Dawa ya wanasiasa hii hapa!

Dawa ya wanasiasa hii hapa!

JRK

Member
Joined
Jul 10, 2012
Posts
47
Reaction score
11
Duniani kuna binadamu halafu kuna wanasiasa. Binadamu wengi huwa wanajitahidi kuwa wanasiasa na siku hizi kila kona wamejaa na wanaboa kweli. Kazi kubwa ya wanasiasa ni kuongea, wakitumia midomo yao, wanaweza kukufanya uamini kuwa wao ndiyo wanajua kila kitu.
Tena wanasiasa wengine huwa wanafikia kuamini wanajua kila kitu. Ukimuuliza kuhusu kilimo anajua, uvuvi anajua, teknolojia yoyote anajua, we anzisha mada mwanasiasa anajua na atakupa majibu ya namna ya kuboresha kila kitu hata kama hajawahi kukifanya wala kukisikia.
Huyo ndiye mwanasiasa na wako wengi, kwa kuwa fani yao ni kuongea ukikosea ukawaruhusu waongee utajuta kuzaliwa, wao hawajali muda gani unawasikiliza wao wataongea tu. Lakini leo nataka niwapeni dawa yao. Hawa wanasiasa wako kila mahala, mradi wakijua kuna watu wanawasikiliza basi hufungua maktaba ya ujuzi wao, na siku hizi wameingia kwenye sherehe na misiba.
Mtu anaalikwa mgeni rasmi kwenye sherehe, kabla ya chakula anaombwa azungumze, hilo linakuwa kosa. Kitu cha kwanza ukitaka kujua anayeanza kuongea ni mwanasiasa, utasikia wana kasentensi kao wanakoanzia utasikia, “Ndugu zangu hapa kwa kweli si mahala pa hotuba kwa hiyo sitasema mengi…” akianza hapo ujue nusu saa itapita bado anaongea. Au kwenye sherehe za harusi baba mzazi akiambiwa atoe wosia basi tabu imeanza, ataongea historia toka alipokuwa mtoto mpaka alipooa na hatimaye kuzaliwa wanaooana na ataendelea, hamalizi!
Dawa yao nimeipata, siku hizi kuna watu wanaalikwa kutoa machache msibani, kabla ya mazishi au baada ya mazishi, basi ndiyo utajua kuna mwanasiasa, ataongea mambo kibao hayana hata uhusiano na msiba. Dawa yao leo nakupatia. Ukishasikia mtu kaanza kale kasentensi kao kanakoanzia, “Hapa siyo mahala pa kutoa hotuba…..” ujue mwanasiasa kaanza kazi yake.
Ukiona kaongea anakuchosha, au anaongea kabla ya chakula mpaka chakula kinapoa haachi hotuba, au anaongea mno kabla ya mazishi na muda unapita bila sababu, dawa yake ni hii. Chukua karatasi andika maneno manne tu, kama mwanasiasa ni mwanaume andika SAMAHANI MZEE ZIPU IMEFUNGUKA… kama mwanasiasa ni mwanamke andika….SAMAHANI MAMA SIDIRIA IMEACHIA….hakikisha kijikaratasi hicho kinapita mpaka kumfikia mwanasiasa wako. Sekunde mbili baada ya kusoma kikaratasi hicho, Utasikia “Kwa hayo machache namalizia hapo.”
 
Hata wewe ni mwanasiasa aisee...
Manake maelezo yako yanachosha sana.
 
mm nakupa zote mbili zipu imeachia na sindiria imefunguka.
 
Back
Top Bottom