Dawa ya Babu yazidi kukubalika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya Babu yazidi kukubalika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 4, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Medicinal Plant (TMF) imetoa taarifa ya utafiti wake na kusema dawa ya mchungaji Ambilikile Mwasapila inafaa kutibu magonjwa mbalimbali.
  Taasisi hiyo imetoa taarifa hiyo baada ya kufanya utafiti katika kijiji cha Samunge-Loliondo katika Wilaya ya Ngorongoro nyumbani kwa Mwaisapila.
  Utafiti huo ulifanywa na wataalamu kutoka katika taasisi hiyo, ambao walikaa Samunge kuanzia Januari mpaka Februari mwaka huu na kubaini kuwa tiba hiyo inatibu magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, pumu, shinikizo la damu na mengineyo.
  Alisema walitafiti kwa kukusanya maoni kutoka kwa wakazi wa kijiji hicho pamoja na wao wenyewe kutazama mazingira ya eneo hilo.
  Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa TMF, Marwa Gonzaga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akimtambulisha Mganga wa jadi kutoka kijiji cha Nyamwilolelwa Ingombe wilayani Ilemela, mkoani Mwanza, Mhangwa Kapeji, ambaye anatoa tiba inayoonekana kufanana na ile ya Babu.
  Hata hivyo, alisema hawakupata ushirikiano wa Mwasapila kutokana na imani yake ndipo Machi walipohamia Ilemela kwa Kipeji.
  Alisema wakati wakiendelea na utafiti huo walibaini kuwa tiba hiyo ni mchanganyiko wa mizizi ya miti shamba ya aina mbili ambayo ni ule anaoutumia Babu, kwa jina la kisayansi unaitwa Carissa Spinarum na kwa lugha ya Kisukuma unaitwa Mulo na mti mwingine umefahamika kwa jina la kisukuma la Ntuntwa ndio inapatikana tiba hiyo ya magonjwa sugu.
  Alifafanua kuwa watoa tiba hao wote wawili wanatumia mti wa aina moja ambao ni Carissa Spinarum.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Haya!! Kazi kwenu wanajamii ambao bado hamjatalii kwenye mkoa wa Arusha wenye historia kibao na hata maajabu kutokea na kuibua wengine wenye uchu wa pesa kuibuka Nchini kote. KARIBUNI NGORONGORO YENYE KILA SABABU YA KUTOA MAAJABU DUNIA,iko siku hapo Ngorongoro atatokea na kutoa kali zaidi ya huyo Mchungaji Ambikile Mwasapila 2ombeni uzima tu.
   
 3. Stevemike

  Stevemike Senior Member

  #3
  May 4, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyu wa mwanza anayetumia the same tree, naye haruhusiwi kutoka pale alipo kama babu? Je, naye alioteshwa? Kama ndiyo, na nani? Je, naye anatibu kwa imani maana babu alidai anatibu kwa imani na mwingine akijaribu kutumia mti huo huo hatafanikiwa mpaka yeye tu. Leo mwingine anatumia mti huo huo na kuponyesha!! eh, mtuweke wazi.
   
Loading...