikiwa na Cyanogenmod OS..
Kampuni ya Cyanogenmod ipo chini ya watu wawili muhimu sana Steve Kondik na Kirt Macmaster ambao wamenuia kuichukua Android kutoka kwenye utawala wa Google..
Hivyo basi kwa wewe mtumiaji wa simu za Android unatakiwa kujua jambo hili muhimu. SIO KILA SIMU YENYE UWEZO WA KUPATA CYANOGENMOD.., mara nyingi OS hii inakuja kwa simu ambazo ni high end(powerful) kama Samsung Galaxy S hadi S6, HTC ONE zote, Google Nexus zote, Motorola na nyinginezo, simu zenye Mediatek Chipest kama Tecno, baadhi ya Huawei huwa zinaachwa mbali kidogo..