Dawa ya mpenzi anayekukalia kimya ni nini?

Katika mahusiano kuna wakati mpenzi wako akaamua kukukalia kimya au kukuchunia bila sababu au kwa sababu zake anazozijua yeye akaamua tuu kukaa kimya hakutafuti wala nini?

Unadhani nini suluhisho la tatizo hili. Ikifikia hatua hii hebu tupeane mawazo kuna ndugu yangu kaniomba ushauli
Mtumie laki mbili atakujibu
 
Yamenikuta hayoo ila nilichojifunza

Mtu anayekukalia kimya mwache kama alivyo ji keep bize na mambo yako alafu hata mkiwasiliana usipende kumuuliza siku Hizi mbona upo kimya sijui umebadilika utampa kichwa wee jifanye hujui kinachoendelea na hiyo hali hakuumizi jinsi anavyozidi kukaa kimya we jifanye uko bizee sana siku hizi kiasi kwamba ahisi kuna mchongo gani umeupata

Akikaa kimya tuseme labda week mpigie simu jifanye ukoo mtwara kwa dangote kuna mishe umekuja kuipiga na jifanye Kama unaomba msamaha Week nzima hujamcheki mambo yamekubana kweli siku hiZi.

Nakuambia utaanza Kumumiza moyo Kwan mtu anayekukalia kimya lengo lake akuone ukitapa tapa sasa anapokuona ukimya wake Haukumizi wala kuangaika nae hujikuta yeye ndo anaumia zaidi kitendo cha wewe akuone ukoo bize mpka unamsahau kutaanza kurudisha heshima hata kama alipanga kukumwanga anarudi hatua mbili nyuma kisha anabaki kukuangalia na akose nini cha kufanya Siku zinavyosonga mbele anabakia na maumivu hiyo ndo dawa yake ukiona mtu yupo kimya usiulize kitu Bali na ww jifanye uko bize Sana siku izi
 
Back
Top Bottom