Dawa ya Mchungaji Ambikilie inatibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya Mchungaji Ambikilie inatibu

Discussion in 'JF Doctor' started by Mtumiabusara, Apr 30, 2011.

 1. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Uchunguzi wa NIMRI,MUHAS
  Uchunguzi wa awali uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba cha Muhimbili (MUHAS) umebaini kwamba dawa ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapila ina uwezo wa kutibu magonja sugu zaidi ya sita.

  Katika ripoti yao wamependekeza kufanyika kwa utafiti zaidi juu ya uwezo wa dawa hiyo katika tiba, usalama, kiwango cha dozi anachopaswa kutumia mgonjwa na muda wa matumizi.

  Wataalamu waliochunguza dawa hiyo iliyosisimua na kuvuta watu wengi ndani na nje ya nchi kwenda katika Kijiji cha Samunge, Wilaya ya Loliondo, Arusha kwenda kupata dawa hiyo wamesema imewastaajabisha kwa namna ilivyo na kemikali nyingi zenye uwezo wa kuimarisha afya ya binadamu.

  Wataalamu hao, Profesa Hamisi Malebo na Profesa Zakaria Mbwambo wamesema utafiti huo wa awali umeonyesha kuwa dawa hiyo ina uwezo wa kudhibiti ugonjwa wa kisukari, moyo, saratani, ini, malaria, Ukimwi na magonjwa mengine yanayosababisha uvimbe mwilini, vidonda pamoja na athari za bakteria mwilini.

  Magonjwa mengine yanatajwa kuwa ni ya mfumo wa chakula, athari za mfumo wa akili na moyo kushindwa kufanya kazi sawasawa.

  “Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapaswa kuendesha majaribio ya utafiti ili kujibu maswali muhimu kama vile usalama wa dawa hiyo katika mwili wa binadamu, dozi yake pamoja na muda wa matumizi kulingana na aina ya ugonjwa,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo yenye kurasa 25.

  Jambo jingine ambalo wataalamu hao kutoka katika vitengo vya tafiti za dawa za asili wa NIMR na MUHAS, wanalisisitiza katika utafiti huo ni uwiano wa kemikali kwenye dawa ya mti huo walioupa jina kuwa ni wa maajabu.

  Ripoti hiyo ambayo Mwananchi ilifanikiwa kuiona, ina sehemu saba ambazo zinajumuisha shukurani kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kugharimia utafiti huo, maelezo kuhusu mti huo wa ajabu, muoanisho wa mti huo kibaiolojia, njia walizotumia kutafiti na matokeo yake, maelezo ya majumuisho na mapendekezo.

  Uchunguzi wa kimaabara
  Ripoti hiyo inaeleza kwamba katika kuchunguza sumu iliyopo katika mti huo, walitumia panya na kubaini kwamba ni salama pale ambako haitumiki mizizi hiyo moja kwa moja.

  Wataalamu hao wanaeleza njia anayotumia Mchungaji Mwasapila ya kuichemsha na kutoa dozi ya milimita 200 kwa mgonjwa ni salama na haiwezi kumuathiri binadamu kiafya.

  Wanasema kemikali zilizopo kwenye mti huo zimeonekana kuwa na uwezo wa kudhibiti magonjwa kama ambavyo Mchungaji Mwasapila amekuwa akieleza.Wanasema walipompa panya dawa hiyo, iliweza kuweka uwiano mzuri wa sukari kwenye mfumo wa damu hivyo kuashiria kwamba ina uwezo wa kutibu kisukari.

  Hali hiyo inaelezwa kuwa inatokana na mti huo kuwa na mfumo unaoweza kusababisha muanisho wa utoaji wa insulini ambayo kwenye mwili wa binadamu ni muhimu katika kusawazisha kiwango cha sukari mwilini.

  Kuhusu ugonjwa wa moyo, wataalamu hao wanasema dawa ya Babu ina uwezo wa kushusha mapigo ya moyo ambayo yako juu hivyo kuweza kudhibiti maradhi hayo.

  Mti huo pia umeonekana kuwa na uwezo wa kurekebisha ini ambalo halifanyi kazi zake inavyotakiwa hivyo kutibu aina zote za magonjwa zinazotokana na athari za kushindwa kwake kufanya kazi.

  Kwa mujibu wa maelezo ya kitaalamu, moja ya kazi za ini ni kuondoa sumu mwilini na iwapo halifanyi kazi zake sawasawa, sumu hizo husababisha madhara mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.

  Wameuelezea uwezo huo kuwa unasaidia kupambana na ugonjwa sugu wa saratani.Utafiti huo pia umeonyesha kuwa mti huo wa maajabu una uwezo wa kudhibiti virusi wa aina mbalimbali kama vile vya Ukimwi na polio. Wataalamu hao walieleza kwamba walipojaribu kulinganisha panya walioambukiza virusi, aliyetibiwa kwa mti huo aliongeza uwezo wa kuendelea kuishi kwa kati ya asilimia 28 hadi 35 ukilinganisha na yule ambaye hakutibiwa.

  Ilionekana pia kuwa panya walioathiriwa na virusi waliotibiwa na dawa hiyo waliepushwa na uwezekano wa vitoto vyao vilivyozaliwa kufa mapema kwa asilimia 70 hadi 90.

  Kwa sababu hiyo, wanasayansi hao wakahitimisha kwamba maelezo ya Mchungaji Mwasapila kuhusu tiba ya Ukimwi ina ukweli ndani yake.

  Source: Mwananchi
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  lmemponya meneja wangu, alikuwa na kisukari kikali sana kwa siku anachonma sindano sita lakini sasa anachoma sindano moja tu kwa siku.
   
 3. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ingawaje kuna wachache wata claim haijawasaidia, inabidi tukubali kuwa ni kweli dawa hiyo ina uwezo mkubwa
   
 4. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mediaman, njoo jamvini na wewe uje utoe report yako maana kutokana na maelezo yako huko nyuma wewe ni mtu wa Maabara katika hospital ya Mt Meru. Miss judith nasubiri comments zako.
  ingawa bado inachanganya sana kuulewa ukweli kama Babu alioteshwa na Mungu lakini sasa ukweli umeendelea kudhihirika, je babu na yeye alifanya utafiti kama huu au ndio alipewa maono? mimi na wewe hatujui.
   
 5. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Babu hakupitia hizo complication zote ambazo watafiti wanafanya. Yeye alianza kuchemsha na kugawa kikombe kimoja kimoja, bila hata kujua hicho kikombe kina ujazo wa 200ml
   
 6. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Jamani hebu ingieni hapa muone Babu anavyo tukanwa na kudhalilishwa kuwa ni mshirikina mkubwa na wanawataka wenzao wasiende kupata kikombe.
  Www.alhidaaya.com
  Ukiingia search Babu wa loliondo hatufai.
   
 7. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  KunywaKikombe Kimoja Tu = 200ml, waaaooohhhh! God is great hata kwa asiekanyaga shule ya Medicine anajua makadirio sahihi ya Dose

  Be it any how, that is a great step kuelekea kwenye solution muhimu ya magonjwa yenye kutaabisha.....tuwe tu makini na "vijicho" katika kufanya tafiti za undani

  Kikubwa zaidi ni kuhaikisha nchi inanufaika na ugunduzi wa kisayansi utakaofanyika wa dawa hii na wasijenufaika "vijicho" kama ilivyo kawaida yetu
   
 8. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Achana nao, wameshakunywa kikombe sasa wanapiga kelele, kama hawataki si waende wakanywe kile cha morogoro cha mwenzao
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ngoma haijawachanganyia watakuja wenyewe.kama kitimoto wanakifakamia na kila siku wanapiga kelele bado huja wazoea tu.
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Kuna ndugu yangu alikuwa akisumbuliwa na kisukari muda wa miaka kumi na tano hakuna hospital amabyo hajafika ilifika mahali hata heshima ya ndoa ikapuputika kabisa.Tanguatinge Samunge kwa Babu miezi miwili iliyopita afya yake imeboreka sana hatumii tena dawa na misindano ya kila siku uzito umeongezeka mara dufu hata heshima ya ndoa imerejea.Wanaomponda Babu hawajawahi kuugua.
   
 11. wende

  wende JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sure sure sure,,,,wanaomtukana babu, bado hawajapata matatizo ya afya zao na kama wameshapata matatizo,basi naona bado hawajahangaika.....otherwise hao naona wako njiani kuelekea kwa babu Samunge!! Na wakifikia hatua ya kwenda kwa Babu,watajifanya mabubu! Shame upon them....
   
Loading...