Dawa ya kuzuia ndoa(kuolewa)

Dawa ya kuzuia ndoa(kuolewa)

Habarini wana JF hasa jukwaa hili. nimependa kushare habar hii japo kwa ufupi na nyinyi.

Kuna rafiki yangu wa kiume alikuwa na rafki yake wa kike (mchumba) ambae awali walikubaliana kuwa wataoana. kwa wakati huo miaka mitano imepita kijana alikuwa mfanya kazi binti alikuwa akisoma high school baadae kwenda chuo (education).

Mwaka wa tatu kijana akataka atoe mahali binti akamwambia asubir hadi amalize masomo pia awe ametulia na kazi ndipo process zifanyike.

Kijana aliamua kutafuta msichana aliyetayar kuolewa na akamtaarifu huyo mchumba wake kuwa ameamua kuoa hivyo hayuko tayar kusubir muda wote huo. kijana akaoa hadi sasa hivi anendelea na ndoa yake mchumba wake wa mwanzo akamliza chuo na kupata kazi ya ualimu.

kwa bahati mbaya binti mwalimu hajapata mchumba na anadiliki kumwambia rafik yake(mchumba wa zamani) kamchawia ili asiolewe, hii inawezekana kweli wadau mtu arogwe ili asiolewe?

Wasichana badilikeni bahati hairudii mara mbili mtasingizia mmerogwa kumbe umejiroga mwenyewe.
Ameolewa? Kama bado mwambie aje awe mke wa pili.
 
Back
Top Bottom