Dawasco

The Retired Planner

Senior Member
Sep 22, 2015
189
250
Naomba kujuzwa hizi bill za Dawasco zinakwenda kwenda vipi wajameni. Bill ya mwezi September na October ilikuja kama TZS 720,000 hivi wakati hii ya mwezi November na December mpaka kufikia tarehe 20 Dec imekuja kama TZS 160,000 hivi.

Ukiachilia mbali huo utofauti mkubwa ninaouona baina ya hiyo miezi tofauti tofauti, najiuliza hivi kweli kwa matumizi gani ya nyumbani kwa wapangaji watatu wenye familia za watu wasiozidi wanne kuwa na gharama kubwa kiasi hicho.

Naomba kusaidiwa yafuatayo:

1. Mwenye kujua gharama halisi ya unit moja ya maji - kutoka katika meter za Dawasco
2. Namba ya mtu wa Dawasco (Kinondoni) - Hapa ntaomba uni PM

Asanteni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom