Dawa za kulevya zatikisa Shirika la Posta nchini

Dawa za kulevya zatikisa Shirika la Posta nchini

Mkurugenzi wa udhibiti madawa ya kulevya Afande Siang'a amejibu kuwa issue hii imejawa na utata mwingi ikijumuishwa na mgongano wa madaraka.
Posta masta jenero aagize bangi gram 100!
Postamasta aagize heroin gram 1.0 .Bangi ya Moro ni Kali sanaa?

Yote tisa kumi ni vipi mchele ukapimwa kule Moro na ukakutwa na uzito wa 25 kg lakini pale Dar ukapungua mpaka 20 kg ? kwa kila mifuko?
 
Hivi haya madawa wanayoa wapi wakati hii vita tuliwaita watumiaji na kuwahoji vituoni?
 
Biashara ya madawa ya kulevya inasemekana kulitikisa shirika la Posta ambapo Meneja wa usalama aliyeripotiwa kutoweka nyumbani na ofisini anadaiwa kumuwekea boss wake yaani Posta master heroin na bangi. Mtumishi huyo sasa anatafutwa kwa udi na uvumba.
Source gazeti Mtanzania!

=====

MKUU wa Kitengo cha Usalama wa Shirika la Posta nchini, George Mwamgabe ambaye hivi karibuni mwajiri wake alitangaza kwenye magazeti kuwa anatafutwa, amedaiwa kumtegea dawa za kulevya Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe.

Taarifa ya Posta iliyotolewa kwenye magazeti ilisema; “kutokana na kutoonekana kazini na nyumbani kwako, baada ya jitihada za kukutafuta kushindikana kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja, tunakufahamisha popote ulipo uhudhurie kikao cha nidhamu kitakachofanyika Jumanne Novemba mosi saa nne asubuhi kwenye ukumbi wa mkutano ghorofa ya 12 Posta makao makuu kujibu tuhuma za kinidhamu zinazokukabili.

“Aidha shirika litaendelea na kikao hicho cha nidhamu kama utashindwa kuhudhuria bila taarifa kwa mwajiri wako.”

Wakati taarifa hiyo ikiendelea kusambaa, chanzo cha kuaminika ndani ya Shirika la Posta kiliileza MTANZANIA kuwa Mwamgabe alitoweka baada ya kudaiwa kumtegeshea Mwang’ombe dawa za kulevya ambazo ni heroin gram 1.5 na bangi gramu 100.

Taarifa hizo zilidai kuwa sakata hilo lilitokana na kifurushi kilichotumwa kutoka Morogoro kwenda kwa Mwang’ombe ambaye ni Postamasta Mkuu.

Chanzo hicho kilieleza kuwa dereva aliyekuja na mzigo huo, baada ya kufika kwenye ofisi za Posta alishusha mizigo mingine, lakini alikawia kushusha kifurushi hicho.

“Alipoulizwa sababu za kutokishusha, alidai mtu aliyeelekezwa amkabidhi hamuoni eneo hilo.

“Mizigo hiyo ilifika hapa asubuhi ikitokea Morogoro, kwanza ilianza kucheleweshwa kushushwa kwenye gari, baadaye ilishushwa na kupitishwa kwenye mashine ya ukaguzi na kupelekwa stoo.

“Baadaye majira ya mchana mkuu wa kitengo cha usalama alikuja na kuingia stoo, kisha alipotoka akaagiza mizigo hiyo ikaguliwe upya,” kilisema chanzo hicho.

Kilieleza kuwa mkuu huyo wa ulinzi alisema amepigiwa simu na wasaidizi wake wawili kuwa wana mashaka na mizigo hiyo, hivyo na yeye alimpigia simu mkaguzi wa mizigo ambaye alikuwa msikitini na kumtaka arejee ofisini na kufanya upya ukaguzi.

Baada ya mkaguzi huyo kurejea, ilielezwa kuwa alikuta mizigo hiyo imefungwa tofauti na ilivyokuwa awali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chanzo hicho, mkuu huyo wa usalama alisimamia ukaguzi wa mara ya pili na kusema kuwa wamebaini kulikuwa na dawa za kulevya.

Taarifa hizo zilisema kuwa Mwamgabe aliwaita polisi na walichukua mizigo hiyo kisha kuipeleka katika kikosi cha utambuzi cha mbwa ambako walithibitisha kulikuwa na dawa hizo za kulevya na baada ya siku tatu ilirejeshwa Posta, kisha kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Kuzuia na Kudhibiti Dawa za Kulevya.

Chanzo hicho kilieleza kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 25 na polisi walichukua mizigo hiyo na waliirudisha Septemba 28 na jukumu hilo kukabidhiwa kwa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya.

MKANGANYINGIKO

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, upimaji mizigo kwa mara ya pili uliibua mkanganyiko kwa kuwa awali ilivyopimwa kulikuwa na mifuko miwili yenye mchele kilo 25 kila mmoja.

“Mara ya pili baada ya kupimwa kutokana na agizo la mkuu wa usalama, kila mfuko ulikuwa na kilo 20 jambo lililozua utata zaidi,” kilisma chanzo chetu.

Pia inadaiwa kabla ya kuamuru mizigo hiyo kukaguliwa mara ya pili, kamera za usalama za chumba cha kuhifadhia mizigo zilichezewa, kwamba kamera moja ilibadilishwa uelekeo na nyingine ilifutwa baadhi ya matukio.

Inadaiwa mtu aliyekuwa ameingia katika chumba hicho ni Mwamgabe na baada ya kutoka ndipo akaagiza mizigo hiyo ipimwe upya.

Chanzo kingine kilieleza gazeti hili kuwa katika kufuatiliwa ukweli wa suala hilo, mtu wa Posta kutoka Morogoro ambako mzigo ulitumiwa alihojiwa na vyombo vya dola na kuthibitisha kuwa mzigo alioutuma Dar es Salaam ulikuwa ni mifuko miwili yenye kilo 25 za mchele kila mmoja na siyo kilo 20.

Pia inadaiwa kuwa vijana wawili waliohusika kupima mizigo hiyo walipohojiwa walisema siyo kweli kwamba walikuwa wamemweleza mkuu wa usalama kwamba wana wasiwasi na mizigo hiyo kama ambavyo bosi wake huyo alikuwa amedai awali.

Chanzo kilieleza pia kuwa Postamasta Mkuu ilibidi afanyiwe vipimo mbalimbali ili kuthibitisha kama anatumia dawa za kulevya ama laa, na ikathibitika kwamba hatumii dawa hizo.

“Unajua kiasi cha dawa kilichokutwa kwenye hiyo mizigo ni cha matumizi ya mtu tu ambaye hutumia dawa za kulevya, kwahiyo ilibidi bosi apimwe mkojo lakini akabainika yupo salama,” kilieleza chanzo hicho.

Alipoulizwa na MTANZANIA kuhusu taarifa hizo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, alikiri kuzipokea na kusema kwamba mamlaka yake inaendelea na uchunguzi.

“Ni kweli tumepata taarifa hizo na tunaendelea na uchunguzi, japokuwa taarifa nyingi zina utata na inaonekana kuna mambo yanayoendelea ndani yakihusishwa na mgogoro wa kiuongozi,” alisema.

Msaidizi wa Postamasta Mkuu, Abubakar Athuman, alipoulizwa juu ya dawa hizo kutegewa bosi wake, alisema suala hilo ni binafsi sana na inatakiwa alizungumzie Postamasta Mkuu ambaye kwa sasa yupo nchini Uswisi kikazi.

Alipoulizwa juu ya Mwamgabe kutoonekana ofisini, alisema Postamasta Mkuu ndiye anayepaswa kuzungumzia suala hilo.

Msemaji wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa, alisema hajapata taarifa kuhusu tukio hilo na kuelekeza kuwa huenda taarifa hizo ziko kwa watendaji wa chini na kuomba apewe muda kufuatilia.

NJIA ZA KUINGIZA DAWA ZA KULEVYA

Katika hatua nyingine, jana Kamishna Sianga alisema wamedhibiti uingizaji wa dawa za kulevya nchini na hali kwa sasa si kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Alisema kwa sasa wamebaini kuwa baada ya ulinzi kuimarishwa katika viwanja vya ndege na ukanda wa bahari ya Tanzania, wasafirishaji wa dawa hizi wameanza kutumia pwani ya Msumbiji kisha kusafirisha kwa njia za panya kuingia nchini kwa kutumia magari na pikipiki.

Sianga alisema tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma ambapo wasafirishaji walikuwa wakitumia zaidi watu waliokuwa wakimeza dawa hizo kuanzia nusu kilo hadi kilo mbili, kwa sasa wasafirishaji wanatumia njia ya kuficha dawa hizo katika mabegi na mizigo na kusafirisha kwa njia ya ndege na majahazi.

“Lakini zaidi tumebaini kwamba wasafirishaji wamekuwa wakichukua vijana hapa na kuwapa mafunzo, kisha kuwapeleka Afrika Kusini, Angola na Msumbiji ambako huwabebesha mizigo na kuondokea huko.

“Lakini pia tumebaini wanatumia wazee wa hadi miaka 80 na watu wa nje kusafirisha… kuna babu mmoja wa miaka 80 alikamatwa akiwa na dawa za kulevya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,” alisema.

Alisema tangu kuanza kwa ushirikiano baina ya Mamlama yake na vyombo vya ulinzi vya kimataifa ikiwemo Indian Ocean Forum on Maritime Crimes mwaka 2010 na baadaye Combined Maritime Forces/ CTF 150 vinavyohusisha muungano wa majeshi ya nchi mbalimbali katika bahari ya Hindi vilivyoanzishwa kudhibiti uharamia, imesaidia ukaguzi wa meli na kupungua kasi ya usafirishaji wa dawa za kulevya katika pwani ya bahari hiyo.
Hapa kuna mkanganyiko pia inaelekea boss ndiyo katengeneza Sinema ili apatee kisingizio cha kumkomoa pengine kakimbia kubambikiwa kesi yafaa wachunguzi wenye weledi na mbinu za kisayansi wachunguze hilo Tukio sio wale waliochunguza lile tuko la MO ambao walichunguza kianalogia sana.
 
Aliyekimbia pengine ni mnyonge kakimbia kukwepa kubambikiwa kesi na boss ambaye pengine kaandaa mtu mwake wa kumwajiri, au vilevile yawezekana aliyekimbia kakimbia baada ya kuona mbinu yake ya kuharibia boss imefelli vyote vinawezekana kuwepo cha Msingi ni Uchunguzi mzuri ufanyike na uwe uchaguzi wa hapa pasipo Rushwa kupenyezwa ndipo Ukweli utajulikana.
 
Cheo ni dhamana

Kuna uwezekano wa kukomoana au kukomeshana au kuna uwezekano wa kutengeneza mazingira ya kusaka kisingizio pia ni uchaguzi huru na wa haki utaweza kutoa jawabu la kweli
 
HAPA SIONI BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA. WHY? KIASI NI KIDOGO MNO UKIFANANISHA NA NAFASI YA MTUHUMIWA. SIONI KWANINI MTU MWENYE NAFASI HIYO AFANYE UZEMBE NA AHATARISHE NAFASI YAKE KWA KIASI HICHO KIDOGO CHA MADAWA YA KULEVYA.

UKISOMA HIYO STORY UNAONA WAZI AMA LIKO BIFU AU KATUMWA MTU KUMCHAFUA MTU SASA UNAJIULIZA MKUU WA USALAMA HAWEZI KUWA MKUU WA SHIRIKA. SASA KATUMWA NA NANI?

MAELEZO HUMO HAYAJITOSHELEZI.
NA HUYU ALIYELETA UZI HUU WA MASWALA YA NDANI YA SHIRIKA ANA MASLAHI GANI?
AU AMEONA BAADA YA KUHAKIKISHA IMEANDIKWA GAZETINI AKAONA HAIJAPATA COVERAGE YA KUTOSHA AKAONA AJE HUKU?

SOMEBODY IN POWER AINGILIE KATI KABLA HAWAJAHARIBU SHIRIKA LETU LA POSTA AMBALO KIMSHINGI LINAPAMBANA NA USHINDANI WA KUTOSHA KWA SASA.
FUJO ZA NDANI TENA?
 
Post office security chief is entitled to a presumption of innocence

Huwezi kumtega mtu madawa kwa kumtumia package, kutumiwa package ya madawa sio kosa kwa sababu naweza kutuma package ya madawa nikaweka address ya "Freeman Mbowe," au "Tundu Lissu" ambao tumetangaziwa ni "maadui wa nchi." Mtaenda kumkamata Mbowe? Kosa ni kupokea package, kwa aidha:

1. kuifuata mwenyewe posta (which means ulikuwa unategemea mzigo kutoka kwa mtumaji)

2. kuletewa nyumbani ukasaini ukapokea (which means unamjua huyo aliyekutumia

3. kukuta mzigo umedondoshwa nyumbani, ukaufungua ukakaa nao bila kutoa taarifa (which means umeumiliki)
 
HAPA SIONI BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA. WHY? KIASI NI KIDOGO MNO UKIFANANISHA NA NAFASI YA MTUHUMIWA. SIONI KWANINI MTU MWENYE NAFASI HIYO AFANYE UZEMBE NA AHATARISHE NAFASI YAKE KWA KIASI HICHO KIDOGO CHA MADAWA YA KULEVYA.

UKISOMA HIYO STORY UNAONA WAZI AMA LIKO BIFU AU KATUMWA MTU KUMCHAFUA MTU SASA UNAJIULIZA MKUU WA USALAMA HAWEZI KUWA MKUU WA SHIRIKA. SASA KATUMWA NA NANI?

MAELEZO HUMO HAYAJITOSHELEZI.
NA HUYU ALIYELETA UZI HUU WA MASWALA YA NDANI YA SHIRIKA ANA MASLAHI GANI?
AU AMEONA BAADA YA KUHAKIKISHA IMEANDIKWA GAZETINI AKAONA HAIJAPATA COVERAGE YA KUTOSHA AKAONA AJE HUKU?

SOMEBODY IN POWER AINGILIE KATI KABLA HAWAJAHARIBU SHIRIKA LETU LA POSTA AMBALO KIMSHINGI LINAPAMBANA NA USHINDANI WA KUTOSHA KWA SASA.
FUJO ZA NDANI TENA?
Board of Directors nayo imekosa sifa ya kulisimamia Shirika.
Ama wamelea ugonjwa tangu mwanzo kwa kuwabeba CEO na Security Officer.
Itabidi Wizara Mama aingilie.
 
Post office security chief is entitled to a presumption of innocence

Huwezi kumtega mtu madawa kwa kumtumia package, kutumiwa package ya madawa sio kosa kwa sababu naweza kutuma package ya madawa nikaweka address ya "Freeman Mbowe," au "Tundu Lissu" ambao tumetangaziwa ni "maadui wa nchi." Mtaenda kumkamata Mbowe? Kosa ni kupokea package, kwa aidha:

1. kuifuata mwenyewe posta (which means ulikuwa unategemea mzigo kutoka kwa mtumaji)

2. kuletewa nyumbani ukasaini ukapokea (which means unamjua huyo aliyekutumia

3. kukuta mzigo umedondoshwa nyumbani, ukaufungua ukakaa nao bila kutoa taarifa (which means umeumiliki)
My local investigation:
1: Guys (CEO & Security) were friends.They know each other
2:Security guy help CEO to acquire the post
3: Security demands much, which CEO hesitate to fulfil
4: Conflict of interest in some of tenders, there is an auditing query impinch the Security guy.
5: Toto's
 
HAPA SIONI BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA. WHY? KIASI NI KIDOGO MNO UKIFANANISHA NA NAFASI YA MTUHUMIWA. SIONI KWANINI MTU MWENYE NAFASI HIYO AFANYE UZEMBE NA AHATARISHE NAFASI YAKE KWA KIASI HICHO KIDOGO CHA MADAWA YA KULEVYA.

UKISOMA HIYO STORY UNAONA WAZI AMA LIKO BIFU AU KATUMWA MTU KUMCHAFUA MTU SASA UNAJIULIZA MKUU WA USALAMA HAWEZI KUWA MKUU WA SHIRIKA. SASA KATUMWA NA NANI?

MAELEZO HUMO HAYAJITOSHELEZI.
NA HUYU ALIYELETA UZI HUU WA MASWALA YA NDANI YA SHIRIKA ANA MASLAHI GANI?
AU AMEONA BAADA YA KUHAKIKISHA IMEANDIKWA GAZETINI AKAONA HAIJAPATA COVERAGE YA KUTOSHA AKAONA AJE HUKU?

SOMEBODY IN POWER AINGILIE KATI KABLA HAWAJAHARIBU SHIRIKA LETU LA POSTA AMBALO KIMSHINGI LINAPAMBANA NA USHINDANI WA KUTOSHA KWA SASA.
FUJO ZA NDANI TENA?

Wengi hawajajua jinsi gani ya kukikabili kimbumnga tulichonacho na kijacho, mbinu za zamani sasa hivi nyingi hazifanyi kazi na matokeo yake ndio hayooo ya kuviziana kazini halafu nia ovu inabuma kirahisi, atake asitake Boss hapa kashika mpini naye Mwamgabe kashika kwenye makali
 
Hivi morogoro hatuna ukaguzi wa mizigo? Nchi ipo hatarini kusafirisha silaha kupitia post office.
Enzi zile haikuwa hivi.


Nimeshangaa! Lakini kama ni "Enzi zile" nazofikiria mimi, then things were worse kuliko sasa! Sema binaadam ni zaidi ya panya ukiziba hapa anafungua kule!
 
Possibly.Ila dah,uadui utakuwa ni mkubwa sana,that is going too far.

Huyo Afisa Usalama naye inaonekana he has connections somehow to drugs,amezipata wapi?Akipatikana ashuhulikiwe kikamilifu.

Finally mkuu kuweza kutambua kwamba hako kamzigo kalikuwa na ngada haikuwa rahisi,kwa kuwa kwanza no body would suspect, kwa kuwa mambo yenyewe yalienda kiofisi ofisi.Na imagine kama ingekuwa mimi,I believe it would be the same story!

Kuna watu wamebarikiwa roho za kisasi huwezi hata kuamini ni binadamu! Sad kwa kweli!
 
Huyo Afisa Usalama naamini akienda kuombewa atatoa mapepo mengi sana,I believe he is demon possesed.Yaani hana roho ya ubinadamu kabisa.

The bitter truth is, "they live among us".....hata kwa maombi hawaondoki! Walishaandikwa kwamba 'watakuwepo wabaya zaidi ya hayawani wa mwituni', Kwahiyo lazima maandiko yatimie.
 
Back
Top Bottom