Dawa ya stress ni nini?

Dawa ya stress ni nini?

GenuineMan

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
7,068
Reaction score
16,381
Je ushawahi kupatwa na Stress.?

Hivi ukiwa na stress huwa unafanya nini? Au unafanyeje?

Kama Pombe hunywi au hautaki kunywa.
Na usingizi hupati.(insomnia)
Unafanyeje ili kuondokana nazo.?


Ulifanyeje kuondokana nazo?



NB! Stress ni mbaya,
zinachangia kushusha kinga ya mwili,
zinachangia kuongeza sukari mwilini.( Mbaya kwa mtu wa kisukari)
Zinachangia vidonda vya tumbo.
Zinasababisha mtu kunenepa

Zinapelekea Depression.
nk....

Na mbaya zaidi mtu aweza kujaribu kujitoa uhai ( Suicidal attempt)
 
Wafilipi 4:13 “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.

Isaya 41:10 “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”.

Isaya 40:31 “bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia”.

Kumbukumbu 31: 6 “Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha”.

Isaya 40:29 “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo”.

1Wakorintho 10:13 “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.

Kutoka 15:2 “Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza”.
 
Pole sana mkuu kwa uyapitiayo.
Stress katika zama hizi imekua ni jambo lisiloepukika, ukikoswa koswa huku lazma utapatikana kule.

Nini cha kufanya basi kukabiliana na hali. Naamini kila mtu yuko na upekee wake hivyo yale yatakayonisaidia yanaweza yasiwe yatakayo kusaidia, kwaiyo cha msingi ni kujijua kwanza, kwamba kitu gani kinakupa relief pale unapopata changamoto hiyo.

Kujichanganya na watu itakusaidia, pia mazoezi yale yatakayo ushughulisha mwili mzima, na ni vyema ukafanya hadi uchoke kabisa, tatu aina ya vyakula matunda, maji yakutosha na maziwa fresh vitakusaidia uweze kupata usingizi kwa haraka na mzuri, epuka vyakula vyenye sukari nyingi na wanga sana.

Cha mwisho lazma uangalie njia madhubuti zitakazo kurahisishia kutatua tatizo hilo, si yote utaweza kutatua papo hapo, mengine yatahitaji mda na yale yasiyotatulika lazma ukubaliane na hali na kuachana nayo. Si vibaya kushirikisha wale unaowaamini pia.
 
Mazoezi mkuu,fanya mazoezi mwili ukichoka kuna hormon flani inakuwa released kwenye damu so you feel rexed…na kingine tafuna karanga za almonds
 
Je ushawahi kupatwa na Stress.?

Hivi ukiwa na stress huwa unafanya nini? Au unafanyeje?

Kama Pombe hunywi au hautaki kunywa.
Na usingizi hupati.(insomnia)
Unafanyeje ili kuondokana nazo.?


Ulifanyeje kuondokana nazo?



NB! Stress ni mbaya,
zinachangia kushusha kinga ya mwili,
zinachangia kuongeza sukari mwilini.( Mbaya kwa mtu wa kisukari)
Zinachangia vidonda vya tumbo.
Zinasababisha mtu kunenepa

Zinapelekea Depression.
nk....

Na mbaya zaidi mtu aweza kujaribu kujitoa uhai ( Suicidal attempt)
Kunywa kvant
 
Je ushawahi kupatwa na Stress.?

Hivi ukiwa na stress huwa unafanya nini? Au unafanyeje?

Kama Pombe hunywi au hautaki kunywa.
Na usingizi hupati.(insomnia)
Unafanyeje ili kuondokana nazo.?


Ulifanyeje kuondokana nazo?



NB! Stress ni mbaya,
zinachangia kushusha kinga ya mwili,
zinachangia kuongeza sukari mwilini.( Mbaya kwa mtu wa kisukari)
Zinachangia vidonda vya tumbo.
Zinasababisha mtu kunenepa

Zinapelekea Depression.
nk....

Na mbaya zaidi mtu aweza kujaribu kujitoa uhai ( Suicidal attempt)
Uwezi kunenepa.
 
ukiwa na stress
1. sikiliza muziki mzuri unasaidia kupunguza mawazo
2. Jichanganye usikae peke yako mfano. nenda kutazama mpira, kijiwe cha draft, etc
3. faya mazoezi ya viungo na rafiki
4. tazama au sikiliza comedy huwa zinasaidia kurudisha mood
5. Nenda vacation kama unahela inasaidia kupumzisha akili

Mwisho japo sio kwa umuhimu kubaliana na hali halisi iliyokutokea kama ni kupata hasara, kuachwa na mchumba, kufukuzwa kazi n.k maana usipokubaliana na hali halisi itakuwa kama unatwanga maji kwenye kinu
 
Back
Top Bottom