DAWASA yafika Mikocheni kutatua changamoto ya Majitaka

DAWASA yafika Mikocheni kutatua changamoto ya Majitaka

DAWASA

Official Account
Joined
Oct 7, 2010
Posts
201
Reaction score
121
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) imetatua changamoto ya utiririshaji majitaka iliyotokea katika mtaa wa TPDC Mikocheni na kutoa elimu juu ya utunzaji na matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka kwa Wakazi wa eneo hilo ambao wameunganishwa na mfumo wa Majitaka wa Mamlaka.
WhatsApp Image 2026-08-20 at 13.05.54 (2).jpeg

Meneja usimamizi wa Miundombinu ya Majitaka DAWASA, Mhandisi Jolyce Mwanjee ameeleza kuwa timu ya wataalamu ilifika na kufanya uchunguzi wa kitaalamu kubaini tatizo kisha kulitatua.

"Baada ya kupokea changamoto hii tumefika eneo la tukio na kubaini chanzo cha utirirshaji majitaka katika eneo hili ni maunganisho yasiyo halali katika mtandao wa majitaka yaliyopelekea kuziba kwa chemba baada ya uchafu kujaa na kutiririsha maji mtaani" alisema

Mwanjee ameongeza kuwa sambamba na kazi hiyo pia walitoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka na kuwaasa wananchi wote wanaohitajii huduma ya majitaka kufuata utaratibu sahihi na kuunganishwa majitaka kwa kufuata miongozo ya DAWASA.
WhatsApp Image 2026-08-20 at 13.05.55 (1).jpeg

Mwenyekiti wa mtaa wa TPDC Mikocheni ndugu Idrissa Ramadhan Hashim ameishukuru DAWASA kwa kufika kwa wakati mara baada ya kuripoti changamoto hiyo na sasa imetatuliwa na kuacha mazingira safi na salama mtaani hapo.

"Changamoto tuliyoibaini ni mmoja wa wananchi kuunganisha majitaka ya nyumbani kwake katika mfumo wa DAWASA isivyo halali na kupelekea changamoto ya kuziba kwa mfumo, niwaombe sana wananchi tunapohitaji huduma hii tuweze kufika DAWASA na kufata utaratibu ulio sahihi" ameeleza ndugu Hashim.
WhatsApp Image 2026-08-20 at 13.05.54 (1).jpeg

DAWASA inawasisitiza wananchi na wateja wote kutoa taarifa ya mapema wanapopata changamoto ya majitaka lakini pia kuepuka utupaji wa taka ngumu katika mifumo ya ili kuiruhusu kufanya kazi kwa ufanisi wakati wote.​
 
Back
Top Bottom