Dawa ya Utando Mweupe kwenye ulimi wa mtoto

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,605
501
Habari Wakuu,
Nina mtoto wa miezi 3...ana utando mweupe kwenye ulimi wake kama maziwa hivi....tumempeleka Hospital amepewa Dawa but hauishi.

And sometimes akicheua huwa anacheua maziwa mengi sana kama ametaapika hivi na siyo kwa mara moja tu.

Najua huku kuna watu wazima na Madaktari huwa wanapita huku....Pls nisaidie kama unajua dawa yake....Thanks!!!!
 
Habari Wakuu,
Nina mtoto wa miezi 3...ana utando mweupe kwenye ulimi wake kama maziwa hivi....tumempeleka Hospital amepewa Dawa but hauishi....and sometimes akicheua huwa anacheua maziwa mengi sana kama ametaapika hivi...na sio kwa mara moja tu....najua huku kuna watu wazima na Madaktari huwa wanapita huku....pls nisaidie kama unajua dawa yake....Thanks!!!!
Kamuone specialist wa magonjwa ya watoto mkuu, ila kwa kiasi kikubwa utaambiwa ni fungus anapata kwa nyonyo ya mama au kama mnampa ile midude ya kunyonyanyonya...!
Kama upo dar es salaam kuna dr. Masawe pale Morocco. Karibu na airtel makao makuu.
 
Asante Mkuu bigmind hatumpi ile midude ya kunyonya....niko Arusha nitamtafuta Specialist wa watoto...nataka tu kupata mawazo ya wazazi wengine amabao walishawahi kukutana na tatizo hili...
 
Wakati huo unamtafuta specialist wa watoto jaribu kumlambisha ASALI MBICHI kama utaipata mkuu
 
Kaka asali ni hatari sana kwa mtoto mdogo kama huyu, mumeng'enyo wake ni mgumu kushinda mfumo wa mumeng'enyo wa mtoto haishauriwi mtoto mdogo kupewa asali.
Nashukru kwa ushauri wako mkuu nitaufanyia kazi
 
Habari Wakuu,
Nina mtoto wa miezi 3...ana utando mweupe kwenye ulimi wake kama maziwa hivi....tumempeleka Hospital amepewa Dawa but hauishi....and sometimes akicheua huwa anacheua maziwa mengi sana kama ametaapika hivi...na sio kwa mara moja tu....najua huku kuna watu wazima na Madaktari huwa wanapita huku....pls nisaidie kama unajua dawa yake....Thanks!!!!
Iyo kawaida mno wala usiangaike inaisha yenyewe anavyoendelea kukua
 
Kaka nimekua naona kijijini kwetu madogo wanatibiwa kwa dawa za kienyeji kuna mti flani hivi sijui kwa Kiswahili unaitwaje, ule ndo naonaga wanavunja tawi lake then Yale maji maji yake yanatumiwa kusafisha ulimi wa mtoto kwa kusugua na kidole chako mpaka ule utando mweupe wote unatoka, sasa sijui km unaweza kukubali kumtibu mwanao kwa dawa za asili.
 
Huenda ikawa ni rangi ya kawaida hasa hasa kama upo maeneo yenye joto, ama inaweza ikawa ni ugonjwa (Oral thrush) ?Fangas, ambapo utaona wakat ananyonya havuti maziwa sawasawa, ama hanyonyi kabisa, ama analia sana baada ya kunyonya kidogo, ama kuambatana na vipele kwenye lips & Joto ..!!

Kwahiyo ili kutatua hayo yote ni muhim sana kwenda tena Hospital, usichoke kwenda maana watoto ndivyo walivyo, nenda tena Hospital.

Kwa sasa unaweza ukatumia Nystatin Oral Susp.
 
Kaka nimekua naona kijijini kwetu madogo wanatibiwa kwa dawa za kienyeji kuna mti flani hivi sijui kwa Kiswahili unaitwaje, ule ndo naonaga wanavunja tawi lake then Yale maji maji yake yanatumiwa kusafisha ulimi wa mtoto kwa kusugua na kidole chako mpaka ule utando mweupe wote unatoka, sasa sijui km unaweza kukubali kumtibu mwanao kwa dawa za asili.

Hapana hatakubali. Asugue ulimi wa mtoto wa miezi mitatu!. Hapa hapana. Bila shaka amekataa. ushauri mwingine?
 
Back
Top Bottom