Dawa ya chango ni nini?

LENGISHO

Senior Member
Sep 15, 2017
169
245
Wadau naombeni kuuliza dawa ya chango ni nini kwa mzazi ?
Naomban msaada wenu sana
 
Mkuu, dawa ya chango ni dawa. Zipo dawa mbalimbali hospitalini na zile za mitishamba/mizizi. Niliwahi kuambiwa kuwa dawa kuu kuliko zote ni kwa mwenye chango kushika ujauzito.
 
Mkuu, dawa ya chango ni dawa. Zipo dawa mbalimbali hospitalini na zile za mitishamba/mizizi. Niliwahi kuambiwa kuwa dawa kuu kuliko zote ni kwa mwenye chango kushika ujauzito.
Mkuu hapa ndio kajifungua hana hata wiki mbili ...
 
Mkuu, dawa ya chango ni dawa. Zipo dawa mbalimbali hospitalini na zile za mitishamba/mizizi. Niliwahi kuambiwa kuwa dawa kuu kuliko zote ni kwa mwenye chango kushika ujauzito.
Hsushikiki ukiwa nalo ni ngumu kweli na kwa jinsi linavyouma kila mwezi utatamani uzae hata kesho
 
Chango la uzazi baada ya kujifungua⁣

Wanawake wengi wamekuwa wakilalamikia maumivu ya tumbo mara baada ya kujifungua hasa wakati wanapokuwa wananyonyesha. Wenyewe huita chango la uzazi. Hali hiyo ni ya kawaida.⁣

Je hali hiyo husababishwa na nini?⁣
Mara baada ya mama kujifungua mwili wake unakuwa unatoa homoni iiitwayo oxytocin. Homoni hii kazi yake kubwa ni kusaidia maziwa kutoka. Sasa mama anapokuwa ananyonyesha homoni hii inatolewa kwa kiasi kikubwa. Homoni hii inakwenda kwenye mfuko wa uzazi ambako inasababisha mfuko wa uzazi kujikamua. Mfuko wa uzazi unapokuwa unajikamua ndipo unasikia maumivu makali na pia utaona hata damu zinatoka kwa wingi. ⁣

Iwapo unapata maumivu haya unaweza kutumia dawa za maumivu. Mara nyingi maumivu huisha yenyewe baada ya siku kumi.⁣
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom