Picha ni Mwananchi Kimara Bonyokwa akiwa wameanza kupata huduma ya Majisafi kwa mkopo toka DAWASCO.
Huduma ya maji kwa mkopo ni kampeni iliyoanzishwa na Dawasco kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya Majisafi bila kujali kipato chao
Watu wote wenye uwezo mdogo wa kuunganisha maji, tembeleeni Ofisi za DAWASCO ili waweze kusaini mkataba wa maunganisho mapya ya maji kwa gharama nafuu na kulipa kidogo kidogo.
Kuna kampeni inafanywa na DAWASCO ya ''Mama Tua Ndoo' ndani ya siku 90. Malengo ni watu 151,000 wauunganishiwe maji hata kwa mkopo wa miezi 12.
Mteja wa DAWASCO, atafungiwa huduma ya Maji safi kwa mkopo ambapo atatakiwa kulipa gharama hizo kidogo kidogo mara baada ya kuanza kupata Maji. Hivyo wananchi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi kupata maji.
Kwa Mawasiliano, Ushauri na Maswali na mapendekezo, Usisite kuwapigia DAWASCO kupitia namba: 0800110064.
Namba hii ni bure.