Dawa ya tapeli/mwizi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya tapeli/mwizi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Senior Boss, Sep 20, 2012.

 1. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  Habari zenu wakuu...

  Wadau inakera sana mtu unaye muamini anavyoku dhulumu pesa ulioihangaikia kuitafuta kwa shida na uchungu sana..unamkopa kwa lengo la kumsaidia shida yake na kiustaarabu unampatia bila masharti magumu (ushahidi) yet bado anakuzunguka na kupotea nayo mazima. Another case mtu mwngne unamuweka akusimamie biashara yako....siku ya siku anatoweka na kiwango kikubwa cha fedha au kukuibia kinyemela inakua in a certain situation huna ushahidi wa kumfungulia mashtaka.....Kweli hii tabia inakera na inarudisha watu nyuma kimaendeleo. Nilikua naomba ushauri na mawazo yenu wakuu je, mtu wa namna hii tuna deal (shughulika) nae vipi ?? Maana kwa vyovyote vile pesa lazima irudi...vinginevyo itakua ni hasara kubwa na muda umepotea bure ukicheck wengine tuna majukumu mengi sana !!

  Ahsanteni sana !!
   
 2. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Mkuu Senior Manager,
  Kwa kweli hayo uliyoongea yanakera sana na kutia hasira. Na haswa ukizingatia vyombo vya Dola na sheria havifanyi kazi ipasavyo kushughulikia hayo MAJITU. Maana unaweza ukapigwa pesa na Huyo jamaa aliyekupiga akahonga vyombo vya Dola mchezo ukawa umeisha. Ukabaki ukienda Polisi unaambulia kauli Kama " Hizi kesi zenu za Kitaperi mkamalize kwa Serikali za mitaa" Eboo!

  Kuna jamaa yangu alipigwa mchanga wa macho Million 10 na Vijana wa mjini kwa karata ya kuagiziwa gari kutoka Japan.
  Alihangaika nao Kama miezi 6 bila mafanikio. Ndipo alipoamua kupanda boti na kwenda Pemba. Alichokifanya huko Pemba anakijua mwenyewe,Ila hiyo Mitapeli haikuchukua hata wiki 2 ikamtafuta yenyewe na kumrudishia hela nusu halafu nusu ya pili wakamalizia baadae. Hiyo MIJITU kwa kweli huwa inarudisha watu nyuma sana.
   
 3. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  We acha tu...inauma sana na ni mshkaji tunaheshimiana sana, ila mi niko tayari kwa lolote, lolote nalitokee...hela yangu atarudisha tu...ntauza hadi viatu nimshughulikie..sometimes i panic too much...ts a big loss kwa kweli !! For more advice wakuu mnaweza ni PM. Ntashkuru sana.
   
 4. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu. Usipanic kiongozi,maana utapoteza mwelekeo na umakini halafu wewe ndio ukaonekana tatizo.
  Tuliza akili fanya mambo kiumakini. Na uhakika humu JF utapata ufumbuzi wa Hilo tatizo.
  Pole sana mkuu.
   
Loading...