Je, DAWASCO imeongeza gharama za maji mwezi Agosti kimyakimya?

mapenzi hasara

Senior Member
Feb 28, 2020
102
275
Wakuu,

Bills za maji zimetoka mwezi wa August na nimeziona kama bills tatu tofauti zote zinashangaza. Nimeiona bill ya ofisini hii inapitia kwangu
Nimeona bill ya mshua wangu na Leo nimepewa bill ya ninapoishi

Bill ya ofisini imekuja mara tatu ya pesa tunayolipa
Bill ya Kwa mshua imekuja mara mbili
Na ya kwangu mara mbili

Kwa wajuvi wa haya mambo, je DAWASCO wameongeza gharama za maji kimya kimya? Au kwako bill uko sawa?
 
kwan mara ya mwisho uliletewa bili lini?
Inaonesha Dawasa hawajatuma bili kama miezi miwili,kwa hiyo inawezekana bili ni kubwa kwa kuwa hakuleta ya mwezi jana
 
Mimi pia niliwahoji kuhusu ili jambo maana bili ilikuja kubwa,wakasema mwanzo walikuwa wanatoa ofa ya kuanzia unit 1-5 wanakuchaji Tsh 1,100 ila kuanzia unit 6 na kuendelea wanakuchaji 1660 kwa unit,kwa hyo kwa mfano umetumia unit 10 kwa mwezi
1-5 *1,100= 5,500
5 * 1,660= 8,300
Total unit 10=. 13,800.

Kwa hyo hiyo ofa ya unit 5 za mwanzo kwa tsh 1,100 wameiondoa sasa hivi wanachaji kuanzia unit moja na kuendelea kwa tsh 1,660.sasa hivi kama umetumia unit 10 kwa mwezi.
Unit 10 *1660= 16,600.
 
kwan mara ya mwisho uliletewa bili lini?
Inaonesha Dawasa hawajatuma bili kama miezi miwili,kwa hiyo inawezekana bili ni kubwa kwa kuwa hakuleta ya mwezi jana
Hapana mara ya mwisho tumelipa around 162,000 bill mpya 536000
 
Mimi pia niliwahoji kuhusu ili jambo maana bili ilikuja kubwa,wakasema mwanzo walikuwa wanatoa ofa ya kuanzia unit 1-5 wanakuchaji Tsh 1,100 ila kuanzia unit 6 na kuendelea wanakuchaji 1660 kwa unit,kwa hyo kwa mfano umetumia unit 10 kwa mwezi
1-5 *1,100= 5,500
5 * 1,660= 8,300
Total unit 10=. 13,800.

Kwa hyo hiyo ofa ya unit 5 za mwanzo kwa tsh 1,100 wameiondoa sasa hivi wanachaji kuanzia unit moja na kuendelea kwa tsh 1,660.sasa hivi kama umetumia unit 10 kwa mwezi.
Unit 10 *1660= 16,600.
Maelezo mazuri mkuu.
 
Maelezo mazuri mkuu.
Lakin pia mkuu mimi naona ni kama wizi kwa wateja,hili ni shirika la ambalo linapewa ruzuku zinazotokana na kodi zetu,kwa hyo haya maji ni naona hatukutakiwa kununua zaidi ya sh 1000 kwa unit 1
 
Back
Top Bottom