Dawa ya msaliti hii hapa, wala usiumize kichwa

Dawa ya msaliti hii hapa, wala usiumize kichwa

Yaani aende aliwe huko na mimi nikae kimya?Enzi zile ambazo ugonjwa mkubwa wa zinaa ni kisonono kweli theory yako unaweza kujaribu. Akapigwe nje akuletee ukimwi tena uwe una habari ni ujinga kuendelea naye. Aende nje bila mimi kujua kitachotokea ni fate lakini nikijua ndio mwisho wangu kuwa nae . Ni sawa na kuonja sumu ili ujue kitachotokea.
 
Kama kufa tutakufa hata usipokufa kwa ukimwi utakufa kwa ajali mwanamke/mpenzi wako akitoka nje ya mapenzi atakaeenda kuipiga hatakuwa na uwezo wa kuiondoa hapo wala kuisongeza hapo ilipo sema tunapenda kujitoa ufaham bila sababu za msing so relax
 
Na je wakati huo utakuwa unamgonga tu kama kawaida?
 
HII NDIYO ADHABU KUBWA YA MPENZI ANAYEKUSALITI

Wanaume wengi wanapogundua kuwa wapenzi wao wanawasaliti, wanatunisha misuli kuonesha umwamba kwakuwatwanga makonde wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa watalaam wa mapenzi unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.

Wapo wengi ambao wamewafumania wake zao, wamewapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi yakuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana kwa maneno kama vile:“mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi Wanaenda zao Gesti au sehemu yoyote wanayoijua” au utasikia“vipi yule alikuuliza jana ulipochelewa kurudi”

Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenziwa mtu Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana mume/mke au mpenzi. Watu huazimana magari na pesa, lakini kwa mpenzi hakuna jasiri wa namna hiyo!Hivyo ndivyo inavyokuwa lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia?

Jibu ni kwa hakusaidii, kwasababu ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo, kesho yake watakutana watakusaliti tena na kupozana machungu. Maamuzi ya kuachanaye hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona wameshikana mikono mitaani kwa uhuru na raha zao.

Kwa sababu ukiamua kuua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila siku, kwani si huwa tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku? Sasa kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali akibembelezana na ‘kidume chake’ mwingine kwa maeneo fulani.

Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa umeona lile la stejini laivu bila chenga. Twende pamoja ili tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi msaliti. Kwanza, baada ya kuwaona usokwa macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa umewaona, halafu ondoka eneohilo.

Ukishafika home, mtu mzima nini pale endelea kunywa zako maji ili kupoza presha.Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha, lakini usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe. Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza, halafu baada ya kumaliza uchunguzi wako mtumie tena sms hizo mkeo/mumeo.

Ukifanya hivyo usimuulize, endelea kumpenda na ikiwezekana ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’ akaange kila siku na umpe penzi moto moto.Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hatoweza kukusaliti kwa kwasababu atakuwa anawaza unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache! Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu msaliti.

Mwadhibu kwa upole, wanasaikolojia wameithibitisha adhabu hii ninayokweleza hivi sasa kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya kupiga au kukemea. Ukisemaumwache siyo dawa kwani unaweza kutafuta mwanamke/mwanaume mwingine nayeye akawa na tabia zile zile, sasa kama ikiwa utaamua kuacha, utaachana na wangapi katika maisha haya maana usaliti upo?

Adhabu ya mpenzi anayekusaliti ni kumnasa kwenye usaliti wake kisha kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia kupunguza maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi kili siku hakusaidii.

Na magonjwa vipi
 
Mkuu umesahau.. Piga picha na kumrusha kwenye insta.. Whatsapp... Nk

ndiooo! asante kwa kunikumbusha yaani nitahakikisha ulimwengu wote umejua yeye ni msaliti wa ndoa
 
Hii ngumu kwangu coz nimejaribu kuvaa uhusika nikagundua kuwa nikikaa kimya lazima nipasuke mimi maana nitashindwa kuhimili maumivu ya moyo atayokuwa kanipa.
 
Hii ngumu coz ilishanitokea na nikapiga window chini ( nikaachana na demu wangu) ingawa iliniumiza kuachana naye na pia sikukurupuka kumwacha bali nilitulia mpaka akasahau dhambi yake kisha nikamwacha kwa surprise ili afeel pain kama nilivyokuwa nikijisikia.
 
Usaliti ni hulka ya mtu km nyantu nyantu hata hufanyaje ana midumu ya petrol kibao we jfanye unaongeza mapenzi akulipue ndio utaelewa ukiwa kuzimu
 
kuna jamaa kapewa hiyo adhabu ya namna hiyo kaja na series ya matukio, hadi lifti ya boda boda anaogopa..........!, sema inauma dizain
 
unaotupa ushauri tupo humu Jf na wanaotusaliti wamo humu Jf,na njia ya kutibu hilo tatizo tumelisoma sote wasaliti na wasalitiwa.
Sina uhakika na njia hii kama italeta matokeo chanya mana hapa Jambazi kamuua sterling unategemea nini?
 
Nyooo! Uendelee kumpa mapenzi moto kama amekuletea moto si una ungua? Hii sio kabisa ntamng'oa hayo meno akose wa kumtamani
 
Back
Top Bottom