Dawasco na operesheni sitisha maji taka

habayu

Member
Feb 22, 2011
17
7
Katika siku za maisha yetu kama watanzania nimekutana na operasheni nyingi za mashirika ya umma yakiwa na lengo la kuhakikisha yanapata makusanyo ya kutosha ingizigatiwa mengi yao sasa yako taabani kipesa.

Katika kudai haki yao hiyo muhimu kwa ustawi wa mashirika na taasisi zao vilevile inapaswa tuwakumbushe wajibu walionao wa kuhakikisha umlaji nae anatimiziwa haki zake,kulindwa, na kuheshimiwa.
Hivi karibuni nimekutana na kali ya mwaka ambapo Dawasco wamekuwa hakipita nyumba hadi nyumba katika mitaa ya Mwenge jijini Dar es salaam ili kusitisha huduma ya majitaka kwa wateja.

Uzoefu unaonyesha kuwa awali tozo hili la maji taka lilikuwa likitozwa sanjali na tozo la huduma ya maji safi.Lakini inaeleweka wazi kuwa huduma ya maji safi sasa imekuwa kitendawili japo hakipigiwi kelele kama kile cha umeme wa Tanesco hivyo pengine ndio sababu ya “kuanzishwa” huu mgawanyo wa tozo (i.e. maji taka na maji safi)

Hii naiita kali ya mwaka kwa sababu zifuatazo:

  1. Kwanza kama itakuwa ni kweli sasa tozo za maji taka na maji safi ni tofauti na zinalipiwa katika akaunti tofauti ilibidi watumiaji waarifiwe na wapewe muda wa kujipanga.
  2. Pili ni kuwa usitiswaji wa huduma umekuwa ukifanywa kwa kuziba “main chamber” kwa mawe na saruji kitu ambacho hakihitaji shahada ya uhandisi kujua kuwa ni kinyume cha taaluma.
  3. Tatu “main chamber” huwa zinahudumia nyumba zaidi ya moja hivyo kuzibisha hizi chamber mara nyingi inapelekea kuadhiri waliomo na wasiowemo.
  4. Nne gharama inayosababishwa na usumbufu huu ni kubwa kifedha na pili kuwaweka wakazi katika hatari ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Ni historia miundo mbinu ya maji taka maeneo ya Mwenge ilijegwa mwaka 1974 (wakati huo kikiitwa kijiji cha Ujamaa Mwenge) Mwenge ikiwa moja ya maeneo yaliyo na bahati ya kupata miundo mbinu ya maji taka jijini ambayo inasafirisha maji hayo kuelelea mabwawa ya maji taka kabla ya kuingia katika bahari ya Hindi.

  • Lakini yote ya yote ni kuwa hakuna haki isiyo na wajibu,sasa iweje Dawasco watake tozo katika miundo mbinu ambayo hakuisisi na waisiyoikarabati?
  • Hivi ni kweli wataalamu wa kampuni hii wamekosa njia ya kiungwana ya kudai hizi tozo na badala yake kuamua kuzibisha hizi “chemder”?
 
Back
Top Bottom