KERO DAWASA wanatoa maji usiku pekee

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
919
Reaction score
2,516
Ebana kipindi cha hivi karibuni nimejikuta nimemaliza mwezi mzima bila kuona kina mama wengi wa mtaa wa pili wakipita wamebeba maji, nikahisi labda wamejiunga na DAWASA.

Ebana kumbe sio, ni kwamba dawasa sasa hivi wanatoa maji usiku wa manane , sijajua kama ni maeneo yote au laa na by saa 12 asubuhi wanakata.

Ndio nikakumbuka kumbe ndio maana kila kila niki flash maji yanatoka mara moja yanaisha.

Sasa najiuliza DAWASA wanamtolea maji nani usiku huo ili hali wanajua uhalisia wa maisha ya watanzania, wengi wanategemea wakateke maji kwa jirani.

Usiku huo wanateka maji vipi?
Hebu DAWASA njooni hapa mseme mnapotoa maji usiku wa manane huwa mnamlenga nani?
 
Na bili za maji bado zitasoma figure nne (XX,xxx) ama tanoo (XXX,xxx)
 
Ni full majanga, nilifukiri ni huku tu kumbe ni balaa
 
Miaka 60 ya Uhuru CCM wakisimama jukwaani bado wanahubiria maji, barabara, madawati.
 
Sijajuaga tatizo ni nini eti mpaka miaka hiyo Daslam kuna shida ya maji, mito yote tuliyonayo bado kuna shida ya maji? Hao Dawasa wafumuliwe tu wanacheza tu hawako serious
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…