Dawa za kulevya janga la taifa

Dawa za kulevya janga la taifa

Nsera Ndawani

Senior Member
Joined
May 5, 2013
Posts
136
Reaction score
38
Ni ukweli usiopingika taifa ambalo vijana wake ambao ni nguvu kazi , wakijiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya ,sii tuu nchi itakuwa na watu mazezeta, pia nchi itakuwa masikini wa kutupwa na tegemezi .

Na nchi itaporwa rasilimali kirahisi kwa kuwa vijana watakuwa hawana uwezo wa kusimamia rasilimali za Taifa.

Lakini pia kwa upande wa kimataifa nchi yetu ya Tanzania imepoteza sifa kubwa tuliyokuwa nayo mwanzo, kwa sasa wasafiri wa kitanzania wanaosafiri kwenda nje ya nchi upekuzi umekuwa ni mkubwa sana tofauti na mwanzo.

Kumekuwa na taarifa mbalimbali zinazosikika kwenye vyombo vya habari, kuhusiana na watanzania wengi kukamatwa na idadi kubwa ya dawa za kulevya nje ya nchi.

Cha kushangaza hizo dawa zinapitia kwenye viwanja vyetu vya ndege ambavyo vina ulinzi mkubwa wa vyombo vya dola.

Kwa sasa nchi kama china kuna vijana wengi wa kitanzania wako magereza wakingoja kunyongwa.

Lakini kuna tetesi kuwa hawa vijana wamekuwa wakifanya hizi biashara kwa usimamizi kutoka kwa watu wakubwa wakiwepo wanasiasa.

Hili la wana siasa kusimamia biashara ya dawa za kulevya kama taarifa zinavyosikika sina mashaka nalo, kwani kuna wakati viongozi wa kisiasa hapa nchini walisema wanayo majina ya wahusika na watatajwa, lakini hadi leo hatujasikia majina ya hao wauwaji wa vijana na Taifa letu.

Nivipongeze baadhi ya vyombo vya habari hapa Tanzania ,kwa kujaribu kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya dawa za kulevya .

kuna kipindi kinacho rushwa na ITV, kila siku ya Alhamisi usiku kinaitwa malumbano ya hoja .

kimekuwa ni kipindi huru kinachokutanisha watu mbalimbali kuzungumzia mambo mbalimbali yanayolisibu Taifa letu.

Jana nilitazama hicho kipindi ,na mjadala ulihusu dawa za kulevya na kulikuwa na wazungumzaji wakuu ,ambao baadhi wakitoka kwenye idara ya jeshi la polisi.

katika huo mjadala kuna watu wengi walichangia vizuri sana, lakini cha kushangaza walipokuwa wakichangia walikuwa wakikatizwa na mtangazaji hata kabla ya kumaliza dakika mbili walizokuwa wamepewa.

Katika ule mjadala ilionekana wazi jeshi la polisi kushindwa kabisa kujibu baadhi ya maswali yaliyoelekezwa kwao, na wakati wote wakisaidiwa na mtangazaji kukatiza baadhi ya hoja za msingi zilizoelekezwa kwenye vyombo vya dola .

Ninashauri kipindi kiwe huru na watu wapewe muda wa kujieleza. Kwa sasa uwezo wa vyombo vyetu vya dola kiutendaji uko chini ya kiwango.

Ninasema hivyo kwa sababu taarifa za watu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya wanapewa wanashindwa kuzifanyia kazi

Swali
vyombo vya dola vinafahamu madhara ya dawa za kulevya?

Ni kweli hizi dawa za kulevya zinapopitishwa katika viwanja vyetu jeshi la polisi halizioni?
 
Back
Top Bottom