Dawa za Kulevya: Wasanii na watuhumiwa wengine wafikishwa Mahakamani, wapata dhamana

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
HabariJF,

Wasanii akiwemo Tunda, Wema na Rachael na baadhi ya watu wanaoshikiliwa na kituo cha polisi kati kwa tuhuma ya dawa za kulevya wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

IMG_3032.JPG

IMG_3033.JPG

IMG_3015.JPG


Watuhumiwa hao wameshushwa nyuma ya majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku baadhi ya wakijifunika nyuso zao kukwepa camera za mapaparazi...



IMG_3025.JPG


======
UPDATE:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa amri kwa TID na wenzake saba kufanya yafuatayo;

1. Kusaini dhamana (bond) ya Milioni 10.

2. Kuwa na tabia nzuri kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

Hivyo watuhumiwa wote wako huru wakishatia saini karatasi za Bond.


======
HIVI PUNDE:

Mahakama imekubali maombi ya Jamuhuri kuhusu tuhuma zinazomkabili Petitiman na wenzie wanne, watakuwa nje kwa dhamana ya shilingi milioni 20.
 
Viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu vimesheheni wazazi,walezi,wapenzi,waandishi na mashabiki wa watuhumiwa wa madawa ya kulevya wanaotarajia kupandishwa kizimbani hivi punde.

Kati yao,yupo mlimbwende,msanii na Miss Tanzania wa zamani Wema Sepetu. Mawakili wamejitokeza kwa wingi na kwa ari kubwa. Ingawa nipo hapa kwa shughuli zangu binafsi,nitaarifu nitakachokipata. Taarifa zaidi zitafuata.

SAHIHISHO: Wema hakupandishwa kizimbani bado!
 
Watembelee na pale Mikocheni,karibu na Mabwawa ya maji taka.Kuna kijiwe cha mtoto wa mkubwa pale ambacho huwa kinaanza kuchanganya kuanzia jioni.

Nje kuna bendera ya Tawi la Chama kubwa,watoto wa kishua huwa wanakutana ku-sniff na kupiga pombe.Tumeshawapa uelekeo,ili ile kauli ya Mkuu wa Kaya kuwa vita hivi havichagui "brand" kama alivyosema [HASHTAG]#Nape[/HASHTAG] viweze kutimia.

Rachel waliomfundisha ni hicho kijiwe cha Mikocheni

Pale ndio maskani ya kina Babuu na Wakuvanga!!Inaposemwa vita hii ni kubwa!!Inamaanisha kuwa wakitajwa wahusika hasa,kuna makaburi ya zege yasiyofukuliwa.

Wakimaliza hapo wapite na pale Magomeni Chipolopolo!!Pale huulizi,ila unaulizwa unataka cha wapi?Brazili au "mapumba" ya Pakistan yaliyochanganywa hovyo!!
 
Back
Top Bottom