Mba kichwani (Dandruff): Fahamu Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Kwa Dar au Mbeya yanapatikana haya mafuta ya maji yanaitwa MPL chini yameandikwa hair oil Original ni mafuta mazuri ya Nywere na ni medicated pia ukitumia siku chache tuu hizo MBA utaziondoa..yanatoka SA na bei yake ni ndogo nadhani hayazidi 5000 kwa madogo..
 
kiafya mba ni fangasi wanaitwa Tinea Capitis. Dawa ni kupiga upara au kutumia shampuu zenye antifungal. Kawaida ukipiga upara huwa wanapotea hata nywele zikirudi ikiwa utakuwa na utunzaji mzuri.
 
Habari wajuvi,

Nikichana nywele kichwani hua panatoa vumbi nilizani labda ni wingi Wa nywele kichwani hivyo basi nikamua kuachana na ufugaji Wa nywele nyingi na kuanza kutumia aina mabalimbali za mafuta yakiwemo mafuta ya Nazi lakini sijaona mabadiliko yoyote.

kama kuna yeyote anayejua jinsi ya kuondoa tatizo hili msaada tafadhali
Una mba za kwenye nywele sasa,nenda kwenye maduka ya vipodozi, watakupa mafuta ya kutumia mba ziishe
 
Saga tangawizi changanya na ndizi au parachichi paka kwenye ngozi ya kichwa kaa nayo kwa muda wa nusu saa osha kichwa chako.

NB: husipake tangawiz bila kuchanganya na tunda mojawapo hapo itakusababishia maumivu.
 
Habari ya asubuhi wana JF kwa wanaofahamu dawa za mba wa kichwani tuelekezane, pili nimeamka sikio likiwa linaniuma sana nashindwi kuelewe tatizo nimelia au la maana hata sielewe kwa mwenye uelewa na hayo mambo mtueleze mimi ni mgeni nimefungua jana account na nimeona watu wanatoa ushauri mzuri asanteni karibuni
 
Dawa ya sikio chemsha mafuta ya nazi au ya zaituni ila bora ya zaituni yakianza kuchemka tia vitunguu somu viache vichemke kwa dakika 5-7 epua subiri yapoe kisha tumia kama njia ya kusafisha sikio
 
Mba kichwani kuchua kitunguu maji kisage upate juisi yake na saga tangawizi upate vijiko viwili juisi yake na asali vijiko viwili tia kichwani fanya massage kisha vaa mfuko wa nailoni nusu saa kisha osha kichwa chako.
Mafuta ya nazi yanaleta mba kichwani acha kutumia tumia mafuta ya mnyonyo,zaituni na parachichi
 
Au pia unaweza kutumia alovera jelly(mshubiri)au limau unasugulia kichwani kisha osha kichwa kwa maji ya uvuguvugu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom