Dawa ya Vikojozi

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
3,475
3,231
Wadau, Naomba tusaidiane katika kujadili hili suala la watoto ambao wamefikisha miaka 10 au zaidi kuendelea kukojoa kitandani, wakiwa wamelala usiku. Je, tataizo ni nini? na matibabu yake ni yapi?
 
Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,068
1,345
mimi nilikojoa kitandani hadi karibia miaka kumi na nane halafu ikaacha yenyewe hali hiyo.
 
mgange hussein

Senior Member
Sep 10, 2012
158
43
Pole sana.Jaribu kupanga utaratibu wewe mwenyewe wa kumjengea utaratibu wa kumuamsha kila baada ya masaa 3.
 
Mwadilifu

Member
Feb 13, 2011
74
20
I would suggest kama mtu uko vizur ni bora kuchek na system yote ya mkojo,mfano figo kama zipo safi na vi2 ka hivyo,haya mambo huwa tunachukulia easy na kumtreat mtoto harshly kumbe tatizo lingeweza kurekebishika mapema,bt linaachwa na kujikita miziz
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,598
1,533
Mkuu Q Man,

Tatizo la kukojoa kitandani(Bedwetting)..ama Nocturnal Enuresis..ni tatizo ambalo huwapata watoto(mara chache waru wazima) ambao kwa kawaida hutegemea kuweza kumudu utoaji wa taka mwili(kukojoa) wenyewe.

Kwa kawaida, katika Umri wa miaka miwili hadi minne watoto hujifunza kujimudu kibofu kujaa, na kukojoa.Hata hivyo bado kuna sababu zinazofanya kutomudu mkojo katika kibofu na kuutoa mwilini.Hizi hujumuisha;

Kurithi: Baadhi ya tafiti zinaonyesha, tatizo hili linaweza kuwa linarithiwa toka kizazi hadi kizazi hasa katika familia ambazo ni tatizo.

Unyanyasaji wa watoto: Tatizo hili huonyesha kuwa watoto ambao hunyanyaswa, hukosa kujiamini(less confident and low self esteem) ambazo humfanya kutojiamini na kumueleza mzazi/mlezi anapojisikia kwenda haja.

Matatizo ya kimaumbile: Baadhi ya watu(watoto)huwa na maumbile tofauti kidogo mf(bladder anomalies, matatizo ya uti wa mgongo n.k) ..pia baadhi ya matatizo mfano magonjwa ya kifafa, matatizo ya usingizi(OSA) yamekuwa yakihusishwa sana na kukojoa kitandani.

Madhara:
- Kijamii, mtoto kutengwa na kuzidi kutojiamini.(harufu) na kutaniwa.
-Kiafya- Kuharibika kwa ngozi hasa kutokana na kuwashwa kwa mkojo.

Vipimo:
-Kutokana na tatizo hili kuhusishwa na malezi sana vipimo vichache hufanyika na USHAURI zaidi ndiyo kutolewa.Hata hivyo vipimo vya mkojo, picha za viungo vya ndani,(USS, Cystogram n.k)

Matibabu:
-Kumueleza mtoto(kumshauri INGAWAJE NI "mdogo",
-Kumwamsha usiku kwa vipindi(baada ya masaa kadhaa) ili akojoe.
-Kupunguza kutumia maji mengi sana wakati wa jioni(watoto wengi hutumia REHYDRATION baada ya kucheza na kutoka jasho jingi...Hii haimaanishi watoto wasicheze.
-Kutibu kwa upasuaji /dawa baada ya kuona tatizo katika vipimo.
 
Last edited by a moderator:

Asante sana mkuu
 
smallvile

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
493
236
hippocratessocrates kwa ufupi nimependezwa na maelezo yako,,
kuongezea,

toilet learning kwa watoto ni kitu ambacho anajifunza kutoka kwa jamii, kama jamii inayomzunguka haina toilet practice nzuri kwa ujumla mtoto anaweza pata matatizo,,,matatizo ya kimaumbile, kurithi, yapo lakini sio significant kutaja ya kwanza,,
nimefurahishwa na unyanyasaji wa watoto,, hili ni tatizo kubwa especially pale mlezi anapodhani kumpiga mtoto anaekojoa ni njia sahihi ya kumsaidi, ikumbukwe kama alitangulia kusema ndugu ni kwamba hawa watoto wanakua na umri wa just kuanzia miaka 4 ndo tunasema ni tatizo hivo bado wana umri mdogo kupigwa

mazingira mapya, hili ni tatizo kwa wengi, familia inapohamia makazi mapya au yale yaliyopo yanapompa hofu mtoto kutumia huduma hii ipasavyo, na hili tatizo litakua Secondary Bedwetting kama atakua alishaweza kujitunza
aina ya choo, kilivo choo, usiri wa mtu anapokua chooni, mahali choo kilipo ndani au nje ni baadhi ya mambo ambayo yanaelekea kuathiri ukuaji wa mtoto katika swala zima la bladder control

tatizo linakua Primary kama mtota haijatokea akaweza kujisitiri tangu kuzaliwa,,,

magonjwa ya njia ya mkojo pia yanaweza kumsababisha mtu akakosa bladder control,

kwa watu wazima ambao ni secondary, magonjwa ya uzeeni, ujauzito msongo wa mawazo ni baadhi tu kutaja ambayo yanaweza mpa mtu alose bladder control,

dawa, ,
almost always kwa watoto dawa ni training, psychotherapy, cuting down abuse if any, na kurekebisha mazingira ya choo yawe condusive kwa watoto
kama alivotangulia kusema kumwamsha usiku, kumreward mtoto baada ya kumpa zoezi ya kwamba kama ataweza kuamka mwenyewe atapewa zawadi, insentives
kuepuka vyakula vyenye vimiminika sana wakati wa jioni kabla ya kulala, especially cafein soda ,na the like,
epuka kumvalisha mtoto diepers baada ya umri huu maana itakua inamshawishi kuendelea kukojoa
epuka kuendelea kutumia hash ways maana izi zitakua another sort of abuse kwa mtoto

kama kweli unampenda hutampiga
 
Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,575
521
mpikie utumbo wa kuku na mchanganyie na nyama kidogo ataacha kabisa ila usimwambie kama ni utumbo wa kuku
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom